Jack Daniel
JF-Expert Member
- Sep 23, 2021
- 4,815
- 19,483
Salaam jamiiforum.
Dunia inaenda kasi, mitindo ya maisha inabadilika,watu wengi wanakata tamaa.
Asiye na pesa anadhani tatizo lake ni kutokuwa nazo ndiyo maana anateseka? Yes swali ni lenye maumivu,ambapo majibu yake ni kufanya kazi na si kingine.
Fanya kazi Kwa kiasi na uwezo wako,buni vitu na vyanzo vipya vya mapato.
Usipelekeshwe na misemo ya tafuta pesa,utaugua magonjwa si yako,fanya vitu Kwa wastani.
Usiisubiri Sana Ajira hata kama Una Elimu nzuri inayoweza kukupa kazi nzuri ,badala yake shughulisha ubongo Kwa kubuni vitu vitakavyokupunguzia Mawazo.
Starehe zipo tu,
Mademu wapo Tu,
Vilikuwepo,vipo na vitaendelea kuwepo.fanya Kwa wastani.
Acha kuiga kila kitu,
Najua utaumia kuona vijana wa umri wako au uliowazidi Wana mafanikio kukuzidi.usifanye hivyo wewe kimbiza mwizi kimya kimya.
Ngoja nikupe mfano hai,
Miaka fulani wakati nasubiria kazi na elimu yangu ya kuungaunga nilipata kazi isiyo rasmi ya kumuendesha boss wa kiarabu Kwa malipo duni Sana.
Nilikula vizuri,nilivaa vizuri kwani anachokula boss ndicho nilichokula lakini nilinunuliwa nguo nzuri na boss ili kuwa na good appearance mbele za watu,ila sikuwa na pesa hata chenji ndogo ikibaki boss aliiulizia,na nilimpatia.
Ndani ya miezi mitano nikagundua sina akiba yeyote,zaidi ya umaarufu fulani niliopata Kwa kufahamika kwenye hotels, filling stations,na benki wengi waliniona kama mtoto wa kishua niliruhusiwa kutoka na gari na kwenda popote,sikukatazwa ila sikuwa na pesa ni kama nilifungwa.
Nikaamua kuacha kazi hiyo iliyonipa mademu,na kuamua kuungana na vibarua wenzangu kwenye kazi za kusaidia mafundi ujenzi.huku nikiomba kazi huku na huko.
Naam,nikiwa na miezi miwili kwenye kazi ngumu, kazi isiyo jali muda wa kutoka ni mpaka fundi achoke au apate dharula.
Boss wangu alinitafuta na kudai kwanini nimeamua kutoka kwake? na kujiingiza kwenye kazi ngumu sioni anateseka?,nilimjibu kiume na kijasiri kwamba kazi yake ina maslahi madogo na Mimi umri unasogea nitawezaje kujitegemea na kujiongoza?
Boss wa kiarabu akaniambia nipeleke CV zangu kwenye kampuni moja ya ndugu yake,nimtaje yeye na akanihakikishia nitapata kazi.
Naam kila kitu kilienda vizuri, kumbuka kama nisingefanya maamuzi ya kutoka kwake huenda ningeishia kuwa dereva na kupata umaarufu usio na faida .
Ndani ya miezi miwili ya kusaidia fundi nilisevu kiasi cha shilingi 48000 akiba ambayo niliifurahia kwani ilitokana na jasho halali .kwangu ilikuwa pesa nyingi.
Ewe kijana mdogo amua leo Una viungo vyote ,wewe si mlemavu Acha ubishoo fanya kazi au kibarua chochote,mambo mengine yatakuja tu