Jihadhari na aina mpya ya wizi wa simu

Mkaa Mweupe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
654
183
Baada ya kusikika habari kuwa kuna mwanamke aliuwawa kule mwanza kwa kosa la kuiba simu, kweli nilisikitika kuwa pengine alikuwa ameonewa sana. Lakini sasa nimepata kujua kuwa kuuwawa kwake ni sawa tu na vibaka wengine.

Imenigusa kufikia uamuzi huu baada ya kugundua kuwa kwa sasa wanawake wadogo wadogo ndio wamekuwa vibaka maarufu wa simu za mikononi.

Katika tukio moja lililotokea hivi karibuni, binti mmoja mtanashati alikwenda kumuazima simu kijana mmoja mjasiria mali katika biashara zake kwa madai kuwa simu yake imekwisha chaji na kuna simu muhimu anataka kupiga ili aweze kukutana na mwenyeji wake katika mitaa hiyo. Yule kijana kwa uelewa wake alimjibu kuwa pale mbele kuna kibanda unaweza kwenda kupiga. Binti akasema kuwa hakuwa na hela ila line yake ina hela na kusisitiza kuazimwa simu. Kijana akamuelewa na kumpatia TZS 500 ili akapige hiyo simu pale kibandani.

Binti alipoke ile pesa na kwenda kuvunga pale kibandani pasi na kupiga simu kama alivyodai. Baada ya muda yule binti alirejea tena maeneo yale ya mjasiriamali (Shoe shine) pasi na kujua kuwa yule aliyempatia ile TZS 500 ndio mmiliki wa ile sehemu. Kijana alikuwepo pale ila alikuwa amegeukia nyuma. Binti alipofika alirudia maneno yale yale kwa mteja mwingine akimwomba amuazime simu yake. Mjasiriamali aliposikia yale maneno aligeuka na kumweleza yule binti, "Si nilikupatia hela uwasiliane? Imekuwaje tena?". Binti aliposikia alishtuka na kuingia mitini.

Katika tukio jingine kuna binti mdogo (miaka kati ya 10 na 12) alitumiwa na vibaka kwenda kuazima simu kwa mzee mmoja ili aweze kuwasiliana na ndugu yake. Mzee bila hiyana alimpatia ile simu. Hamadi yule binti aliposema tu "Hallo!", alitokea kibaka ambaye alimpora simu yule binti na kutokomea nayo.

Tahadhari: Tuendelee kuishi kwa amani ila tusiwe na imani na kila tumwonae, dunia imeharibika!
 
Mimi juzi nimewapa lift wanafunzi tisa wa sekondari moja,nilipofika mwisho wa safari yao nikagundua simu yangu moja imeibwa kutoka ktk dashboard.Nikasimama ghafla na kutoa vitisho kuwa nitawapeleka polisi ndipo mmoja wao akasema mwenzie aliyekaa kiti cha mbele ndiye aliyechukua.Nikateremka garini na kutaka kutoa kisago,yule kijana akaidondosha ile simu.Kwakweli nilihudhunika sana kwa hali ile yaani natoa msaada tena unageuka karaha!Nimeamini why watu wengi wenye magari binafsi hawataki kusaidia watu barabarani kutokana na matatizo kama hayo.Jihadharini jamani!
 
When people with sufficient, regular and legal income are less than 30% u can expect more than that really. Mvurugano wa kiuchumi unasababisha breaking -down ya mifumo ya kijamii, ndio maana kuna mfumuko mkubwa wa watoto wa mitaani, magonjwa, uhalifu, na kadhia nyengine zinazoindicate kwamba jamii yetu ni GONJWA. With time hali itazidi kuwa mbaya maana hakuna counter-matching ya hizi changamoto.
 
Hahahahaha hii kali sana! Kuna nilikuwa narudi home baada ya misele pale mjini, kupita karibu na water front lile jengo la NSSF nilisimamishwa na polisi wawili. NIliposimama waliniomba lifti wanakwenda mtoni Mtongani, nami nilikuwa naenda njia hiyo. Nikawabeba tukawa tunakata storiez, walipofika nikawatelemsha. Kumbe waliuposhuka waliteremka na Nyama yangu Kg 3 na chupa za maji bahati nzuri laptop niliihamishia mbele. Nafika home nashusha mizigo ndipo nilipogundua.....mdogo wangu akaniambia polisi ndo zao hizo ukiwabeba hamishia vitu kwenye boot! Polisi anayeiba Kg 3 za nyama unategemea atakwepa rushwa ya 2000?
 
kazi po tena kubwa haswaa...
 
