Jifunze jinsi ya kuunda vifaa vya umeme

sumu-ya-panya

JF-Expert Member
Aug 6, 2016
632
572
Ijapokua Elimu kuhusu vifaa vya umeme inahitajika pia kuna open project kadhaa wa kadhaa ya vifaa hivi (schemastic) bure.
Wengi tumekua tukiaminishwa kuwa wachina na wazungu wanaakili sana ndio maana wao wanakuwa wabunifu wa vifaa vingi vya umeme.
tatizo kubwa litakalotushinda sisi watanzania ni PCB manufacture ingawa kuna method za kutengeneza PCB body kirahisi.

hapa tunaweza fungua wajasiriamali wengine watakao tengeneza vifaa bora zaidi ya vile vilivyopo vya kichina.
mfano unaweza tengeneza Taa zinazojiwasha zenyewe kwa kuangalia uwepo giza au kwa muda maalumu.
ubunifuni wa vifaa hivi hauhitaji gharama kubwa sana kama vile vinavyouzwa na wachina au vingine vinakuwa dhaifu kutokana na matumizi ya part hafifu.

mfano gharama za kuunda automatic light switch by times gharam yake na vifaa
IC555 timer === bei ni 1000/=
transistor 2pcs BC547 ===bei ni 1500 mbili
capacitor tatu 100uf === 1000/
resistor 1n === 100/=
resistor 47k ==== 100/=
resistor 4.7k ==== 100/=
resistor 430n ==== 100/=
resistor 330n ==== 100/=

kwa idadi hii ya vifaa hivi unapata hesabu litakalo kua off kuanzia saa 1 asubui mpaka saa 12 jioni na kuja kuwa on kuanzia saa 12 na dakika 1 mpaka saa 12 na dakika 59.

watuwengi wamekua wakiamini mifumo hii mfano taa za barabarani zina tumia teknolojia kubwa sana kivile kumbe ni mahesabu pekee. na wanapoona hesabu ni kunasiku jua linachelewa au kupatwa kwa jua basi wanatumia sensor za light badala ya hesabu.
hapa tukumbushane yale mahesabu ya darasa la kwanza kwenye mti pana ndege watano ukitoa wawili watabaki wangapi linatumika hapa bila sisikufikiri kwa kina,

au gari linatembea toka kituo A mpaka kituo B kilometa kazaa kwa muda wa saa 3,mtu wa kitua A hufika kituo C ambacho ni kilometa kazaa tafuta muda gari litasafiri hadi kituo C

Natamani hawa mafundi redio sasa wangeongeza thamani ya ujuzi wao kwa kuacha kurepair na kuunda vifaa vitakavyowezesha kukuza vipato vyao na hata nchi kwa ujumla.

wengi hufikiri waundaji wa vifaa hivi ni wataalamu sana hata wakabuni kwa akili zao pekee .ukweli ni kwamba wanatumia software za CAD zilizojazwa akili na hesabu zima na hata kutest kwa kutumia computer zao. baada na kutest design yake katika computer na kufanya vizuri muundaji huyu huunganisha parts zote katika breadbord na kuona kinadharia ubunifu wake uko sawia na CAD software unapokua sawa huprint katika pcb body na kufanya assembly na kupata motherbody (controller ya kifaa anachotaka kutengeneza..
kisha huamia kwenye covers na body shape ya kifaa chake na bidhaa kuingia tena katika testing baada ya assembling.
kisha kuingia sokoni kwa bei atayolinganisha na zilizopo sokoni.

Miongoni mwa softwire izo ni circuit wizard,eagly pcb,pcb wizard etc software hizi zipo trial na huwa na limeted function kuna baadhi ya vitu haifanyi au haitoi majibu ya kweli ikiwa ni trial mode. ni vizuri mtu kulipia au kununua softwire keys ili aweze kuwa huru kufanya chochote.

zipo softwire na design nyingine kwa hapa Tanzania sio rahisi kufanyika pasipo kuwa na daraja fulani katika electronics mfano engineer hawa hudesign na kutoa schemastic itayoenda fanyiwa assembly. na zingine zinahitaji tehnolojia zaidi kama vile mashine maalumu ambazo ni kampuni kadhaa humiliki na huchukua tenda toka katika makampuni na kutengeneza.
mfano unataka tshirt ya rangi fulani yenye mandishi fulani kwa stail fulani na rangifulani itakulazimu kumfata anaefanya screen printing n.k

Kwa kutumia method za kutengeneza PCB hapa inakulazimu kupata cooper body,printer ya kawaida, chemikal ambazo hazijazuiwa kutumika na zinauzwa kwa yeyote zisizo na madhara.

unaweza search jinsi ya kutengeneza PCB body tazama youtube zipo nyingi.

