Jiji la Dar uchafu umekithiri

Jiji la Dar uchafu umekithiri

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,767
Reaction score
288,340

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Terezya Huvisa, amembana Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Abdallah Chaurembo, kutoa maelezo ni kwa nini wameshindwa kusimamia kampeni ya kuliweka jiji katika hali ya usafi.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa taarifa ya hali ya mazingira ya jiji hilo, Huvisa alisema kutokana na watendaji hao kuzembea katika kusimamia kampeni hiyo iliyozinduliwa hivi karibuni na Makamu wa Rais, ameahidi kuwa hatavumilia hali hiyo bali atawabana.

Alisema amekuwa akipata maswali mengi kutoka kwa Makamu wa Rais kutokana na hali hiyo ya uchafu uliokithiri katika jiji hilo huku watendaji hao wakishindwa kueleza matatizo yanayofanya washindwe kuendesha kampeni hiyo ya usafi inayopaswa kufanyika kila tarehe za mwanzo wa mwezi.

"Unajua mimi ni Rais wa Mazingira Barani Afrika sasa ni aibu kwa Rais kuishi katika jiji chafu kama hili, namwaagiza kila mtu atekeleze kampeni hiyo ya kuliweka jiji hili katika hali ya usafi kinyume chake sitawaelewa," alisema Huvisa.

Aidha, waziri amezitaja wilaya za Kinondoni na Temeke kuwa zimeshindwa kusimamia kampeni hiyo na kufanya kuongoza kwa uchafu katika maeneo mbalimbali.

Huvisa alisema kwa mfano wilaya ya Kinondoni imeshindwa kwa zaidi ya mwaka mzima kuusafisha mtaro wa Mwenge unaotiririsha maji katika mto Mlalakuwa.

Naye Naibu Meya wa jiji hilo, Abdallah Chaurembo, alisema wanazipokea changamoto hizo ambapo hata hivyo, alibainisha kuwa hali hiyo inachangiwa zaidi na ongezeko na ujenzi holela usiofuata taratibu za mipango miji.




[TD="bgcolor: #FFFFFF"]
Naibu Meya abanwa uchafu Dar

na Shehe Semtawa
Tanzania Daima

[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
 
Hamna mji mchafu kama Dsm, Zunguka Tanzania na hata afrika mashariki.

Ukipita kariakoo kunanuka uvundo!!! Mvua ikinyesha maji taka yanatiririka barabarani!
 
Panda treni ya stesheni-ubungo, angalia hali ya uchafu (madampo bubu) maeneo kati ya Matumbi na Mwananchi. Ukifika maeneo ya KAMATA muda wa jioni kila siku kuna watu sijui wanachoma vitugani hapo pembeni ya reli, moshi mzito na harufu kali sana, inatisha!
 
Mataa ya Mnazi mmoja hadi Clock tower (ingawa saa yenyewe ilishakufa siku nyingi), sijawahi kuona hiyo barabara ikiwa kavu hata kipindi cha kiangazi maji ya vyooni toka magorofani yametapakaa barabarani na ndo maana haiishi kuwa na mashimo. Aibu katikati ya jiji.
 
Back
Top Bottom