Jifunze kuheshimu kila mtu

Jifunze kuheshimu kila mtu

kwa hiyo picha, kweli heshima haipo hapo....
 
Wanajamvi tujifunze kumuheshimu kila mtu hata kama mtu flani ana/una mali nyingi kiasi gani ipo siku na wewe utakosa au uchumi utayumba.

Wadau tukumbuke hali ya maisha huweza kubadilika wakati wowote, leo waweza kuwa tajiri lakini kesho ukawa masikini.

Endapo unaamini hayo yanaweza tokea wakati wowote, basi huna budi kumuheshimu yule asiye nacho, ulicho nacho wewe sababu wakati wowote unaweza ukawa katika hali aliyonayo mwenzako.
Nawatakia tafakari njema.


attachment.php

Ili kumheshimu zaidi, hiyo gari angeikunja na kuitia mfukoni na kupita kwa miguu au angeweka gea ya kuruka ! au pengine hakukuwa na barabara nje ya soko
 
Binaadamu wengi wakipata mali basi hujawa na kiburi sana...nilishawahi kukumbana na matuki ya kudharaulika na mengine nilishayasimulia humu....lakini kubwa ni la yule mzee pale posta wakati huo nafanya kazi ya umachinga...alivyokuwa anatunyanyasa sana vijana tuliokuwa tunapanga bidhaa karibu na ofisi yake...yaani ilikuwa mara anatuitia polisi wanatuweka ndani kana kwamba sie ni vibaka..mara anatuitia wagambo wa jiji wanatupiga marungu.....yaani ilikuwa ni mateso kwa kwenda mbele.....lakini siku moja tukageuka mashujaa kwake baada ya yeye kushikwa na ugonjwa sijui ni kisukari au PRESHA....ninachokumbuka ni kwamba mimi ndiye nilikimbia kwenda kumnunulia dawa baada ya yeye kushindwa hata kushuka kwenye CRUISER yake kwa maumivu....huku akijitahidi kuunyoosha mkono angalau akifikie kitufe cha kushusha madirisha ili aombe msaada.....tukio ambalo lilimgharimu karibuni dakika ishirini hadi kulifanikisha....baada ya vijana kumhudumia na kurudi katika hali ya kawaida akatoa hela kiasi kama laki mbili ili tugawane maana tulikuwa kama watu wawili tu.....lakini sisi tukakataa na kumwambia kwa kauli moja UTU KWANZA....sisi ni binadamu na kumekusaidia kama binaadamu mwenzetu......TANGU HAPO YULE MZEE AKAWA RAFIKI YETU SANA..mpaka watu wakawa wanashangaa pale kijiweni...tuliapa kutomwambia mtu yoyote tukio lile..
 
Wanajamvi tujifunze kumuheshimu kila mtu hata kama mtu flani ana/una mali nyingi kiasi gani ipo siku na wewe utakosa au uchumi utayumba.

Wadau tukumbuke hali ya maisha huweza kubadilika wakati wowote, leo waweza kuwa tajiri lakini kesho ukawa masikini.

Endapo unaamini hayo yanaweza tokea wakati wowote, basi huna budi kumuheshimu yule asiye nacho, ulicho nacho wewe sababu wakati wowote unaweza ukawa katika hali aliyonayo mwenzako.
Nawatakia tafakari njema.


attachment.php
Ningekuwa mimi hapo ningemtegeshea misumari chini ya tyre akazibe pancha mbele kwa mbele.........
 
angalia wewe usije wakuta wenye magari wote wako mbinguni wewe uko jehanam
 
Sasa hapo si barabarani? Nani ambaye hamuheshimu mwenzio? Watu wengine wanatumia kigezo cha umaskini ku play victim waonekanae wananyanyaswa.Hapo mwenye gari ndo ananyanyasika. Analipia road licence ya gari lake lakini anakuta kaweka nynya barabarani na huyo mtu halipi hata senti tano ya kodi

umasikini isiwe sababu ya kuvunja sheria na kanuni tulizojiwekea. Saa nyingine umasikini unaanzia kwny akili halafu unajitokeza bayana kwny maisha halisi ya mtu kama huyo alie maskini wa kuelewa alipopanga bidhaa zake si sehem sahihi
 
Back
Top Bottom