Jimbo la Arusha naliona kama litarudi CCM 2020

Tajiri Tanzanite

JF-Expert Member
Oct 23, 2016
1,051
2,000
Hapo vip!!

Watu wa Arusha ni watu opportunist sana,sasa hivi kwa kauli ya Mh. Dr.Magufuli rais wa jamuhuri wa muungano wa Tanzania kuwaruhusu machinga wafanye biashara katika ya mji naona kama itawashawishi wamachinga waipigie kura CCM.

Kwa uchaguzi mdogo ngazi ya madiwani na jinsi CCM walivyojizolea kata za kutosha ni ishara tosha CHADEMA hawatakuwa salama.

CCM sasa hivi itatumia mbinu yeyote ili mradi watangazwe washindi, so hapa Lema anakazi kubwa mnoo.

Arusha sasa hivi hakuna mikutano ya kimataifa inayofanyika hapa na hii yote kwa sababu ya tofauti za kisiasa.CCM mkiadi kurudisha mikutano ya kimataifa hapa wanaweza wakajizolea kura nyingi sana.

Serikali kama imeisahau mkoa wa Arusha,wakati mkoa huu unachangia pato kubwa la taifa,siasa za namna hii zikiendelea hii mikoa ya kask, inaweza kuja kuwa nyuma kimaendeleo.

Lema ni Mbunge mzuri lakini kwa siasa anazofanya inampa wakati mgumu sana kutoka na nature ya Utawa,uwafrika wetu na nature ya demokrasia tuliyonayo.

Sisi watu wa Arusha tuna msimamo lakini linapokuja swala la maslahi au pesa mtu anakusaliti mchana peupe.

Watu Arusha tumepata fundisho kubwa dhidi ya mabomu yaliyowaua na kuwaachia ndugu zetu vilema vya maisha,kumbe mwisho wa siku zile familia zilizo adhirika zinatelekezwa.

Tunaitaji Arusha ya zamani yenye Neema.
 
Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
23,298
2,000
Kurudi linaweza kurudi hata kwa matokeo ya 100%. Ila ujue wapiga kura hawatorudi kamwe. Ukweli ndio huo
 
mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
6,952
2,000
Kuna majimbo ambayo yatabaki chadema daima. Haya ni mbeya mjini, Arusha mjini, Iringa mjini na moshi mjini! Hata kwa greda haiwezekani!
 
elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
8,439
2,000
Hapo vip!!

Watu wa Arusha ni watu opportunist sana,sasa hivi kwa kauli ya Mh. Dr.Magufuli rais wa jamuhuri wa muungano wa Tanzania kuwaruhusu machinga wafanye biashara katika ya mji naona kama itawashawishi wamachinga waipigie kura CCM.

Kwa uchaguzi mdogo ngazi ya madiwani na jinsi CCM walivyojizolea kata za kutosha ni ishara tosha CHADEMA hawatakuwa salama.

CCM sasa hivi itatumia mbinu yeyote ili mradi watangazwe washindi, so hapa Lema anakazi kubwa mnoo.

Arusha sasa hivi hakuna mikutano ya kimataifa inayofanyika hapa na hii yote kwa sababu ya tofauti za kisiasa.CCM mkiadi kurudisha mikutano ya kimataifa hapa wanaweza wakajizolea kura nyingi sana.

Serikali kama imeisahau mkoa wa Arusha,wakati mkoa huu unachangia pato kubwa la taifa,siasa za namna hii zikiendelea hii mikoa ya kask, inaweza kuja kuwa nyuma kimaendeleo.

Lema ni Mbunge mzuri lakini kwa siasa anazofanya inampa wakati mgumu sana kutoka na nature ya Utawa,uwafrika wetu na nature ya demokrasia tuliyonayo.

Sisi watu wa Arusha tuna msimamo lakini linapokuja swala la maslahi au pesa mtu anakusaliti mchana peupe.

Watu Arusha tumepata fundisho kubwa dhidi ya mabomu yaliyowaua na kuwaachia ndugu zetu vilema vya maisha,kumbe mwisho wa siku zile familia zilizo adhirika zinatelekezwa.

Tunaitaji Arusha ya zamani yenye Neema.
Sio kama, tayari mshindi amepatikana, hawa wengine watakua mahabusu kama wenzao.
 
Malata Junior

JF-Expert Member
Nov 29, 2011
2,999
2,000
Ikulu kuchukuliwa na chadema hilo liko wazi 100%,ccm wachukue tu jimbo la Arusha Mjini maana wanaliona ni kitu cha thamani sana!
 
Twamo

JF-Expert Member
May 27, 2017
2,181
2,000
Siasa za kiafrika za ajabu sana! Badala ya kupigania idadi ya wabunge wa upinzani iongezeke bungeni, ndo kwanza watu wanahangaika ili kuwapunguza! Kisha wanajaza wazee wa ndiyoo! Mimi bado nina Imani na ndugu zangu wa Arusha!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom