Jifunze kuchakachua utafiti kama REDET | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jifunze kuchakachua utafiti kama REDET

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ulukolokwitanga, Oct 9, 2010.

 1. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2010
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Malumbano yanayoendelea baada ya utafiti wa reDIRT yamebase katika sample wengine wakisema ilikuwa bias na wengine ilikuwa haitoshi. Sample ya 2600 inatosha sana kwa watafiti wazoefu kama Dk Bana, lakini kilichofanyika ni tofauti kabisa....
  alichofanya Dr Bana na wenzake (ambacho watafiti wengi wa TZ hasa wale academicians huwa wanafanya) ni kuwaita Makamba na Kinana na kuwauliza mnataka tumpatie % ngapi JK, Slaa (PhD) na Lipumba. Baada ya kupata maoni yao akacheza na data wakati wa coding. Hapo ndipo manipulation yote ilipofanyika in favour of ccm. Ukiangalia ripoti waliyopublish imeificha kabisa questionnaire waliyotumia, hawajaweka appendix so hatuna uhakika hicho wanachosema ktk analysis waliuliza ni kweli au la!
  Kilichofanyika waliwatuma hao watafiti wasaidizi 52 ktk hiyo mikoa na wilaya, kwa vile watafiti wasaidizi hawawasiliani na kila mtu anarudi na takwimu zake kumkabidhi mtu wa coding and analysis, yani Dk Bana, ni vigumu hata wao kujua matokeo yatafananaje. Swali la JK anaungwa mkono vipi akalimanipulate kufuata alivyoshauriwa na Kinana na Makamba ili akifanya analysisi apate output inayoendana na maoni yao huku maswali mengine yakiachwa kama yalivyokusanywa huko wilayani, ndo maana lile la vyombo vya habari vinavyoripoti uchaguzi lina uhalisia wa kutosha ukicompare na Campain trail ilivyo. Akaenda kwenye analysis akatumia descriptive statistics ambazo zikadescribe kama Kinana na Makamba walivyopendekeza kwa kuwa data zilikuwa manipulated kufuata matakwa yao. Mwisho akafanya discussiom kwa kuongeza maoni yake na kuua soo kidogo kwa kusema kuwa CHADEMA inakubalika zaidi kuliko mwezi wa tatu na umaarufu wa Slaa (PhD) umeongezeka ili watu waone kama utafiti ni halisi. Alipomaliza hapo akawatolea waTz hawa wajinga na huku makubaliano ni kuwa kesho yake Kinana unaviita vyombo vya habari kufurahia utafiti, ingawa akaboreka kwa kuwa yeye na makamba walitaka JK apewe %80.
  Hivi ndivyo watafiti wengi wa vyuoni huwa wanafanya hapa Tz, ndo maana taasisi za kimataifa huwa zinafanya kazi na independent researchers badala ya hawa wachakachuaji wa vyuoni. Ni aibu kwa nchi na wao wenyewe ndio maana tafiti nyingi zinaishia ktk makabati kwa kuwa wanajua walichokifanya hakina uhalisia.
   
Loading...