Kwa mimi nina softwire ya circuit wizard 3 full ambayo ni inafanya shughuli zote na ni life time. ikiwa inasupport Ic nyingi n a pia ina empty ic ambazo utaziingizia akili kwa kufuata schematic ya ic husika..

kwa wanaohitaji unaweza ni PM na kuchangia kiasi kidogo zaidi nikakupa copy ya dvD original.
pia unaweza search cracked softwire zilizoconfused na kutoa majibu yasio sahihi kwa baadhi ya project.

Mimi nilipata DVD hii toka kwa Mzungu alienikuta nikiunganisha kifaa cha umeme kwa akili yangu binafsi kinyume kabisa na mifumo sahihi alipenda nilichokua nafanya na kuniahidi kunipa kitu kitachonisaidia,nimetumia softwire hiyo kwa kucopy schematic za wenzetu njee na kisha kutoa pcb na kufanya assembly katika breadboard pekee...

Natamani mafundi redio,tv,umeme kuongeza fursa za kukuza kipato chao kwa kuwa wajasiria mali na kuanzisha viwanda vidogo amabavyo havita hitaji wataalamu sana wa kufanya assembly na pia kukuza uchumi wa taifa letu .

serikali/veta kuhimiza na kutoa elimu kwa wa nafunzi na mafundi kuwa wabuni na kuachana na dhana moja ya kusema niwe fundi milele. ikiwa unaweza kitibu basi kukiunda utaweza kwa msaada wa teknolojia.
 
Marekebisho printer sio za kawaida (ink) ni laser printer na ni expensive unless upate ubahatike za bei rahisi.
Sioni haja ya kuchangisha watu kama una nia ya kuwasaidia, umeanisha mwenyewe ulipewa bure, kwanini uuze.
 
Ili mtu uone thamani ya kitu basi kigharamikie ukithamini na ili thamani yake irudi kifanyie kazi
 
mkuu sumu-ya-panya hongera kwa uzi mzuri
hebu tuendelee sasa ili tufike mwisho..
maana nimesoma nimemaliza..
Mfumo wa elimu wa ya nchi yetu ndo unatufanya tuwe wavivu wa matumizi ya fikra. leo kumpata kijana anatumia internet kujifunza jambo fulani ili limwingizie kipato ni ngumu.

Nilipokua mtoto miaka 4 nilipenda kucheza kwa kuunganisha balbu iwake katika utoto uwo na wenzangu tuliamini chaji inapita kwenye waya tu. lakini nikagundua kumbe chuma nayo tukaunga vyuma vingi kusafirisha chaji hadi katika balb.
tukoa hapo mtaani kulikua na wanatengeneza magari,kuna anaedeal na kuchunguza wadudu,gar likiundwa litaletwa niliweke,wapo watengeneza barabara,na walikua wacheza kamari pia kwa Gololi.

Yapo mambo yaliyopendwa na wote kuwinda na viumbe watakaopatika watafugwa na kuthaminiwa hapa mashindano ya nani wanyama wake (sungura,kanga,kware) wanafuraha na afya wazazi walisupport hili kwani ushindani ule ulileta kipato nyumbani na kuchochea ari zaidi na kupata msukumo toka kwa wazazi.

Tuliweza kwenda shule moja ambayo kuna umbali wa kilometa 3 na unapita katika pori,na wengi wa umri wa kwenda shule tulienda shule moja huko tukakutana na wengi walikua wakituringishia walivyotengeneza hasa vitu vya asili tuliumia na tukaanza jifunza,na kwakua wale walikua hawatokei sehem za mjini tulipojua tulipeleka nyumba kamba ,mwiko,rungu,vipekecho,upinde,ukili n.k ikawa kila tunachoona wakubwa wanafanya lazima watufunze au watu icho kitu tukatoe copy.

Leo yule aliekua akideal na kuchunguza wadudu ni daktari,walikua wakicheza gololi ni wamishem town,kamari,na wenye ushawishi .
walikua wakiunda magari wengine walipenda kabisa magari ni madereva,wengine mafundi gereji wakubwa.
wale kitengo cha umeme tulijikita katika electronics na tecnolojia zaidi.

Iwapo nafasi ingepatika na familia zikawa na kipato cha kuendeleza watoto wao au serikali kuendeleza wale wenye ujuzi na kupenda tasnia fulani,leo taifa letu lingekua na wataalam wengi ambao wangejituma kukuza uchumi wa taifa letu.

