Jifunze kitu hapa - TRUE STORY

Jifunze kitu hapa - TRUE STORY

Aiseeeeeee inaumiza kweli, miaka ya nyuma sana nikiwa darasa la tatu dada yangu mkubwa akiwa anasoma tambaza kidato cha tano alikua na rafiki zake miongoni wa kiume mmoja ndio alikua mashine balaaa alikua anaitwa Emanuel... Kwao walikua vizuri sana kifedha ila ghafla maisha yakabadilika na jamaa akaanza kushuka performance hivyo hivyo ila akajisogeza hadi chuo akaingia mzumbe ila second year aka disco na habari yake ikaishia hapo. Akahangaika we hali haikukaa sawa, baba yake akafariki na sababu alikua na mama wa kambo na mama yake alishafariki basi akatengwa na home akatimuliwa mweupe. Wenzake wote wana life safiiiiiii ye jamaa yupo mtaani mara amenye viazi, afanyishwe usafi n.k mwezi wa nane bahati mbaya akiwa anavuka barabara pale korogwe kimara sijui alikua kajawa na mawazo sana akagongwa na mwendokasi akafariki hapo hapo
This life ain't fair at all
 
Amina mkuu
Fanyia kazi sana ushauri huo apo wa wadau ufanye toba ya kweli ya kwako,wazazi wako mpk wa kizazi cha nne

Simama kwelikweli kwenye maombi kwa kufunga
Kwa kufanya hvyo naamin vifungo vyote vitaondoka na utaona mnavyofunguliwa
 
I can feel the suffering inside your friend's.Binafsi huwa nikikutana na marafiki zangu huwa naumia sanaa,maisha yao yamechange kabisa,wote huwa wanaishia kunihurumia na kunitia moyo.
Moyo uliojeruhika dawa yake ni neno la Mungu, aiseh inauma sana kuwaona uliosoma nao wanakuuliza upo wap huwa sizipendi aiseh nilimaliza form 6 mwk 2011, nikipata fff maisha yakawa magumu aiseh nikarudi kuanza Cheti na diploma ya account 2014 nikaanza degree nikaumwa wkt wa paper chuo wakanipostponed yr sio kwa hiari yangu ila nimemaliza this yr, kwahiyo usikate tamaa wala usivunjike moyo ndio maana kuna mmoja humu kacomment mambo mengine ukijiuliza huwezi pata jibu ww mwachie Mungu na uyaache tu yaexist basi.
 
Aiseeeeeee inaumiza kweli, miaka ya nyuma sana nikiwa darasa la tatu dada yangu mkubwa akiwa anasoma tambaza kidato cha tano alikua na rafiki zake miongoni wa kiume mmoja ndio alikua mashine balaaa alikua anaitwa Emanuel... Kwao walikua vizuri sana kifedha ila ghafla maisha yakabadilika na jamaa akaanza kushuka performance hivyo hivyo ila akajisogeza hadi chuo akaingia mzumbe ila second year aka disco na habari yake ikaishia hapo. Akahangaika we hali haikukaa sawa, baba yake akafariki na sababu alikua na mama wa kambo na mama yake alishafariki basi akatengwa na home akatimuliwa mweupe. Wenzake wote wana life safiiiiiii ye jamaa yupo mtaani mara amenye viazi, afanyishwe usafi n.k mwezi wa nane bahati mbaya akiwa anavuka barabara pale korogwe kimara sijui alikua kajawa na mawazo sana akagongwa na mwendokasi akafariki hapo hapo
This life ain't fair at all
Daaah huzuni sanaaaa!! Mungu aturehemu sana
 
Mkuu umenifanya nilie sana mbaya zaidi nimesoma hii thread nikiwa katikati ya wimbi zito la mawazo ninapita changamoto lakini zangu si kitu kwako natamani hata ningekusaidia lakini sijajaliwa uwezo wa kutosha kukusaidia cha msingi nitakukumbuka kwenye maombi Na kama nitapata nafasi ya kukusaidia kwa lolote nitafanya hivo Ila usikate tamaa tu kwani ukikata tamaa utaharibu zaidi maisha yako
Do so
 
Pole sana mkuu naelewa unapita kipindi kigumu mnoo,muombe sana mungu sana sana maisha yako yatabadrika tu.hakuna linaloshindikana kwake
 
Pole sana Mkuu,Mungu ni mwaminifu mtumainiye Naye hatakuacha kamwe...Ipo siku utakaa na kukumbuka ulipotoka wala hutaamini.
Hii naiweka kwenye nyuzi bora kabisa inayofundisha watu na inayogusa maisha yetu ya kila siku.
 