Pole sana muzee! Hiyo ndo bongo, mtu anakutoa roho kwa ajili ya 500 na traffic anaweza kupokea hata book. Kila 3 nyama ni karibia 15000/-. Pia inawezekana jamaa alionja nyama siku kuu ya pasaka!

Mbombo ngafu malafyale!!
 
Kumbe waliuposhuka waliteremka na Nyama yangu Kg 3 na chupa za maji bahati nzuri laptop niliihamishia mbele. Nafika home nashusha mizigo ndipo nilipogundua.....mdogo wangu akaniambia polisi ndo zao hizo ukiwabeba hamishia vitu kwenye boot! Polisi anayeiba Kg 3 za nyama unategemea atakwepa rushwa ya 2000?

Hahahahaha umenichekesha sana mpaka umenipandisha kiu ngoja nikale kachupa kamoja.
Ulikosea ulishindwa hata kuwapa buku 2 wagawane angalau wapate Mountain Dew,
Pole mzee bora kama haikuwa nyama ya mbuzi au Mwanaharamu.
 
Valuer nilikuwa nazo kwa mbele kwenye dash board wale jamaa noma!
 
Hii mbona kawaida sana hayajakukuta tuu. Watu wameshabamizwa za uso mara kibao. siki hizi hata ukinunua vocha ya sm binti anasimama nyuma yako alfu wakati unaingiza namba na yeye anaingiza kwake fasta wakati unamaliza ukibonyeza reli na kitufe cha kijamini una pata ujumbe vocha hii imeshatumika.
 
Hahahahaha hii kali sana! Kuna nilikuwa narudi home baada ya misele pale mjini, kupita karibu na water front lile jengo la NSSF nilisimamishwa na polisi wawili. NIliposimama waliniomba lifti wanakwenda mtoni Mtongani, nami nilikuwa naenda njia hiyo. Nikawabeba tukawa tunakata storiez, walipofika nikawatelemsha. Kumbe waliuposhuka waliteremka na Nyama yangu Kg 3 na chupa za maji bahati nzuri laptop niliihamishia mbele. Nafika home nashusha mizigo ndipo nilipogundua.....mdogo wangu akaniambia polisi ndo zao hizo ukiwabeba hamishia vitu kwenye boot! Polisi anayeiba Kg 3 za nyama unategemea atakwepa rushwa ya 2000?
Masanilo,Umenikumbusha machungu-aaagh!Nilisimamishwa na trafiki kuwa kuna kizee kinataka lift kwenda mjini,pamoja na uchovu wa safari natoka mkoani,nikakubali.Mbele nilikuwa na vitu kibao,nyuma nimeweka koti ndani lina simu na pochi ina docs tu.
Nikakieleza kizee kikae nyuma maana kilikuwa na barakashia na kifimbo, nikajua huyu tena akiiba basi twende kazini.Simu nilikuwa nimeizima kwa sababu nisingeweza kuzipokea.Kuingia Ubungo huruma ikanituma,nikakiuliza kwani unaelekea wapi babu?Kikasema posta mwanangu.
Kwa sababu nilikuwa nafikia mitaa hiyo, nikakiteremsha posta ya zamani. Nikaenda mbele kidogo nikaamua kuwasha simu-hamna kitu,kuangalia pochi haipo, nikarudi pale posta ya zamani,nikakikuta ndio kinaelekea upande mwingine wa mabasi,nikamwambia mzee samahani inabidi niku search nikikuta huna ninachokitafuta nitakulipa tu. Kuanza mfuko wa kwanza nakutana na pochi, kuingia kwenye kanzu nakuta simu, nikaaapa labda awe baba yangu mzazi!:angry:
 
Mpwa pole sana ....ila walau wewe uliweza mwona huyo babu Kanzu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom