Jifunze kuhusu "choice theory"

boniuso

JF-Expert Member
Mar 13, 2013
670
834
Hii ni nadharia ambayo inaelezea kuhusu uwezo wa machaguo ambayo kila mmoja anaweza kuchagua.

Hii inaeleza kuhusu nguvu ambayo kila mmoja anayo .Nguvu ya uamuzi ipo kwenye fikra za kila mtu nyakati zote za uhai

Hivyo hakuna mtu anaweza kukuondolea kile unachokiamini mpaka uamue kufanya hivyo.

Kila mmoja anajijua sana nafsi yake na uwezo wake lakini utashangaa mtu akiambiwa huwezi kufanya hiki au kile kisha huamini maneno hayo.

Wapo watu ni wataalamu eneo fulani au wanavyo vipaji eneo fulani lakini wazoefu au wakongwe wa eneo hilo wakisema huwezi kufanikiwa eneo hili anaamini maneno hayo

Unatakiwa ujue kuwa kila mmoja anao uhuru wa kuchagua ambao uhuru huo ndio unafanya tunakuwa tofauti kwenye maamuzi ya jambo moja

Badala ya kumlaumu mtu kwa kile amefanya unatakiwa ujiulize kwanini amefanya uamuzi huo

Hii ni kwa sababu unapomlaumu mtu kwa uamuzi amefanya bila kujua sababu za uamuzi huo utazidi kupata hasira juu ya mtu huyo

Thinking is difficult that's why most people judge- Curl Jung

Alisema mwanasaikolojia Curl Jung kuwa kufikiri ni kazi ngumu sana ndio sababu watu wengi huwa wanahukumu kila mtu kwa kila kitu

Usipojua sababu ya mtu kufanya uamuzi fulani usimlazimishe au kulaumu kwaa uamuzi huo

Kumbuka kila mmoja hufikiria tofauti na mwengine hata kama tunatazama kitu kimoja tafsiri zetu huwa tofauti

Maana yake kuna matarajio utaweka kwa watu kuwa wakifanya hivi au vile ndio itakuwa sahihi lakini ukweli ni kuwa hakuna binadamu anaeweza kutimiza matarajio yako yote kwa 100%

Kubali kuwa tunaishi kwenye ulimwengu wenye mapungufu mengi sana hivyo watu kukuvunja moyo ni kawaida kwa sababu unaweka matarajio makubwa sana kwao kuliko uhalisia

"Stress is the gap between expectations and the realities, more the gap more stressed, expect nothing accept everything"

Tafsiri isiyokuwa rasmi ni kuwa huuzuni ni tofauti ya matarajio yako na uhalisia wake,hivyo matarajio makubwa huleta huzuni kubwa na ili usiwe na huzuni kubali chochote kinachokuja kwako na uondoe matarajio

Binadamu huteseka sana kwenye fikra zake kuliko kwenye uhalisia

Kinachoweza kukutesa sio maisha bali tafsiri yako juu ya maisha

Endapo hatutakuwa na matarajio kwa watu hautakuwa na huzuni kwa kile watafanya au hawatafanya

Unapojifunza kukubali chochote watu watafanya au kuzungumza unakuwa huru kwako mwenyewe

Hakuna kinachoweza kukutesa zaidi ya fikra zako mwenyewe

Kwa kutambua kuwa huwezi kubadilisha fikra za watu bali unaweza kubadilisha fikra zako mwenyewe unakuwa huru sana

Unaweza kujituma sana kuliko watu wote lakini huwezi kupanga boss wako akupe pongezi au kusifia kazi zako hivyo kukosa furaha kwa sababu hupewi pongezi hiyo ni adhabu unajipa mwenyewe

Hasira ni kujipa adhabu kwa kosa la mwengine

Huna sababu ya kukasirishwa na uamuzi wa mtu yeyote kwa sababu haumiliki fikra zao au maamuzi yao

Kumbuka unayo nguvu ya kudhibiti akili yako tu sio akili za watu wengine

Fikra zako,hisia zako,tabia yako,imani yako, maoni yako vipo ndani ya uwezo wako

Tabia za watu wengine,fikra za watu wengine, maamuzi ya watu wengine,hisia za watu wengine, maoni ya watu wengine,imani za watu wengine vipo nje ya uwezo wako

Kupata hasira kwa sababu ya tabia za watu wengine ni adhabu kubwa watu wengi wanajipa

Acha watu kuwa vile walivyo kisha utawaelewa

Watu hatufanani fikra hivyo unaweza kuona mtu fulani anafaa sana kumbe mwengine hajaona hivyo vigezo unavyoona wewe

Mara ngapi unaweza kumlaumu rafiki yako kwa mke au mume amekubali kufunga nae ndoa?
Unamlaumu kwa sababu amechagua kitu ambacho ni tofauti na matarajio yako

Wewe unaona hafai yeye ameona anafaa sio kwa sababu mtu ni tofauti bali fikra zenu ni tofauti

Unaweza kuona ubaya kwenye uzuri au kuona uzuri kwenye ubaya

Unaweza kuona mvua ikinyesha ukasema bora mvua inanyesha kuleta maji na kupunguza vumbi mwenzio akalalamika mvua kunyesha inaleta shida kwa sababu nyumba yake inavuja tukio moja tafsiri tofauti

Kinachotokea ni 10% huku 90% ya matokeo hutegemea tafsiri yako mwenyewe.
na furaha yako au huzuni yako ni tafsiri juu ya tukio husika

Kila binadamu anazo sehemu mbili katika tabia yake.
Sehemu ya mazuri yake na sehemu ya mabaya yake

Ukitazama mazuri yake utampenda na ukitazama mabaya yake utamchukia hivyo mtu kukupenda au kukuchukia itategemea ametazama upande gani wa tabia zako

Huwezi kuwa mzuri 100% au mbaya 100%

Kwa chochote utafanya yupo mtu atakuchukia

Anakuchukia sio kwa sababu wewe ni mbaya Lah kwa sababu anajichukia yeye kisha anakuonyesha chuki hiyo

Kila mtu anachokisema kwako ni tafsiri ya hisia zake kwako

Yaani watu wengine wanakuwa kioo kwako kile unachokiona kwao kipo kwenye fikra zako ndio sababu mwengine anaweza kusema tofauti kwa jambo moja mkilitazama

Kwa sababu tupo na tafsiri tofauti tegemea maoni kuwa tofauti kwa tukio moja

Uzuri au ubaya upo kwenye tafsiri unayoweka wewe sio kwenye tukio husika

Ukitazama ubaya wa watu kila wakati utawachukia watu wote na ukitazama uzuri wa watu nyakati zote utawapenda

Mzazi anapozaa mtoto homoni za oxytocin huzalishwa kwa wingi na kumfanya mzazi ampende mtoto wake hata kama mtoto amefanana na nyani

Mapenzi huambatana na mguso wa kihisia ambazo hisia hizo huletwa na homoni.

Hivyo mtu akipenda sana kitu au kukichukia sana kitu ni tafsiri ya hisia zake mwenyewe sio wewe kuwa special au kuwa mbaya

Mtu kukupenda ni maamuzi yake na kukuchukia ni maamuzi yake pia
Hivyo acha watu huru anaekupenda akupende vile ulivyo na akikuchukia akuchukie kwa sababu ya uhalisia wako

Kila mtu anataka mwenza sahihi lakini hakuna anaetaka kuwa sahihi

Kupata kitabu cha
1.FIKRA ZAKO FURAHA YAKO (softcopy)
2TIBA YA MSONGO WA MAWAZO (hardcopy & softcopy)
3.BADILI FIKRA ZAKO BADILI MAISHA YAKO (hardcopy & Softcopy)
4.MALEZI YA UBONGO KISAYANSI( hardcopy & softcopy)
5.TABIA ZA WATU WALIOFANIKIWA (Hardcopy & softcopy)

6 MISINGI 10 YA FURAHA SIKU ZOTE (hardcopy &softcopy)

+255766862579
+255622414991

Imeandikwa na Psychologist
Said Kasege
Temeke,Dar es salaam
 
Back
Top Bottom