Jifunze kumuacha aende

Mkuu,nafikiri hujawahi kupenda kisawa sawa,isikie kwa wenzio tu,unapenda mpaka unachizika,kumuacha huwezi ila cha moto unakiona.
Hapo ndyo unajiona umepatwa!!!!hahahaha..rahisi sna kusema mwache aende...Ahahha..kimbembe wanaokuja hawajamfikia huyo uliyemuacha aende!!!Mkuu mwache aende tuu mi tayari mwenzio
 
Hakuna kitu kigumu kama kun'gan'gania penzi... Unakuwa mtumwa, unafanya vitu kumridhisha mtu asiekuthamini. Muache tuu aende kwakweli
 
Ni sahihi kumuacha aende, japo inauma ila baada ya muda unasahau. Watu wanafiwa na mke/mume analia mpk anazimia, ila baada ya muda anasahau na maisha yanaenda, hata kwa hili utaumia then baada ya muda utasahau. Peace of mind is what is needed.
 
Nashindwa kumuacha bhana,maana mavituz anayonipa napagawa,akiwa mbali napata kisebusebu na kiroho kinapasuka,inabidi nikubali yaishe at least niambulie ngoma ya ukae,kuliko ukame ukinishika nipate wazimu sababu ukame wangu anaeweza kuutoa ni yeye tu hapa duniani bhana,mbona huelewi?enyi wanawake nawapa sifa jamani,sisi wanaume mkitufikisha penye naninhii basi hatuna ujanja tena.
Hako kaujinga, siyo umekaanzisha wewe, bali ni maumbile jinc M/Mungu alivyokusudisha mapenzi yawe.
Lakini hakuna kitu kibaya kama kutumikia penzi mfu. Penzi linatakiwa liwe50/50 toka pande zote, pasiwepo mtumwa na mtwana yaani mpendane.
Halafu unaonesha umri wako bado ni "kinda". Haujawatafiti wanawake ukawaelewa na ukapata uzoefu wa kutosha, usingeendelea kubaki na mawazo ya kudhalilishwa kihisia.
"mapishi matamu" siyo kigezo pekee cha kung'ang'ania. Sifa inajazwa pia na upendo na tabia njema.
Usiwe kama mbwa, akiishanasa harufu ya chatu. Kwanza hufahamu kuwa harufu hiyo ni ya adui, lakini hukosa namna ya kukwepa, hujongelea kwenda kumezwa mzimamzima huku akilia. Sasa iwe kwako binadamu mwenye maamuzi!
 
Shida ni jinsi ya kumuacha nyie mnadhani ni rahisi rahisi tu kumwacha kazi ipo hapo si mchezo yataka uwe umejiandaa hasa kwenye hiyo vita vinginevyo ukikosea tu utageuka kuwa mtumwa mara 1000 zaidi kwa huyo umpendae
 
Hako kaujinga, siyo umekaanzisha wewe, bali ni maumbile jinc M/Mungu alivyokusudisha mapenzi yawe.
Lakini hakuna kitu kibaya kama kutumikia penzi mfu. Penzi linatakiwa liwe50/50 toka pande zote, pasiwepo mtumwa na mtwana yaani mpendane.
Halafu unaonesha umri wako bado ni "kinda". Haujawatafiti wanawake ukawaelewa na ukapata uzoefu wa kutosha, usingeendelea kubaki na mawazo ya kudhalilishwa kihisia.
"mapishi matamu" siyo kigezo pekee cha kung'ang'ania. Sifa inajazwa pia na upendo na tabia njema.
Usiwe kama mbwa, akiishanasa harufu ya chatu. Kwanza hufahamu kuwa harufu hiyo ni ya adui, lakini hukosa namna ya kukwepa, hujongelea kwenda kumezwa mzimamzima huku akilia. Sasa iwe kwako binadamu mwenye maamuzi!
Umesema kweli lakini sina jinsi bhana.
 
Am in tears.....usiombe yakukute utatamani dunia ipasuke uingie mapenzi yanauma jaman haswa ukiachwa na mtu ulie mpenda kwa moyo wote inauma sanaa....haswa akuache mda ambao unamhitaji Sana apo ndo kimbembe lkn inabdi ukubali matokeo tu Let t go...
 
Nataka niwaambie tu ukweli ndugu zangu,, hakuna hata mtu mmoja anaependa akatwe kiungo chake either mguu au mkono eti kwa sababu ya cancer,, ila watu wanatoa pesa ili wakatwe viungo vyao wenyewe kwasababu uwepo wa cancer katika mwili una madhara makubwa ukilinganisha na kutokuwepo kwa mguu au mkono ndo maana watu wanakubali kukatwa viungo vyao ili waendelee kuishi,,, kuwa na mpenzi asie kuheshimu wala kukuthamini ni sawa na kuwa na cancer ambayo inakutafuna taratibu na hakuna tiba nyingine zaidi ya kuitoa kwa kukata kiungo chako,, japo inauma lakini ndo tiba yake,,, mwache aendeeeeeeeee huyo ni cancer kwenye maisha yako
 
Back
Top Bottom