Jihadharini wanawake Dar es salaam - serial killer on the loose!

Vitambulisho gani viachwe mapokezi wakati nchi haina vitambulisho?

Mtu akisema hana kitambulisho asipewe huduma wakati sheria haimlazimu kuwa nacho?

kweli,labda uyu polisi atwambie kama vitambulisho vya taifa vimeshaaza labda...
tutanyimwa huduma ikiwa ivo sasa
 
Kuna dimension nyingine itakayofanya upelelezi wa kesi hii ulegelege.Nilikuwa naongea na baadhi ya watu nimepata kwamba kinachoongelewa na kutiliwa mkazo sasa ni aibu na kumkinga marehemu na hata jamaa zake na aibu zaidi. Jamii inaona kwamba kutoa ushirikiano katika kufanikisha kumkamata muuaji kutapelekea kufukua mambo yanayoweza kuwaaibisha au kuumiza watu.

Je ni kipi bora? Kutokuficha maradhi upone, au kuficha maradhi kifo kikufichue?
Mi nadhani janga limeshaingia katika jamii hivyo 'tujaribu kusahau" kidogo mambo mengine kama aibu ili kuwapa askari ushirikiano unaotakiwa ili mhalifu huyu au wahalifu hawa wapatikane na haki itendeke.
 
Kuna dimension nyingine itakayofanya upelelezi wa kesi hii ulegelege.Nilikuwa naongea na baadhi ya watu nimepata kwamba kinachoongelewa na kutiliwa mkazo sasa ni aibu na kumkinga marehemu na hata jamaa zake na aibu zaidi. Jamii inaona kwamba kutoa ushirikiano katika kufanikisha kumkamata muuaji kutapelekea kufukua mambo yanayoweza kuwaaibisha au kuumiza watu.

Je ni kipi bora? Kutokuficha maradhi upone, au kuficha maradhi kifo kikufichue?
Mi nadhani janga limeshaingia katika jamii hivyo 'tujaribu kusahau" kidogo mambo mengine kama aibu ili kuwapa askari ushirikiano unaotakiwa ili mhalifu huyu au wahalifu hawa wapatikane na haki itendeke.

Sijaelewa
Ina maana kwenye kesi za jamuhuri kutoa uhsirikiano ni hiari? Yaaaani kama Polisi wanajua mtu fulani anaweza kuwasaidia katia uchunguzi inabidi wambembeleze?

Kwa kuangalia CSI tu unajua ndugu wa karibu mume au rafiki wa mrehemu wanatakiwa kuusaida polisi and at worst case mwanzoni wanaweza kuwa kwenye suspect list. Vitu kama profile a record na profile a mawasiliano yake ya simu siku tatu nyuma kabla ya kifo zinaweza kutoa clue muhimu. Polisi wanaweza kujua kalbla ya siku ya kifo marehemu alitembelea area gani wa msaada wa simu nahiyo yote inaweza uwasaidia.

Au Pia polisi inabidi wawabembeleze Telehone service provider uwaatia info hizo?

Unless Polisi wa Tanzania hawajui kazi yao.
Hapo sio kubembeleza wanataiwa waangalie taratibu zao zinasema nini

Polisi wamesema wateja guest houses waache vitambulisho....
Vitambulisho gani sasa . Mfanya biashara solo au mkulima wa Tanzania ana kitambulisho. Na hata ukiaiwauacha vitambulisho zero brain wapo kuhakisha wanaume na wanawake wanaotaka kusaliti nda zao wanafanikiwa.

Kupata banks statement ya azam na signature ya iikulu sio Kazi sasa ndo ije kitambulisho sijui cha mtaa

Alafu tujiulize lile zoezi la TRCA kusajili number za simu
  • dhumuni na faida zake ni nini?
  • Je tuko hatua gani sasa katika zoezi hilo
  • Kiasi gani kimetumika na kitatumika
  • wananchi tutarajie nini?
 
Serial killer ina defintion zaidi ya moja, kinachoshabihiana ni mauaji ya watu 2 au 3 na zaidi yanayotokea katika muundo fulani yakiwa na motive fulani, mengine yakiwa ni race, sex n.k yote yakiwa na psychological gratification.

Nakubaliana na Nyani Ngabu kuwa hakuna mfumo wa uchoraji wa picha za watuhumiwa kutoka kwa mashahidi,sijui wataalamu wa namna hiyo wapo nchini. Mfumo huo umetumika kwa mafanikio makubwa sehmu nyingi duniani.

Pia mfumo wetu wa kufuatilia kesi za mauaji umekuwa hauendi mbali. Wenzetu wanakitu kinaitwa cold case na hizo hufuatiliwa hata miaka 40 na zaidi hadi chanzo cha tukio kitakapopatikana. Sisi kesi inafungwa baada ya mazishi na hasa kama tukio linamhusu mtanzania wa kawaida tu.

Kama detective polisi wetu wangekuwa makini wangeweza kushirikiana na wenye nyumba za wageni na sasa wangekuwa na clue. Kutoa onyo kuwa huwa anavaa kapelo ni njia rahisi ya kumshauri asivae na kuendelea kuuhadaa umma.Wanatakiwa wafanye kazi kitaalamu zaidi.

Kuweka CCTV ni ngumu kwasababu ya 'privacy'. Sio wote wanaoingia guest ni wahalifu. Wapo wasafiri na hata wana ndoa walioamua kuwa mbali kidogo ili kuziimarisha ndoa zao kwa namna moja au nyingine.Wapo waliokwenda kwa kwa ajili ya usalama wao hasa baada ya vinywaji, dansi au madisco. Je hawa tutalindaje 'privacy' yao. Mfumo wa CCTV una namna ya ku monitor kulinda haki za kila mmoja.

Vitambulisho hatuna vya kitaifa. Kama vitatumika basi kutakuwa na vya kuchonga vingi tu kariakoo na hapa ni dili kwa watu bila kupata ufumbuzi. Kama cheti kinaweza kufojiwa sijui kitambulisho itakuwaje. Hatutawatendea haki baadhi ndugu zetu kutoka matombo au Lushoto walioleta bidhaa zao kwani hawana vitambulisho.

Jamii ielewe kuwa mke wa mtu anapofia guest hapo hakuna siri, ni vema kutoa ushirikiano kwa vyombo husika tukielewa huyu ni nyoka na yupo ukumbini kudhuru patakapotugusa tena.Nadhani kuna uhusiano mkubwa wa marehemu na muuaji, haiwezekani ajue kuwa ni wake za watu bila kuwafahamu awali na yawezakuwa wapo ndugu au marafiki wanaoweza kutoa dokezo, hao ndio wanatakiwa kutoa ushirikiano.

Tutakosea kama tutasema linahusu wanawake wasio waaminifu. Hatujui motive ya muuaji ni nini. Yaweza kuwa ni ushirikina na je kama dhima yake ni hiyo watakapokosekana anao wataka haitawezekana kurejea kwa mabinti. Hatujui kwanini anafanya hivyo. Huu si utetezi kwa wazinzi la hasha! ni kutojisahau kuwa linaweza kuchukua mkondo mwingine.
Na je huu si ushahidi kuwa as much as kuna mibaba mikware kuna mimama viwembe? na kwamba uzinzi ni hulka na si jinsia!!!
 
Back
Top Bottom