jerryempire
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 5,128
- 8,648
Habari wapendwa
Imenichukua muda mrefu mno kuandika hii mada lakini imenisukuma tu niandike baada ya kuweka namba yangu kwenye thread fulani humu jamii forum
nimepata simu zisizopungua 30 kutoka kwa watu humu,kuhusiana na masuala mbali mbali yanayowakabili,hizo dm's ndo nyingi mno,itoshe kusema mimi siyo mganga wala mchawi sema maswahibu niliyopitia ni mengi.
kiasi cha kunipelekea kujifunza mengi san sababu,nilishakutana na magwiji wakubwa wa masuala hayo na kuyashuhudia mengi mazito mpaka mengine yakasababisha kuniachia makovu na alama za maisha kwa ambao walisomaga thread yangu humu mnaweza kupata picha halisi.
nitakacho andika ni kile ninachokijua kuhusu masuala mazima ya uchawi hasa jinsi gani unaweza kuchezewa/kujikinga nao na kuhusu majini sababu nayajua na nilishawahi kuyaona na yapi niliyoyaona na utajuaje kuwa uko na jini n.k
NB:
KILA UTACHOTAKA KUKIJUA KUHUSU TIPS NTAZOKUWA NAZITOA, TAFADHALI KAMA UTAKUWA NA SWALI AU LOLOTE NIULIZE AU ULIZA HAPA HAPA KWENYE THREAD NTAKUJIBU SITOJIBU DM WALA SIMU YA MTU NA SIHITAJI PESA YA MTU HVYO SITOTOA NO NA HATA UKIIPATA SITOKUSAIDIA KOKOTE ZAID YA KWENYE THREAD HII KWA MANUFAA YA WENGINE.
UFAHAMU UCHAWI
Wengi ukiwauliza uchawi ni nini watakuwa na tafsiri tofauti lakini hauna maana moja ya kuuelezea,
uchawi umebeba maana nzima ya kuumbwa binadamu na ulimwengu kwa ujumla na ndio,lango kuu linalotumika kuwaunganisha binadamu,mungu,majini,na hata malaika iwe kwa uasi na hata kwa uzuri (toba)
unaweza kujiuliza uchawi unahusikaje na kuumbwa kwa binadamu?
vizuri, Kabla ya kuumbwa binadamu waliumbwa malaika na majini ambao walikaa ndani ya dunia hii miaka na miaka kabla ya kuja kuumbwa sisi binadamu
Aliumbwa adamu na kutokana na upweke wake akatolewa eva/hawa kutokana na pande/ubavu wa adamu ili awe faraja na furaha kwa adamu, na hapo ndipo ilipotokea fitina kubwa ambayo ilimgharimu shetani kufukuzwa mbinguni baada ya kumuasi mungu pale alipoambiwa amsujudie adam.
Mungu alimuumba binadamu kisha akasema kuwa amemuumba binadamu kwenye umbile bora akimaanisha ni kiumbe bora kuliko chochote alichowahi kukiumba,hii ndo kauli ambayo huenda ikawa sababu kuu ya kutokea kwa uchawi na maovu mengi duniani twende pole pole utanielewa hapo baadae,
kuna aina kuu nne za uchawi,
1.UCHAWI WA MAJINI,
Huu ndio uchawi mkubwa na mzito kuliko uchawi wa aina yoyote kwani kafara zake huwa ni kubwa mno na ni level nyingine ya uchawi ambao kama ukifanyiwa ni mkubwa hasa wa baharini,sababu huko ndiko kwenye falme nzito za uchawi.
uchawi huu huhusisha,mito,bahari na maziwa,
uchawi wa aina hii mtu huupata kwa kwenda katika falme za hayo maeneo husika na kukubaliana na masharti ya hao viumbe wa sehemu hizo,na mchawi wa aina hii yeye huwa anasafiri/kwenda kuabudj maeneo ambayo ni jirani na maeneo hayo tajwa hapo.
uchawi wa aina hii mtu huweza kudhuriwa kwa mchawi husika kuchanganya vitu vinavyopatikana ndani ya bahari,ziwa,au mito au mtu anayefanyiwa uchawi kupita katika maeneo hayo au kuwa mfanyaji kazi kwenye maeneo hayo.
2. Uchawi wa pili ni wa anga
Huu ni uchawi ambao mtu huweza kuathiriwa kwa kufungwa kupitia upepo,kimbunga,dhoruba,radi,n.k
uchawi wa aina hii hunuwiwa kumfikia mhusika kwa njia hizo mfano mnaweza kuwa mmekaa tu sehemu ikaja radi lakini hyo radi badala ya kuwapiga watu ote ikampasua mmoja tu kati ya watu 20 wa eneo hilo.
3,Uchwi wa pili ni wa ardhini
huu ndo uchawi unaotumika zaidi katika jamii za wachawi wengi kwani huhusisha mizimu ya asili na kila kilichomo aridhini.
uchawi wa aina hii unaweza kumpata mhusika endapo atachukuliwa kitu kimoja wapo kati ya kivuli,kitovu,nyayo nk
4,uchawi wa moto
huu ni uchawi ambao mhusika akifanyiwa huungua au hata kama ikitokea ajali basi lazima ajali hyo ihusishe moto kuwaka au wahusika kuungua moto.