Aiseee! Hapa huwa najikuta najicheka kabisaaaa...sababu kuu ya kujicheka ni kujiona nna shida au Matatizo makubwa sana...kumbe kuna watu wanashida au Matatizo makubwa yangu cha MDOLI BIN MTOTO,

Naomba niishie hapa nisije kulia bure...
 
Bwana fox kutokana na maelezo yako mazuri inaonyesha vikwamo vyako na vya familia vipo kiroho. Kuna vifungo katika ulimwengu wa Kiroho ambavyo vinatakiwa kufanyiwa kazi. Usije shangaa baadae ukaja gundua kuwa wanao husika na vita hivi wakawa ni ndugu wa karibu kabisa katika familia, sijajua kuwa wewe ni mkristo au la hilo halijalishi. Tafuta uongozi wa kiroho kutoka kwa watumishi wa Mungu ili wakupe hekima na maarifa namna ya kupambana na vita hivi. Jua kuwa vita hii ni ngumu sana na unamuhitaji Mungu sana kuliko wakati wowote wa maisha yako.

Katika maombi utagundua mambo mengi sana na taratibu utaanza kukonect dots kutoka katika maisha yako ya udogoni, nyumbani kuhusu maisha ya wazazi na mambo ambayo wazazi walikuwa wakiongea na kukwambia. PIA usije shangaa kuwa wazazi wako wanahusika kwa anguko la familia kwa namna moja ama nyingine, kama ulivyosema kuwa baba alikuwa mfanya biasha mkubwa na maisha yalikuwa mazuri, inawezekana kuwa palikuwa na mikataba ya kishetani kwa ajili ya mafanikio ya kibiashara na makafara yalikuwa yakitolewa. sasa inawezekana baba alivunja mashariti ambayo ikawa ni sababu ya anguko la familia.

Unaweza uliza kuwa kwanini ikaathiri mpaka elimu ya watoto !!! YES yapo mashariti ambayo yalikuwa pia juu yenu, wakati mkiwa wadogo wazazi waliweza ku control maisha yenu ili msiweze vunja hayo masharti sasa baada ya kukua hasa wewe ambae ulitoka mbali na familia kuna vitu ulifanya ambavyo ni kinyume na masharti ya zindiko la baba ikachangia anguko zima la familia.

Kuna mambo mengi sana, haya nilioandika ni MTAZAMO wa kiroho kutokana na mtiririko wa kisa chako. Kama nilivyo sema inahitaji kujitoa kwa kiwango cha juu sana ili kuweza kufungua hii code iliyofungia maisha yenu. Inahitajika muongozo na msaada wa ROHO Mtakatifu katika kila hatua,
Umeelezea sahihi kabisa sababu utajiri una mambo mengi na siri nyigi
 
Shukuru Mungu kwa kila jambo. Mungu ni mwaminifu siku zote.
Soma Zaburi ya 27.
Pole Sana.
 
Habari,

Nilizaliwa late 80’s ,Nimesoma mkoani na hakika watu wengi walinisifia kuwa nina uwezo mzuri darasani achilia mbali zawadi mbalimbali nlizokuwa nazipata shuleni enzi hizo,ilikuwa ni furaha sanaa kwangu na kwa familia yangu,Mimi ni mototo wa kwanza ktk familia ya watoto 5 na wengine niwa kike.

Nilimaliza msingi with flying colours nkapata nafasi mkoa mwingine shule ya boarding,nakumbuka tulifaulu 14 tu out of 288,nyumban watu hawakuisha kuja home niwafundishe masomo nakumbuka baba kuna siku alinyambia watu sio wazuri mambo mengine km unayajua husifundishe wapotezee jifanye hujui-kwa wakati huo nilikuwa sijui mshua anamaanisha nini?
Baba alikuwa na hali nzuri na biashara zake zilikuwa zinaenda poa sanaaa,pesa kedekede na miradi mingi hapa na pale in short mambo yalikuwa poa sanaa,madogo walikuwa wanasoma shule nzuri nzuri tu

Baada ya kumaliza form six na kupata nafasi udsm nakumbuka mtaan nlikuwa naokekana km msomi flani hivi na vijana wengi walitolewa mifano kwangu yaan nkawa role model wa mtaa mzima.

Baada ya kupata nafasi udsm ndio massive changes zilianza kuonekana ktk familia yangu,baba alifilisika kabisa kabisa kila kukicha ni habari za kuibiwa na wafanyakazi wanakimbia ata wale ndugu zake alioamua kuwapa nafasi kumsaidia kazi zake nao walikengeuka na kusepa na mali zake within 6 months mzee alikuwa taaban sana,madogo wote wakarudishwa shule za serikali na waliokuwa sekondari walipelekwa shule za gharama za kawaida mambo yalichange vibaya sanaaa.Huku kwangu mambo yalikuwa magumu sanaa nilikuwa naumwa kichwa kila siku yani kichwa icho hakielezeki maumivu yake muda wote nipo room hall 5(room no2670) nimelala kwa maumivu ya kichwa daaah.

Despite kuwa one of the best in class,nlipofika mwaka wa pili nilidisco masomo tena kwa GPA kitu ambacho mpk leo huwa sikubaliani nacho period,nakumbuka semester ya kwanza nlikuwa na GPA ya 3.2 ila semester ya pili eti nilipata F masomo yote 8-hii siku mama yangu alilia sana tena mbele yangu,Mkuu wa department alikuwa ananijua uwezo wangu aliniita na kuniuliza imekuwaje ,sikuwa na cha kumueleza zaid ya kumwambia ata mm sijui,aliniomba niandike barua ya appeal ataisimami,baada ya muda nkasikia eti ameteuliwa mkuu mwingine wa department na habar yangu ikashia hapo

Nlirudi kitaa kusikilizia appeal yangu mpk leo naisubiri tu,pesa ya kusoma tena familia yangu hawakuwa nayo nikatafuta kazi ya ulinzi nikaanza kufanya na nlivopata pesa kidogo nkaapply chuo kimoja hapa t own,nlisoma kwa shida ambazo hazielezeki ata kidogo.Huko nyumban mambo yalikuwa worse ile mbaya watu wakawa wanatucheka na kushangaaa nini kimetokea though watu wengi waliamini kuna mchezo mchafu unafanyika ktk familia yangu so wazazi wawe macho wasilale wala nini.

Wadogo zangu wote waliishia form 4 aseee,tena wameyumba kiasi kwamba wawili wamezalishwa na hawana msaada wamekaa home tu hawana pa kwenda wala kitu cha kufanya,baba hana kazi ata shilling mia hana ameyumba kupita kiasi,mama yangu anapika mama ntilie bubu pale mtaani,huwa naumia sanaaa nkiona maisha ya nyumban sasa hivi.

Hapa nilipo sina kazi yeyote nazulula tu mjini,nlishaomba kazi nadhan sehemu zinafika 500 ila hola mpk leo the worse thing ni kuwa wale washkaji zangu udsm wameshakuwa na life bomba sanaaa sa hv ila mm nasaga jiwe tu-hii huwa inaniuma kwelikweli

Simshutumu mtu yeyote kwa chochote pengine ndo maisha tunayotakiwa kuishi .Nina mengi ya kuandika kiasi kwamba zinaweza kufika ata page 100 ila kwa leo naishia hapo ujumbe wangu hapa ni ule ule usemi aloniambia baba “watu sio wazuri mambo mengine km unayajua husifundishe wapotezee jifanye hujui

Mwisho,Napenda niwaombe msamaha wote waliokumbwa na mawimbi kwa kuwa karibu na mm starting from Daddy ,najua mko wengine wengi sanaa mmeumia kwa njia moja au nyingene kwakuwa mko karibu yangu may be one day tutajua ukweli halisi what went wrong?.
pole sana ndugu mimi nakushauri anza mpango wa kutubu dhambi zako pamoja na za kurthi kutoka kwa wazazi na wazee wako kwa sababu dhambi hutafuna kizazi na kizazi hadi cha nne.

Ukitoka hapo nakushauri usiombe kazi wewe fanya kazi za kujitolea ofisi mbalimbali wahusika wakikupenda watakuajiri mambo ya kutembeza bahasha yamepita miaka ya sasa kwani watu wanaangalia skill and competence sio matokeo.
Huko kwenye volunteering jobs unapata uzoefu pia.
MUNGU akubariki.
 
Back
Top Bottom