2017 No Name
Senior Member
- Jul 26, 2017
- 172
- 133
Nilijua ni mimi tu napitia hili,..kumbe nna mwenzangu huku,.. I still believe in God.
I FULLY BELEIVE YOU MY BRO, this was likerly a contract btw his parents and the kingdom of darkness, either the father broke that covenant or refused to sacrifice a certain offering, most likerly one of his childrenBwana fox kutokana na maelezo yako mazuri inaonyesha vikwamo vyako na vya familia vipo kiroho. Kuna vifungo katika ulimwengu wa Kiroho ambavyo vinatakiwa kufanyiwa kazi. Usije shangaa baadae ukaja gundua kuwa wanao husika na vita hivi wakawa ni ndugu wa karibu kabisa katika familia, sijajua kuwa wewe ni mkristo au la hilo halijalishi. Tafuta uongozi wa kiroho kutoka kwa watumishi wa Mungu ili wakupe hekima na maarifa namna ya kupambana na vita hivi. Jua kuwa vita hii ni ngumu sana na unamuhitaji Mungu sana kuliko wakati wowote wa maisha yako.
Katika maombi utagundua mambo mengi sana na taratibu utaanza kukonect dots kutoka katika maisha yako ya udogoni, nyumbani kuhusu maisha ya wazazi na mambo ambayo wazazi walikuwa wakiongea na kukwambia. PIA usije shangaa kuwa wazazi wako wanahusika kwa anguko la familia kwa namna moja ama nyingine, kama ulivyosema kuwa baba alikuwa mfanya biasha mkubwa na maisha yalikuwa mazuri, inawezekana kuwa palikuwa na mikataba ya kishetani kwa ajili ya mafanikio ya kibiashara na makafara yalikuwa yakitolewa. sasa inawezekana baba alivunja mashariti ambayo ikawa ni sababu ya anguko la familia.
Unaweza uliza kuwa kwanini ikaathiri mpaka elimu ya watoto !!! YES yapo mashariti ambayo yalikuwa pia juu yenu, wakati mkiwa wadogo wazazi waliweza ku control maisha yenu ili msiweze vunja hayo masharti sasa baada ya kukua hasa wewe ambae ulitoka mbali na familia kuna vitu ulifanya ambavyo ni kinyume na masharti ya zindiko la baba ikachangia anguko zima la familia.
Kuna mambo mengi sana, haya nilioandika ni MTAZAMO wa kiroho kutokana na mtiririko wa kisa chako. Kama nilivyo sema inahitaji kujitoa kwa kiwango cha juu sana ili kuweza kufungua hii code iliyofungia maisha yenu. Inahitajika muongozo na msaada wa ROHO Mtakatifu katika kila hatua,
Duh!Pole sana kakaSo sad, pole sana![]()
![]()
Usikate tamaa ndugu, Mimi pia nimepitia story km yko. But ni kwa Mungu ndo yanawezekn japo level ya elimu nilinayo ni ndogo diploma. Ila mtumainie Mungu, I was the best from primary mpk nkachaguliwa special school. Ila miaka minne yote hyo minne niliugua sana, advance form five nkaugua Tb matibabu nilisaidiwa na mapadre maana msaada sikuwa nao, nilipomaliza treatment ya Tb form six nikachanganykiwa for one yr shule nkafutwa, nmekuja kujitambua wenzangu washamaliza advance na wamepangwa chuo kikuu. Wote wakanipotezea, sikukata tamaa nkabeba zege na kazi nyngnezo mpk nkaambuliwa kidiploma, nilichoajiriwa nacho serikalini. Bado inaniuma ila sijakata tamaa, hvyo nakuomba sahau yote pambana na kumtegemea MunguHabari,
Nilizaliwa late 80’s ,Nimesoma mkoani na hakika watu wengi walinisifia kuwa nina uwezo mzuri darasani achilia mbali zawadi mbalimbali nlizokuwa nazipata shuleni enzi hizo,ilikuwa ni furaha sanaa kwangu na kwa familia yangu,Mimi ni mototo wa kwanza ktk familia ya watoto 5 na wengine niwa kike.
Nilimaliza msingi with flying colours nkapata nafasi mkoa mwingine shule ya boarding,nakumbuka tulifaulu 14 tu out of 288,nyumban watu hawakuisha kuja home niwafundishe masomo nakumbuka baba kuna siku alinyambia watu sio wazuri mambo mengine km unayajua husifundishe wapotezee jifanye hujui-kwa wakati huo nilikuwa sijui mshua anamaanisha nini?
Baba alikuwa na hali nzuri na biashara zake zilikuwa zinaenda poa sanaaa,pesa kedekede na miradi mingi hapa na pale in short mambo yalikuwa poa sanaa,madogo walikuwa wanasoma shule nzuri nzuri tu
Baada ya kumaliza form six na kupata nafasi udsm nakumbuka mtaan nlikuwa naokekana km msomi flani hivi na vijana wengi walitolewa mifano kwangu yaan nkawa role model wa mtaa mzima.
Baada ya kupata nafasi udsm ndio massive changes zilianza kuonekana ktk familia yangu,baba alifilisika kabisa kabisa kila kukicha ni habari za kuibiwa na wafanyakazi wanakimbia ata wale ndugu zake alioamua kuwapa nafasi kumsaidia kazi zake nao walikengeuka na kusepa na mali zake within 6 months mzee alikuwa taaban sana,madogo wote wakarudishwa shule za serikali na waliokuwa sekondari walipelekwa shule za gharama za kawaida mambo yalichange vibaya sanaaa.Huku kwangu mambo yalikuwa magumu sanaa nilikuwa naumwa kichwa kila siku yani kichwa icho hakielezeki maumivu yake muda wote nipo room hall 5(room no2670) nimelala kwa maumivu ya kichwa daaah.
Despite kuwa one of the best in class,nlipofika mwaka wa pili nilidisco masomo tena kwa GPA kitu ambacho mpk leo huwa sikubaliani nacho period,nakumbuka semester ya kwanza nlikuwa na GPA ya 3.2 ila semester ya pili eti nilipata F masomo yote 8-hii siku mama yangu alilia sana tena mbele yangu,Mkuu wa department alikuwa ananijua uwezo wangu aliniita na kuniuliza imekuwaje ,sikuwa na cha kumueleza zaid ya kumwambia ata mm sijui,aliniomba niandike barua ya appeal ataisimami,baada ya muda nkasikia eti ameteuliwa mkuu mwingine wa department na habar yangu ikashia hapo
Nlirudi kitaa kusikilizia appeal yangu mpk leo naisubiri tu,pesa ya kusoma tena familia yangu hawakuwa nayo nikatafuta kazi ya ulinzi nikaanza kufanya na nlivopata pesa kidogo nkaapply chuo kimoja hapa t own,nlisoma kwa shida ambazo hazielezeki ata kidogo.Huko nyumban mambo yalikuwa worse ile mbaya watu wakawa wanatucheka na kushangaaa nini kimetokea though watu wengi waliamini kuna mchezo mchafu unafanyika ktk familia yangu so wazazi wawe macho wasilale wala nini.
Wadogo zangu wote waliishia form 4 aseee,tena wameyumba kiasi kwamba wawili wamezalishwa na hawana msaada wamekaa home tu hawana pa kwenda wala kitu cha kufanya,baba hana kazi ata shilling mia hana ameyumba kupita kiasi,mama yangu anapika mama ntilie bubu pale mtaani,huwa naumia sanaaa nkiona maisha ya nyumban sasa hivi
Hapa nilipo sina kazi yeyote nazulula tu mjini,nlishaomba kazi nadhan sehemu zinafika 500 ila hola mpk leo the worse thing ni kuwa wale washkaji zangu udsm wameshakuwa na life bomba sanaaa sa hv ila mm nasaga jiwe tu-hii huwa inaniuma kwelikweli
Simshutumu mtu yeyote kwa chochote pengine ndo maisha tunayotakiwa kuishi .Nina mengi ya kuandika kiasi kwamba zinaweza kufika ata page 100 ila kwa leo naishia hapo ujumbe wangu hapa ni ule ule usemi aloniambia baba “watu sio wazuri mambo mengine km unayajua husifundishe wapotezee jifanye hujui”
Mwisho,Napenda niwaombe msamaha wote waliokumbwa na mawimbi kwa kuwa karibu na mm starting from Daddy ,najua mko wengine wengi sanaa mmeumia kwa njia moja au nyingene kwakuwa mko karibu yangu may be one day tutajua ukweli halisi what went wrong?.
I'm suffering the same. Maisha haya ni Mungu pekee anae jua hatma zetu! Sijui nilikosea wapi!Ndugu yangu umenifanya nitoke chozi, a friend of mine has been gone the same way as yours na mpaka sasa anahangaika mpaka huruma. Histori zenu zinafanana kuanzia familia ingawa yeye baba ake alifariki kitambo na mama ake ni mfanyakazi wa kawaida tu shirika la posts. Uwezo wake ulikuwa wa juu darasani na hata rafiki zake A level, Udsm wanatestify hilo lakini 2nd year 2010 akiwa anafanya Bcom in Management Science alidisco kwa GPA ya 1.6. Pamoja na kuappeal, shauri lake halikusikilizwa na kuna waliokuwa na GPA ya 1.5 walifanyiwa mambo wakaendelea. Now amepoteza marafiki zake aliokuwa nao chuo, hakuna msaada basi dah. Anatafuta kazi ya ulinzi atleast hata apate ya kula tu.
Kuna vitu vingine tukijiuliza inabaki kumwachia Mungu tu
Sent using Jamii Forums mobile app
I'm suffering the same. Maisha haya ni Mungu pekee anae jua hatma zetu! Sijui nilikosea wapi!
God help us, forgive us where we went wrong and give light to this dark world of ours. Amen.
Nimekujibu pm mkuu.Upo mkoa gani kaka?
Nimekujibu pm mkuu.
Ahsante boss.Nimeona mkuu
Dah mi sina cha kusema
Sasa kwako ilikuwa nini? Manake umesema huamini kama ilikuwa uchawi!Mleta mada nilipitia hayo unayopitia, siamini kama ilikuwa ni uchawi au ni nini lakini kuna mwanamke alias’s kunifix. Kwa miaka kama kumi kila nilichoshika kilianguka.
Sali sana na umuombe Roho Mtakatifu msaada wa duvine connection na Mungu.
Ni sawa. Mimi pia nayapitia hayo. Naamini Mungu ni mwema ataonyesha njia!Sijui mkuu lakini kwa miaka kumi nilisimama. Nilikutana na mtu kwenye basi simju hanijui aliniambia nisali sana Rosary. Ni matukio mengi yaliyokea moja ni kuwa ni kuwa kwenye ndoto Bikira Maria alitokea akanibeba kutoka katikat ya kinyesi na mikojo niliyokuws nimelalia kutoka pale mambo yalibadilika sana. Lakini nilifunga sana na kusali.