Jifunze sayansi ya kiafrika

Jifunze sayansi ya kiafrika

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
19,899
Reaction score
37,699
JIFUNZE SAYANSI YA KIAFRIKA

UNGO AFRIKA ni taasisi inayo jihusisha na masuala ya utamaduni,mila na desturi za kiafrika . Tunapenda kuwatangazia watu wote kuwa tunatoa kozi maalumu ya kujifunza kozi iitwayo " SAYANSI YA KIAFRIKA". Katika kozi hii utajifunza namna ya kutumia NGUVU YA SAYANSI YA KIAFRIKA katika kukabiliana na masuala mbalimbali yanayo zunguka maisha ya kila siku ya mwanadamu kama vile (mapenzi/mahusiano, ndoa), biashara, kazi, ulinzi na magonjwa.

Tunapatikana jijini Dar Es salaam, na tunao wataalamu walio bobea katika sayansi ya kiafrika kutoka katika makabila yote ya Tanzania bara na visiwani. Wataalamu wetu wana ujuzi na uzoefu wa SAYANSI YA ASILI kutoka katika mataifa yote ya kiafrika,Arabuni na India.
Tupo jijini Dar Es salaam.
Masomo kuanza, tarehe 01 OKTOBA 2013
Kujiandikisha, tuandikie kupitia barua yetu : ungoafrika@gmail.com

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 25 SEPTEMBA 2013.
WAZUNGU WANAITA UCHAWI, LAKINI SISI TUNAITA, " SAYANSI YA KIAFRIKA"

KWA PAMOJA TUUNGANE KATIKA KULINDA NA KUENDELEZA, MILA,DESTURI NA TAMADUNI ZA MWAFRIKA.
 
kozi ya kuruka na ungo itakuwepo.........?....kama ipo bei ni kiasi gani........?
 
Watu gan mashuhuri wametoka katika mafunzo yenu kama mfano tu ili tujiridhshe na mafunzo kabla hatujajiunga?
 
Watu gan mashuhuri wametoka katika mafunzo yenu kama mfano tu ili tujiridhshe na mafunzo kabla hatujajiunga?

Ethics zetu hazituruhusu kutaja majina ya watu hadharani
 
Baada ya kugraduate mtu ataweza kujiajiri mazingira gani?
 
JIFUNZE SAYANSI YA KIAFRIKA

UNGO AFRIKA ni taasisi inayo jihusisha na masuala ya utamaduni,mila na desturi za kiafrika . Tunapenda kuwatangazia watu wote kuwa tunatoa kozi maalumu ya kujifunza kozi iitwayo " SAYANSI YA KIAFRIKA". Katika kozi hii utajifunza namna ya kutumia NGUVU YA SAYANSI YA KIAFRIKA katika kukabiliana na masuala mbalimbali yanayo zunguka maisha ya kila siku ya mwanadamu kama vile (mapenzi/mahusiano, ndoa), biashara, kazi, ulinzi na magonjwa.
Tunapatikana jijini Dar Es salaam, na tunao wataalamu walio bobea katika sayansi ya kiafrika kutoka katika makabila yote ya Tanzania bara na visiwani. Wataalamu wetu wana ujuzi na uzoefu wa SAYANSI YA ASILI kutoka katika mataifa yote ya kiafrika,Arabuni na India.
Tupo jijini Dar Es salaam.
Masomo kuanza, tarehe 01 OKTOBA 2013
Kujiandikisha, tuandikie kupitia barua yetu : ungoafrika@gmail.com

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 25 SEPTEMBA 2013.
WAZUNGU WANAITA UCHAWI, LAKINI SISI TUNAITA, " SAYANSI YA KIAFRIKA"

KWA PAMOJA TUUNGANE KATIKA KULINDA NA KUENDELEZA, MILA,DESTURI NA TAMADUNI ZA MWAFRIKA.
Kwa updates kuhusu taasisi yetu na shughuli zetu, endelea kutembelea:
http:// www. ungoafrika.blogspot.com

Hongereni
 
Umri kuanzia miaka mingapi na je naweza kumleta mdogo wangu aloshindikana, mtaani wanapenda kumwita teja akafuzu vizuri?
 
Hayo makitu huwa nayatamani sana,aisee nitawavisit kesho.Kwenda Dubai na hayo mavitu inatumia muda gani?
 
Hayo makitu huwa nayatamani sana,aisee nitawavisit kesho.Kwenda Dubai na hayo mavitu inatumia muda gani?

Si utani mkuu, hata mimi naihitaji sana hii kitu kwani itanisaidia katika kuizunguka dunia.
 
MAJIDAI ,vipi mkuu ulifanikiwa kusajili "DINI"? au ndo umeamua kutoka kivingine?
 
Last edited by a moderator:
Mzizimkavu unaitwa huku
Mkuu LIKUD Nıngelikuwepo huko Bongo ningelihudhuria huo Mkutano alioanzisha Mkuu.@MAJIDAI lakini nipo Ughaibuni sitoweza kuhudhuria. Ila ninamuomba Mkuu MAJIDAI aje kutupa Feedback wamefikia wapi na wameamuwa ni nini cha kufanya kuhusu hiyo “ SAYANSI YA KIAFRIKA”
 
Last edited by a moderator:
Aisee mimi niko interested sana na hiyo sayansi nimesoma sayansi za dunia sasa nataka nisomee na hiyo sayansi ili niweze kujua mechanism yake inafanyeje kazi niko serious nitawatafuta labda inaweza kunirahisishia shughuli zangu za kila siku za ujenzi wa taifa,nataka nipate training ya theory na practical pia na experiment za kutosha kabisa baada ya hapo nitaitungia kitabu wadau niwauzie ili na nyie muielewe vizuri ni sayansi ya namna gani kizuri mie ninayo elimu ya sayansi ya wazungu sas hii ya kiafrika naitamani sana
 
Mkuu
LIKUD Nıngelikuwepo huko Bongo ningelihudhuria
huo Mkutano alioanzisha
Mkuu.@MAJIDAI
lakini nipo Ughaibuni sitoweza kuhudhuria. Ila ninamuomba Mkuu
MAJIDAI
aje kutupa Feedback wamefikia wapi na
wameamuwa ni nini cha kufanya kuhusu hiyo
“ SAYANSI YA
KIAFRIKA”

Mzizi Mkavu ... mbona unaniangusha Bwana? Umekuwa mzito ... unataka utumiwe feedback? Ungewataka waruke kiafrika watue hapo ughaibuni ... wakujulishe ...uwapokee wapi.
 
Last edited by a moderator:
Mzizi Mkavu ... mbona unaniangusha Bwana? Umekuwa mzito ... unataka utumiwe feedback? Ungewataka waruke kiafrika watue hapo ughaibuni ... wakujulishe ...uwapokee wapi.
Mkuu The Prezident huku ni mbali hawawezi kuja na hizo ndege zao za ungo zitaanguka njiani kwa kuishiwa mafuta ya ndege.Ni mbali sana huku na kuna wachawi wa kizungu huku wataweza kuzizuia hizo ndege za ungo za kiafrika,zisiweze kuruka angani tena.
 
Back
Top Bottom