Kiukweli niwe muwazi sijawihi ingia darasani kujifunza ufundi simu wala computer.niloichojifunza darasani ni Computer basi tena basic course ambayo nilisoma kwa wiki 2 na kufanya mtihani kenya. siku mbili nilichoshwa na kusoma nusu saa nikarudi home nikasoma masaa 8 nikamaliza nikarudi nikaomba nifanye mtihani na wale walikua wanatangulia nikafanya na kufaulu vizuri niomba nipewe cheti kisha nisitishe kusoma.

tokea hapo mimi nikawa mtu wa kujifunza kwa msaada wa mtandao. mtaani kuna mafundi simu wengi simu zikiwashinda zina kuja kwangu. nilipoona sana ufundi ni uvivu niliamia kujaribu kubuni taa amabzo ningetumia nyumbani na kwakua mimi nachelewa kurudi basi taa ziwake zenyewe nilifanikiwa kuunda na kuistall nyumbani.
sikupenda kuweka solar sababu ya gharam nilichukua bettry ya simu nokia. nikabomoa taa za led za bettry za redio nikatoa led diode nikaunga zile zenye mwanga mkali sana , kisha nikaset batry holder ambayo. sasa na tumia bettry ya simu kama power source. itakaa siku 8 ntaitoa na kuichaji
 
big up sana mkuu .hiyo story yako imenikumbusha mbali sana.mm kitu nilichokipenda utotoni mpaka leo hii nakifanya na kilinivuruga kabisaa akili.nilipenda sana ufundi nampaka leo hii naupenda sana ufundi. nakumbuka baada ya kumaliza darasa la saba nilikomaa kwenda veta mzee akanambia hapana marks zako ni za sekondary nilienda TOSAMAGANGA kwa shingo upande lkn nilipo maliza hapo nilipiga brake.nakumbuka nikiwa form 1 watu wa form 4 hesabu za physics topic ya umeme wakinitafsilia kwa kiswahili nawafanyia vizuri sana.hasa yale maswali ya kuelezea sijui taa A na B zimeungwa series taa A ikiungua taa B itawaka na kwa nini??

nakumbuka nimeanza kuendesha trekta darasa la 5 la sita nikawa nashinda gereji nikitoka tuu shule.

nilifika veta chang'ombe nashangaa kila alichonifundisha mwalimu nakifaham kwanza nilifika kwa kuchelewa sana zilibaki kama wiki 3 hivi kufanya mtihani nafika wanafundishwa starter sijui otoneta mwalimu akanambia nikamletee starter nikamletea.mbona nilikaa wiki moja nikawa sishindi tena darasan nikawa nyoka wa mwalimu.
 
Haya kiongozi mi ninazo atakayehitaji bure nitamsaidia hata link.
mkuu naomba unisaidie mm hata ukisema kwa pesa nitachangia haina shida siku zote kizuri ni ghali na vyabure havinaga ubora.naamini kwenye ufundi wangu wa umeme wa magari itanisaidia hasa kwenye sekta ya kupimp gari
 
Ukisema vya bure havina ubora unakosea, hata material, tutorial, na articles mbalimbali mitandaoni ni bure yet watu wanajifunza na kujipambanua mkuu.
 
Ukisema vya bure havina ubora unakosea, hata material, tutorial, na articles mbalimbali mitandaoni ni bure yet watu wanajifunza na kujipambanua mkuu.
sijakosea mkuu bali umekosea kunielewa ni kuwa ukinipa bure au siku zote kitu unachokipata kwa free bila kutumia jasho kamwe kukitunza au kukidhamini huwa inakuwa sio kwa kiwango cha juu sana.tukiachana na hayo fanya mpango basi mkuu
 
Ok kiongozi ulikuwa wahitaji nini.
 
Mkuu nitakupataje maana mimi pia ishu ya circuit printing na case design imekua changamoto sana nina circiuit nyingi nataka kudesign ila nimefail hapo sijui nitakupataje
 
sijakosea mkuu bali umekosea kunielewa ni kuwa ukinipa bure au siku zote kitu unachokipata kwa free bila kutumia jasho kamwe kukitunza au kukidhamini huwa inakuwa sio kwa kiwango cha juu sana.tukiachana na hayo fanya mpango basi mkuu
Haya circuit wizard aliyokuwa akiizungumzia mtaalam hapo juu, ya ku design PCB link zipo chini.
1.jpg

2.jpg

Link setup
Link installation instructions
 
Back
Top Bottom