Jifanyie mazishi ungali u hai

Jifanyie mazishi ungali u hai

bahati93

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2015
Posts
1,567
Reaction score
2,966
Kuna mambo ya ajabu mbalimbali yanayotokea kwenye ulimwengu tunaoishi mpaka yanakufanya mtu kuwa na wasiwasi juu ya uhalisia (je ni ninaota au ndo uhalisia!) kifrika hayaingii akilini (kwanini kaamua kufanya maamuzi yale, kwa nini walimwengu wana fanya wafanyao ambayo siafiki nayo, nk). Basi kama umeshawahi kutwama kwenye mawazo yanayoendana na haya ungana nasi kwenye njia hii mbadala ambayo tangu enzi na enzi yafikiriwe na wanasalfasa mashuhuri (Zeno, Marcus Aurelius) haijawahi kurekebishwa kwani yametukuka busara.

Kwanza kabisa yakupasa kuhudhunika na kukiri ukingo wa ewezo (kufikiri, kuimba, utajiri, upendo, mahusiano, Amani, nk) ambao tunao binafsi, huu ni uhalisia upo pande zote za dunia endapo utafanikiwa kudhuru utakuta watu mbalimbali na kila mmoja kwa namna moja au nyingine kuna kitu hawezi kufanya kwa ufanisi unaotakiwa angali anataka kufanya Lakini kutokana na alivyoumbika na makuzi aliyokulia yanashindikana kutokea. Basi fanya mazishi kwa mawazo na roho ambayo inakushawishi kwamba yote yanawezekana.

Hamna haja ya kuangaika na vitu ambavyo vipo nje ya uwezo wetu. Kitu kilicho chetupekee ni mawazo yetu tuu vingine vyotee vipo nje ya uwezo wetu. Fanya mazishi ya vitu vyote vya thamani unavyohitaji, fanya mazishi kwa kukosa watu wa karibu kukupa mwongozo katika jinsi ya kuishi.

Kwa kufanya mazishi ni kukubali yote yanayotokea katika maisha yako kuwa yanategemea uwepo wako ili yatokee.
 
Inawezekana ngoja nisome vyema kwanzaa
 
Back
Top Bottom