Jifunze kuhusu ndoa

Emanuel Musa

New Member
Aug 2, 2017
1
1
*NDOA:*

NDOA ni shule pekee ambayo unapata cheti kabla ya kuanza masomo. Ni shule ambayo kamwe hauwezi kuhitimu.
-----------------------------------
Ni shule ambayo unatakiwa kuhudhuria siku zote za uhai wako. Ni shule ambayo hakuna likizo ya kuumwa au sikukuu.

Ni shule ambayo iligunduliwa na Mungu katika misingi ifuatayo;

1. Msingi wa upendo.

2. Kuta za shule zimejengwa kwa "uaminifu"

3. Madirisha yametengenezwa kwa "uvumilivu"

4. Samani zimetengenezwa kwa "msamaha"

5. Na ikaizekwa kwa "Imani"

Ukumbuke kuwa wewe ni mwanafunzi tu na sio mkuu wa shule ya NDOA. Mungu ndio Mkuu wa Shule.

Hata wakati wa mapito, majaribu, kimbunga na misukosuko ya hapa na pale usikimbie nje ya shule.

Kamwe usiende kulala kabla hujamaliza homework yako. Kamwe usisahau kusoma somo la mawasiliano. Wasiliana na mwanafunzi mwenzio pamoja na Mwalimu mkuu.

Kama utaona kuna kitu kwa mwanafunzi mwenzako ambacho kimsingi haukipendi, basi ukumbuke mwenzako nae ni mwanafunzi na sio mhitimu mwalimu Mkuu bado hajamalizana nae. Hivyo ichukulie ni changamoto na muifanyie kazi kwa pamoja.

Msisahau kusoma kitabu kitakatifu kilicho kwenye mtaala wa shule ya Ndoa (Biblia). Najua kuna muda unaweza ukajisikia kutokuhudhuria darasani lakini unatakiwa uhudhurie tu.

Utakapojaribiwa kuacha shule jipe ujasiri wa kuendelea na shule. Najua mitihani mingine ya muhula au nusu muhula inaweza kuwa migumu isiyo na majibu kwako.

Lakini kumbuka Mwalimu Mkuu anayo majibu tayari na anafahamu unaweza ukakabiliana nayo na anaona hiyo ndio shule nzuri kwako kuzidi nyingine.

Ni moja ya shule nzuri kabisa katika ulimwengu huu. Furaha, amani, na upendo husindikiza masomo ya kila siku.

Masomo mbalimbali hutolewa katika shule hii, ila somo kuu kuliko yote ni UPENDO.

Baada ya miaka yote ya kusoma kwa nadharia, ukijiunga na shule hii utasoma kwa vitendo.

Kupendwa ni kitu kizuri, lakini kupenda ni upendeleo wa vyote. Ndoa ni sehemu ya furaha. Inatakiwa kufurahia tofauti zenu na sio tofauti zenu ziwe chanzo cha kutoelewana.

Nawatakia kila la kheri wote mliopo kwenye hii shule takatifu. Na sisi ambao bado tumuombe mwenyezi Mungu ambae ni Mkuu wa Shule akatuchagulie wanafunzi wenzetu walio bora ambao tutaweza kujiunga nao katika hii shule nzuri hapa Duniani.
 
Back
Top Bottom