Jifunze kusamehe hata kama huoni kosa

Jifunze kusamehe hata kama huoni kosa

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,758
Reaction score
9,592
Natumai mko fiti waungwana na mnaendelea na shughuli, kazi, masomo na pilika pilika za hapa na pale
ilimradi tu kujiingizia kipato chenu cha kila siku. Na wengine wanaendelea kuendekeza mambo yasiyofaa kwao.
wote hawa napenda kuwapa hai iliyo na furaha ndani yangu.

Leo nimekuja na kitu hiki ambacho wengi wetu tunaona kama ni kizuri tu na wala hatuoni madhara naccho.
Nacho ni "kutokusamehe". Wengi wetu tumejawa na mioyo iliyokuwa na uchungu ndani yetu hata tunashindwa kusamehe hata kama umefanyiwa jambo dogo la kukuuzi na ndugu au jirani yako. Kwanini tunashindwa kusamehe na kuachilia na kusahau kwa wale waliotukosea kwa mambo makubwa ama madogo. Utaona mtu analipiza kisasi kwa mwenzie ambaye hakukusudia kufanya kosa lile ilikuwa ni bahati mbaya tu imetokea lakini yeye atalivalia njuga mpaka linaonekana kuwa kubwa na kuweka uchungu moyoni dhidi yake. Wengine wetu hata kama hakuna kosa lolote llilitendwa hapo basi yeye atachukulia kuwa ametendewa na kuanza kuporomosha matusi yasiyokuwa na idadi.

Hivi kwanini sisi viumbe wanadamu tumekuwa hivi, kwanini ukiuziwa au ukitendwa unachukua sheria mkononi na kuanza kumhukumu mwenzio na kufyolea ovyo kisa tu amekukosea. Kwanini tunashindwa kuwa na moyo wa kusamehe, na kuachilia na kupenda huyo aliyekukosea0, hivi hujui kuwa hata Baba yetu aliye mbinguni alitusamehe makosa yetu kwanini sisi tushindwe kusamehe. Ukiwa na moyo wa msamaha utakuwa mtu mwema na mwenye upendo kwa adui yako. Hebu jamani tujifunze kusamehe hata kama hatuoni kosa au hata kama tumetendewa vibaya na wapenzi, marafiki, ndugu na jamaa zetu. Wewe msamehe na achilia na kusahau kabisa. Utaziona baraka za Mungu zikiwa juu yako.

Rafiki zangu jifunzeni kusamehe na kusahau hata kama mtendewa vibaya na jamaa zenu

be blessed

 
Mwanamke yeyote akigundua mmewe au mshikaji wake anamsamehe samehe tu hovyo, hata kama yeye mwanamke ndo mwenye makosa, anamwona ---- na ataanza kumtangaza kwenye masaloon.
 
umenielewa kivipi ndugu yangu; je ewewe ukikwaza, kuuziwa au kufanyiwa kitu mbaya utakuwa na moyo wa MSAMAHA kwa huyo aliyekuuzi wewe?
Kusamehe nimuhimu sana katika maisha kwaupande wangu nasamehe lakini sio same time, nachukua mda lakini nasamehe ila yule alonikera sitaki kumuona tena au najaribu kuanae mbali,hata kama alikua rafiki yangu wa karibu sana baada ya salam nishamaliza...
 
hapo umenielewa kwa kiasi unapomsamehe mtu usiwe na uchungu naye kabisa moyoini mwako, bali umpende na kumjali na ikiwezekana waweza kumkaribisha hata home kwako hii yote itampa fundisho yeye aliyekukosea kuwa kumbe alifanya makosa na kuona kuwa yeye ni mkosaji na wewe itakusaidia usipatwe na maradhi
Kusamehe nimuhimu sana katika maisha kwaupande wangu nasamehe lakini sio same time, nachukua mda lakini nasamehe ila yule alonikera sitaki kumuona tena au najaribu kuanae mbali,hata kama alikua rafiki yangu wa karibu sana baada ya salam nishamaliza...
 
Kusamehe ni kuzuri sana lkn wengine wakigundua kuwa kila wafanyalo husamehewa basi watakukwaza kila kukicha.Lbda uwe huna roho maana utapata heart attack kwa kukwazwa kutwa. Sometime you need to show seriousness kwa kuonyesha umekasirika !
 
kyumbo mambo! umzima? lete habari ujakwaza wewe au kukosewa
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom