Jifunze kumuacha aende
- Kamwe usihisi kama ulimwengu unakaribia mwisho pale umpendaye anapokuacha...MWACHE AENDE
- Kujaribu kumlazimisha mtu akupende ni sawa na kumlazimisha nguruwe kutambua usafi, usimlazimishe kama hakupendi...MWACHE AENDE
- Wewe ni wathamani mno kulilia penzi akupendaye kwa dhati atakuheshimu hatokudharau ikiwa anakudharau... MWACHE AENDE
- Usikasirike pale mtu wako anapompenda mwingine tofauti nawewe siku zote nivigumu kumshawishi nyani kuwa asali ni tamu kuliko ndizi... MWACHE AENDE
- Mwanamke/mwanaume anayekuchukulia kirahisi sikuzote atachukulia faida kuburuta anavyotaka akijua haufurukuti kwake. Yeye si MUNGU akufanye atakalo... MWACHE AENDE
- Kuna watu hawatakupenda hata kama utajitoakiasigani kwako, ni sawa tu, haimaanishi unakitu kibaya bali hawako kwa ajili yako... usilazimishe chungwa kuwa fenesi... MWACHE AENDE
MUHIMU
. Huwezi badilisha maoni mabaya ya watu juu yako ila unaweza
kuzuia maoni yao yasikubadikatikae wewe kama wewe.
. Acha kichwa chako kiongoze moyo wako kukuondoa katika mahusiano sumu. Lengo la mahusiano sio kuleta mfadhaiko bali nikuleta furaha juu yako.
MWACHE AENDE HATAKAMA UNAAMINI AMEZALIWA KWA AJILI YAKO.