Jihadhari! Google wanakujua kuliko mama yako

Papa Mobimba

JF-Expert Member
Dec 6, 2018
1,153
1,359
Si ajabu ukiulizwa leo hii nani anayekufahamu zaidi. Jibu linaweza kuwa mama yako au mpenzi wako.

Sasa kwa taarifa yako kama ulikuwa hujui, Google wanakujua zaidi kuliko mtu yeyote mwingine. Google wanajua kuanzia kuamka kwako, kulala kwako, mazungumzo yako, sehemu ulipo sahihi na hata ukitoka hapo watajua. Google wanajua karibu kila kitu kuhusu wewe. Wanajua unachofanya kwenye mtandao. Wanajua kuanzia muda unaotumia kuangalia porn, muda unaotumia kutazama video YouTube, ugomvi wako na mkeo. Sijui niseme ambacho Google hawajui kuhusu. Nafikiri hakuna.

Hatua hiyo ya kampuni ya Google kuhifadhi taarifa za siri za wateja imesababisha CEO wa Google kuitwa na kuhojiwa na Congress ya Marekani. Tuhuma kama hizo zimeikabili kampuni ya Facebook pia.

Kwahiyo hapo ulipo Google wanakucheki wanachekaa! Ni muhimu kuchukua tahadhari kuzima data, location, WIFI, BLUETOOTH unapokuwa sirini!

Tazama kibano alicho pewa CEO wa Google kutoka kwa Congress
 
ishi zako kama osama ukitaka kuwasiliana unatumia codes tu kwenye kipande cha karatasi

mtu wako wa karibu akitaka kuwasiliana inabidi atoke labda tuseme mwanza aitafute chato ndipo apige simu na akimaliza...
 
Ila hawa jamaa wajirekebishe, masuala unagoogle kitu yanaanza maneno ya ajabu hatutaki.

Mfano unataka kugoogle neno kutohoa , ukianza kutype kuto .... utaona maneno yanayokuja hapo halafu mbaya zaidi umekaa na mtoto.
 
ishi zako kama osama ukitaka kuwasiliana unatumia codes tu kwenye kipande cha karatasi

mtu wako wa karibu akitaka kuwasiliana inabidi atoke labda tuseme mwanza aitafute chato ndipo apige simu na akimaliza...
Labda Wamarekani waibane isiwe inahifadhi kila information za watumiaji
 
Back
Top Bottom