Jihadhari na tapeli huyu

Simba Mkali

JF-Expert Member
Jan 31, 2012
620
239
Binafsi ni mtoto wa mjini ambaye ninajua kuwa si rahisi kupata fedha kirahisi, kuna tapeli mmoja alinipigia simu na kunitaja jina langu kwa ukamilifu, akajifanya yuko Arusha kwenye mbuga za wanyama akanitaka eti ninunue madawa kutoka DFP pale Tazara kwa kuwa wakala wake wa zamani hayupo hapa mjini. Akasema eti kuna dolla kibao zitapatikana kwa kuwa hayo madawa nitawauzia wazungu ambao tutaenda mimi wakala wa kuuza madawa hayo Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, kisha tutaenda Kilimanjaro Hoteli kugawana dolla hizo.
Tahadhari kwa watu wamuogope tapeli huyu mwenye namba 0717 302481 kwa kuwa jamaa ni fundi sana wa kuongea na anajua vitu vingi sana, kwa jinsi inavyonekana anaishi jijini Dar lakini ni mjanja mjanja anayejua kupangilia maneno kwa ufundi mkubwa.
Ninachojiuliza inakuwaje anatumia namba hii kwa kutapeli watu na asikamatwe? Je namba yake haijasajiliwa? Hebu watu wa Tigo wamfutilie na kumuumbua ni hatari sana.
 
Aaaah namjua huyo jamaa! na hii Thready ilishawahi letwa hapa kitambo hapa! Lakini asante haibiwi mtu hapa!
 
Binafsi ni mtoto wa mjini ambaye ninajua kuwa si rahisi kupata fedha kirahisi, kuna tapeli mmoja alinipigia simu na kunitaja jina langu kwa ukamilifu, akajifanya yuko Arusha kwenye mbuga za wanyama akanitaka eti ninunue madawa kutoka DFP pale Tazara kwa kuwa wakala wake wa zamani hayupo hapa mjini. Akasema eti kuna dolla kibao zitapatikana kwa kuwa hayo madawa nitawauzia wazungu ambao tutaenda mimi wakala wa kuuza madawa hayo Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, kisha tutaenda Kilimanjaro Hoteli kugawana dolla hizo.
Tahadhari kwa watu wamuogope tapeli huyu mwenye namba 0717 302481 kwa kuwa jamaa ni fundi sana wa kuongea na anajua vitu vingi sana, kwa jinsi inavyonekana anaishi jijini Dar lakini ni mjanja mjanja anayejua kupangilia maneno kwa ufundi mkubwa.
Ninachojiuliza inakuwaje anatumia namba hii kwa kutapeli watu na asikamatwe? Je namba yake haijasajiliwa? Hebu watu wa Tigo wamfutilie na kumuumbua ni hatari sana.

Ukitaka kumjua mmiliki wa namba ya simu
ingia garama ya kumtumia pesa kwenye simu
yake kama 500 hivi itakupa particulars za mwenye namba
 
Back
Top Bottom