Jihadhari na mawakala wanaosajili laini mtaani

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
Habarini ndugu zangu,

Ndugu zangu napenda niwafahamishe style mpya ya mawakala wakusajili line za simu.

Jamaa yangu ukienda kwa wakala kusajili line yako sasa hivi wanakupiga picha mara 3 na wanakusainisha dole gumba mara 3. Hivyo inawawezesha wao kukusajilia line 3 bila wewe kujua.

Ukishaondoka na line yako moja hizi zingine Wanauza tena mara nyingi huwauzia watu wanaoonekana wa vijijini wasiojua kusoma na wale wasiokuwa na vitambulisho vya Uraia.

Hili jambo ni hatari kwa sababu huyo aliyeuziwa line hiyo akifanya tukio baya utatafutwa na kukamatwa wewe.

Hizo line huuzwa Sh 5000 hadi 3000. Unaambiwa zishasajiliwa kila kitu lipia usepe nayo.

Hii ni tahadhari kwenu ndugu zangu nawapenda sana.
 
Tatizo hili linajulikana makampuni ya mitandao wanawachukulia hatua gani hawa mawakala wanao kwenda kinyume na maelekezo ya serikali?. Pia mamlaka ya mawasiliano imejipanga vp kwenye hizi changamoto pasipo kumuathiri aliye futa matakwa ya serikali?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wa kulaumiwa hapa ni NIDA na serikali.Vitambulisho mpaka unachoka,wao watusaidie tu.Liwalo na liwe huko mbele ya safari.Pita haraka usepe zako bwana.
 
Back
Top Bottom