Jifunze kutengeneza mafuta ya kujaza ndevu

Jifunze kutengeneza mafuta ya kujaza ndevu

Wengine tuna ndevu kama msitu tunatamani hii shida ingenitoka kumbe wengine wanateseka kuzipata dah,


Spendi ndevu sijui kwa nn
 
Hakika zitakua za ukweli ..

Ngoja tuone...

Itapendeza sana... mwalimu...

Mimi kama mwanafunzi ningeomba darasa...

namna ya kutengeneza na hata ukinionesha matumizi yake itapendeza zaidi...


Cc: mahondaw
 
Ukitengeneza ya kufuta upara uniambie plies
Habari zenu wapendwa..

Naamini wote mko poa..

Yna2 Leo nimeamua kuwaletea somo la namna ya kutengeneza mafuta ya kujaza ndefu kwa wanaume (natural beard balm).

Mafuta haya siyo kwamba yatajaza ndevu tu ila yanatafanya ndevu na mn'garo,kuondoa mfungamano,na kuondoa m'ba.

MAHITAJI

beeswax(sega la nyuki) 1tbsp
-kazi yake ni kufanya mafuta yetu yagande na vilevile inasaidia kufanya nywele in'gae.

Shearbutter 1tbsp
-inauwezo wa kujaza nywele na kuipa ulaini na mn'gao.

Coconut oil 2tbsp
-kazi yake kujaza nywele na kuondoa ukavu kwenye ngozi na kuifanya nywele in'gae (nakushauri tumia mafuta ya Nazi yasiyopikwa)

Sweetalmond oil 2tbsp
-kazi yake kuzuia nywele isikatike,kuipa nywele mn'gao,na kuijaza.

Lavender essential oil 10drops
-kazi yake kuondoa matatizo ya ngozi Kama m'ba..fangasi kwenye ngozi..kuzuia nywele kukatika na kujaza nywele.

Rosemary essential oil 5drops
-kazi yake ni kuifanya nywele kua nzito..ndefu.. kupunguza wingi wa mafuta..kuipa nywele ulaini na mn'gao.

JINSI YA KUTENGENEZA

weka sufuria jikoni ..weka maji yachemke ..chukua sufuria nyingine au bakuli la udongo weka beeswax na shearbutter..chukua bakuli lako/sufuria weka juu ya sufuria lenye maji huku ukikoroga taratibu hadi iyeyuke.

Kwanini tunayeyusha butter na beeswax juu ya sufuria nyingine badala ya kuiweka sufuria moja kwa moja kwenye Moto..? Tunafanya hivi sababu ya kuepuka kuua vitamini zilizomo kwenye butter na beeswax.

Butter na beeswax vikiwa vimeyeyuka weka mafuta yaliyosalia isipokua essential oils..koroga Kisha ipua.

Acha yapoe kidogo weka essential oils..koroga vizuri Kisha weka kwenye vikopo tayari kwa kuuza/kutumia.

Nb: ukikosa sweetalmond oil tumia castor oil sio yale ya rangi nyeusi.

Ahsanteni.

Moderators naomba msiuamishe huu Uzi tafadhali.

Mchana mwema.

View attachment 1250851View attachment 1250853View attachment 1250854
 
je unajua kutengeneza sabuni za kujichua. uweke na mafuta ya kupika for maximum slope ahaha full kuteleza
 
Mi nitauza nyembe, shaving cream na shavers....
 
Back
Top Bottom