TCRA na usajili wa laini kwa alama za vidole

TCRA na usajili wa laini kwa alama za vidole

Vitalis Msungwite

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2014
Posts
3,318
Reaction score
7,985
Juzi nilipata tetesi kutoka group moja la WhatsApp kuwa kuna zoezi la kuthibitisha usajili kwa kuweka alama za vidole.

Leo nimepata ujumbe ufuatao toka kwenye lain yangu ya vodacom.

MUHIMU: Ndugu Mteja, kuanzia Tarehe 1 Mei unatakiwa Kusajili UPYA laini yako kwa mfumo wa alama za vidole. Tembelea duka letu na kitambulisho cha Taifa au namba ya NIDA

Updates

Kupata namba ya kitambulisho unapiga *152*00# chagua 3 kisha NIDA kisha fuata maelekezo, ghalama ni Tsh 100. Lakini inaonekana 100 wanafyeka na majibu wanasema taarifa hazipatikani. Binafsi ninacho na nimewachangia 100 lakini majibu ni hayohayo.

Mtandao wa Vodacom utatoa vifaa kwa mawakala wa usajili, hivyo huduma itawafikia mlipo. Na zoezi litaenda mpaka mwezi wa tisa.

Related Comments

ZEE LA HEKIMA
TCRA Tafadhalini !! Please !!Juzi CAG alitoa ripoti kwamba ni watu MILIONI NNE TU nchi nzima ndio vitambulisho vyao vilitoka kati ya maombi ZAIDI YA MILIONI 19 !! Sasa leo TCRA mnasema tuende na vitambulisho vipi vya NIDA? Haya !! Sisi watoto tulimpa simu mama yetu kule kijijini ili tuwe tunamtumia pesa kila mwezi. Akitaka kwenda kuandikisha alama zake za vidole lazima afunge safari mpaka mjini. Nauli kwenda na kurudi elfu 15, na hiyo safari akiwa mwenyewe hataweza kwa sababu ya uzee.
Akiweza kufika kwenye ofisi husika mnataka akakae kwenye foleni ili kujiandikisha? Na kesho na keshokutwa arudi tena kama hajafanikiwa siku hiyo kwa sababu ya foleni? Are you serious? Mkifunga hizo simu za mamilioni hayo ya watu wenye line za simu (ambazo zinakisiwa kuwa zaidi ya milioni 20), serikali si itakosa mapato mengi sana ya kufanya miamala na kodi kila mwenye simu anaponunua vocha? Kwa nini msijipange mshirikiane na tume ya uchaguzi ili tume ipange muda wa kuhuisha au kusajili vitambulisho vipya na wakati huo huo uwe ndio wa kuchukua alama za vidole kwa ajili ya simu? Mmeshafikiria masaa ya kazi yatakayopotea wakati watu wote watakapoenda kuandikisha alama za vidole?

Kertel
hiyo ni biashara ili serikali ipate mapato kupitia namba za vitambulisho vya taifa,msg inasema kama huna kitambulisho cha taifa basi nenda na namba ya kitambulisho cha taifa,kuipata namba ya kitambulisho unalipia tsh 100,haya hiyo msg imetumwa kwa wangapi na wangapi wana vitambulisho vya taifa nchi hii. Tupige hesabu ndogo tu

100×19,000,000,000 = 1,900,000,000,000.

Kwahiyo wataingiza billion 1 na million 900. Hapo utaambiwa taarifa hazipatikani, na mtu unaweza kukomaa hata Mara 5 ili tu upate hizo namba.
 
Mimi nilipata 2015 Iringa, lakini huku home wilaya nzima wenye NIDA hatufiki 2,000
hiyo NIDA imekizi kila mtu kupata kitambulisho.mbona tunachekeshana mchana wakati wa jua kali.

Barafu la moto
 
hiyo ni biashara ili serikali ipate mapato kupitia namba za vitambulisho vya taifa,msg inasema kama huna kitambulisho cha taifa basi nenda na namba ya kitambulisho cha taifa,kuipata namba ya kitambulisho unalipia tsh 100,haya hiyo msg imetumwa kwa wangapi na wangapi wana vitambulisho vya taifa nchi hii.
 
hiyo ni biashara ili serikali ipate mapato kupitia namba za vitambulisho vya taifa,msg inasema kama huna kitambulisho cha taifa basi nenda na namba ya kitambulisho cha taifa,kuipata namba ya kitambulisho unalipia tsh 100,haya hiyo msg imetumwa kwa wangapi na wangapi wana vitambulisho vya taifa nchi hii.
Wewe umewaza mbali sana, sikulifikiria hili kabisaaa

Barafu la moto
 
Back
Top Bottom