Jifunze tofauti kati ya display za AMOLED na LCD

Jifunze tofauti kati ya display za AMOLED na LCD

Strictly Syrup

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2013
Posts
1,227
Reaction score
1,821
Display.jpg


Habari zenu Ndugu wana-JF,

Nimeamua kuandika article hii kutokana na kuona thread ya mtu mmoja akitaka kujua tofauti kati ya display za AMOLED na LCD. Hizi ni display za kisasa zenye ubora wa hali ya juu, ukilinganisha na display za kawaida. Yaani ni kama exclusive kwa kuwa huwezi kukuta display hizi katika simu za bei ya kawaida. Nitaainisha tofauti zake.

LCD:
Display hii inafahamika kama "Liquid Crystal Display" LCD ni abbreviation tu. Kama jina linavyojitaja, display hii imetengenezwa na liquid crystals ambazo zikutana na mwanga zinatengeneza rangi halisi na zenye mvuto. Lakini LCD haipo vizuri katika kutengeneza realistic black. (Yaani rangi nyeusi inakuwa brighter kidogo. LCD inatumia teknolojia mpya iitwayo IPS (In-Pane Switching) ambayo inaboresha muonekano wa rangi na unakuwa unaexperience viewing agles zenye muonekano thabiti. Sifa kubwa ya LCD ni uwezo wake wa kudumi zaidi.

AMOLED:

AMOLED (Active Matrix Organic Light Emitting Diode) ni teknolojia iliyojipatia umaarufu mkubwa sana kwa miaka ya karibuni, display hii utikuta sana katika Samsung Smartphones ama Nokia. Simu kama Nokia N8, Lumia 820 ni baadhi ya Nokia zinazotumia display za AMOLED, pia Samsung ndiyo wamekuwa watumiaji wakubwa wa AMOLED displays. Screen za amoled zimetengeezwa kwa gamba lenye molecules nyingi ambazo zinatoa mwanga endapo zikikutana na mkondo wa umeme. Teknolojia hii rahisi ya amoled imeweza kutumika kufanya matengenezo ya screen nyembamba ambazo hazihitaji backlight. Kwa mantiki hii, AMOLED screens zinakuwa zinazalisha rangi nyeusi amabayo ni nzito sana, yaani inakuwa imekolea kiasi kwamba pixels za mwanga hazihitaji kutumika wakati kwa sehemu zote zenye rangi nyeusi zinapoonekana kwenye picha wakati unapotumia simu yako. Na hii ni sababu kubwa ya simu zenye AMOLED screen kupunguza matumizi makubwa ya battery. Pia kuna Amoled iliyoboreshwa zaidi iitwayo Super Amoled ambayo utaikuta kwenye devices za hadhi ya juu.

Learn-everythin9076.jpg


FAIDA: AMOLED.

• Display hii ina contrast ya kiwango cha juu.

• Ina rangi nzuri iliyokolea (Saturated colors)

• Ina rangi ambazo zinavutia kwa macho yako.

• Bado ni technolojia mpya ambayo inaendelea kukua na improvements nyingi zitafanyika kuongeza ubora.
• Inarespond kwa haraka sana, katika activities za mtumiaji.

FAIDA : IPS


• Ni technolojia kongwe, kwa hiyo ina asilimia kubwa ya kuendelezwa.

• Ina zalisha rangi halisi kabisa (kasoro black ambayo inakuwa inaonekana kama grey)

• Inazalisha mwanga mkubwa zaidi.

• Ni muhimu kutumika mahali popote (kwa kuwa hata sehemu kama juani, bado utaona vyema.

HASARA: AMOLED.
Hasara kubwa ya kutumia device yenye AMOLED ni kwamba ina limited lifetime (ambayo ni miaka mitano) screen hizi huweza kuchoka mapema iwapo mtumiaji atakuwa anatumia screen kwa maximum brightness, ambayo husababisha light pixels kuchoka mapema. Lakini hili lisikue wasiwasi kutokana kuwa Amoled technology bado ni mpya na inazidi kukua, hivyo maboresho yataongezeka maradufu.

HASARA: LCD
Hasara kubwa ya LCD ni kuwa inatumia kiasi kikubwa cha umeme kutokana na kutumia technology backlight kuongeza mwanga zaidi katika screen. Pia LCD ni technolojia kongwe hivyo hakuna haja ya kutegemea maboresho mengi (Maboresho makubwa hayatatokea, labda madogomadogo tu).
 
Unagundua vipi kuwa screen hii ni LCD au a
AMOLED

AMOLED inagundulika kirahisi sana kwa macho, kama nilivyoeleza kuwa haihitaji backlight, na pia ukilinganisha na simu za kawaida, AMOLED inakuwa imekolea rangi sana. Na pia AMOLED display zinazalisha rangi nyeusi halisi. Tofauti na display nyingine.
 
Unagundua vipi kuwa screen hii ni LCD au a
AMOLED

Kabla ya kununua smartphone, i browse kwenye mtandao, soma specs zake, huwa wanaandika kioo ni cha teknolojia gani. Kwa mfano simu ninayotumia, teknolojia ya display type ni Thin-film-transistor (TFT). TFT ni aina ya LCD display ambayo imeboreshwa hasa kwenye contrast
 
Mtu anahitaji kuona LCD na AMOLED ili aweze kufanya comparison vinginevyo nadhani ni rahisi kukosea kwa mtu mgeni!!

you're right. most iPhones are IPS LCD na Samsungs are AMOLED, so mtu achukue high ends device za Samsung kisha aifananishe na Apple device, especially iPhone
 
Hakuna app kwa ya thems au kupata huo mwanga wa lcd au amoled kwa sisi watumiaji wa tecno, infinix maana huwa natamani sana kamwanga katamu. Kwenye techo yangu ila baishia kuiona kwa Samsung tu nateseka nitafurahi sana nikipata app
you're right. most iPhones are IPS LCD na Samsungs are AMOLED, so mtu achukue high ends device za Samsung kisha aifananishe na Apple device, especially iPhone
 
Wazee hili swali langu hamlioni au mnalipotezea naomba kujua hamna app inayoweza kutusaidia hata sisi wa techno tupate huu utamu wa hii displays au thems
Hakuna app kwa ya thems au kupata huo mwanga wa lcd au amoled kwa sisi watumiaji wa tecno, infinix maana huwa natamani sana kamwanga katamu. Kwenye techo yangu ila baishia kuiona kwa Samsung tu nateseka nitafurahi sana nikipata app
 
Mzee kwa kifupi hakuna,hyo ni tecnology ya vioo.ndo km ulinganishe quality ya movie ya 480p na 1080p
Wazee hili swali langu hamlioni au mnalipotezea naomba kujua hamna app inayoweza kutusaidia hata sisi wa techno tupate huu utamu wa hii displays au thems
 
Back
Top Bottom