Jihadhari na tapeli huyu anayejifanya kuuza pikipiki na vifaa vya pikipiki

specialist88

JF-Expert Member
Aug 31, 2014
1,141
617


Huyu ni tapeli mkubwa, anatapeli watu kwa kujifanya anauza piki piki na vifaa vya pikipiki.

Akishakutapeli anakublock ili usilalamike kwenye page yake ya instagram.

Lengo la kuleta taarifa hizi ni kuwatahadharisha wananchi wenzangu na kutoa call kwa polisi au vyombo vya dola vimfuatilie na kumtia nguvuni tapeli huyu.

Huyu tapeli anatumia namba 0625933983 na pia anapokea pesa kupitia namba 0719255409 jina Mary mboya.

Tushirikiane kutokomeza utapeli wa mitandaoni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Du hawa watu wanafanikiwaje kukamilisha uhalifu huu bila kukamatwa.ina maana hata mamraka zetu zina lala sana.yaani kama TRA na zingiezo.nilidhani matangazo kama haya ni kuyafuatilia kabla hayajafikia mbali.yaani ilitakiwa tahadhali kama hizi tuwe tunapewa na polisi au vyombo vya serikali.

matukio ya kihalifu ya kimttandao bado naona yameizidi nguvu serikali

Yaani kwa karne hii wuzi uliopo sio ule wa kupora physical cash bali ni kuiba hela kidigitali
 
Mboya mchaga huyo..
Kwaiyo aki kublock ndio huwezi kugoa taarifa police au unapenda kuweka comments kwenye page yake..
Elezea kwanza amekutapeli vipi? Mbona sio rahisi
 
Kamtapeli nani? ,katapeli nini?, katapeli vipi?
Isije ukawa una tatizo lako binafsi na yeye unamchafua hapa jukwaani

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu amini ninachokuambia. Sifanyi biashara kama yake au nina chuki naye. Ninakuambia ukweli ambao umetokea. Hata wewe jaribu kupiga simu uone reaction yake,anaweza asipokee simu hata siku nzima akidhani ni mtu aliyekutapeli umebadilisha namba. Hapokei simu kwa wakati na vitu kama hivyo. Pia naomba nikuwekee screenshot ya chart yake na mtu aliyemtapeli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kamtapeli nani? ,katapeli nini?, katapeli vipi?
Isije ukawa una tatizo lako binafsi na yeye unamchafua hapa jukwaani

Sent using Jamii Forums mobile app
Mpaka leo hajarudisha pesa na amemmblock huyo mteja wake kwenye ukurasa wake wa instagram, huyu ni mwizi mkubwa naomba vyombo vya dola viwasaidie watu ili asiendelee kutapeli watu wengine. Najua kuna watu watasema katoe taarifa polisi hapa sio polisi ila naomba waelewe kuwa taarifa za mitandaoni zinatakiwa kuwa alarm kwa jeshi la polisi na sio kila mtu akienda kutoa taarifa polisi kituoni basi hufanyiwa kazi kwa uharaka zaidi ya kuletewa usumbufu tu na baadhi ya polisi wasiojua wajibu wao. Kama nikihitajika kutoa ushahidi, nipo tayari.
Screenshot_2019-04-13-02-33-49-878_com.android.mms.jpeg
Screenshot_2019-04-13-02-34-13-749_com.android.mms.jpeg
Screenshot_2019-04-13-02-34-31-610_com.android.mms.jpeg
Screenshot_2019-04-13-02-34-36-875_com.android.mms.jpeg
Screenshot_2019-04-13-02-35-56-267_com.whatsapp.jpeg
Screenshot_2019-04-13-02-36-06-425_com.whatsapp.jpeg
Screenshot_2019-04-13-02-36-13-049_com.whatsapp.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Du hawa watu wanafanikiwaje kukamilisha uhalifu huu bila kukamatwa.ina maana hata mamraka zetu zina lala sana.yaani kama TRA na zingiezo.nilidhani matangazo kama haya ni kuyafuatilia kabla hayajafikia mbali.yaani ilitakiwa tahadhali kama hizi tuwe tunapewa na polisi au vyombo vya serikali.

matukio ya kihalifu ya kimttandao bado naona yameizidi nguvu serikali

Yaani kwa karne hii wuzi uliopo sio ule wa kupora physical cash bali ni kuiba hela kidigitali
Hili swala linashangaza sana, kuna watu wapo maofisini hawawajibiki hata kidogo mpaka wasukumwe na vigogo ila wananchi wakawaida ni mara chache kushughulikia kero zetu. Mpaka mkubwa aseme. Hii inaumiza sana na mtu kama huyu anatapeli watu weeengi kila siku. Lakini yupo tu anadunda na atakumia laini za simu. Niliomba mshikaji mmoja aniangalizie taarifa zake alizotumia kusajilia laini hiyo ya tigo inayopokea pesa huwezi amini alichoniambia, aliniambia huyo jamaa hana taarifa wala document yoyote. Sasa inawezekanaje mtu atumie laini bila kuwa na documents kama kitambulisho chake, picha au leseni alizotumia kusajilia. TCRA wawajibike sio kukaa maofisini kusubiria amri za vigogo tu. Watu kama TCRA wanaifanya serikali ionekane haifanyi kazi. Hata hapa watasoma na watapita kimya tu. Inakera sana hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom