Jicho letu laangaza viunga vya jiji la arusha.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jicho letu laangaza viunga vya jiji la arusha..

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngofilo, Jul 10, 2012.

 1. Ngofilo

  Ngofilo JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 214
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  [h=2]katika pita pita zangu nimekutana na habari hii kwenye blog mbili tofauti ila mwandishi akiwa huyo huyo mmoja. blog ni ya Jamii na media2solution.

  JICHO LETU LAANGAZA VIUNGA VYA JIJI LA ARUSHA.
  .[/h] July 10, 2012 by Pamela Mollel  Jicho Letu lilipoamua kuzungukia jiji la Arusha pamoja na viunga vyake lilikumbana na kadhia pamoja na taswira ya kustua, Jicho likabaki katika hali ya sintofahamu na kujiuliza je hili ndilo lile jiji la kitalii linalo pendekezwa kuwa makao makuu ya Jumuia ya Afrika Mashariki?
  [​IMG]TASWIRA YA MITARO KATIKATI YA JIJI LA ARUSHA JUMATATU JULAI 9, 2012


  Awali Jicho lilisikia sifa ya Jiji hili zikivuma kuwa sehemu hii ni Geneva ya Afrika. Jicho Letu likaamua kufunga safari kuzuru Jiji hili lisilo na Madiwani wala Mbunge.
  [​IMG]SEHEMU YA KITUO KIKUU CHA MABASI JIJINI ARUSHA IKIONYESHA TASWIRA YA UCHAFU ULIVYO TAPAKA JUMATATU JULAI 9, 2012


  Safari ya Jicho Letu ilianzia Kituo cha mabasi! Mazingira ya Kituo Kikuu cha mabasi yalilishangaza Jicho Letu, hali ya uchafu wa kupindukia, chupa zilizo tapakaa harufu za mikojo zilitosha kuliaminisha Jicho kuwa wale waliosema kuwa jiji la Arusha ni Genever ya Afrika walisema hivyo kwasababu za kisiasa tu.
  [​IMG]SEHEMU YA VIJANA WANAO SHINDA BILA KAZI KATIKA MAENEO YA KITUO KIKUU CHA MABASI JIJINI ARUSHA HUKU MALI YA UCHAFU IKIONEKANA WAZI WAZI JUMATATU JULAI 9, 2012


  Uchunguzi wa Jicho Letu uligundua pamoja na uchafu ulio tapakaa vilevile katika Kituo hicho kuna vijana wengi wasio na kazi maalum bali hushinda maeneo hayo wakivuta bangi hadharani bila ya vyombo husika kuwachukulia hatua stahiki. Jicho lilistaajabu pale lilipo waona askari wakipita na kuvifumbia macho vitendo hivyoÂ…. Hapo Jicho Letu likapata taswira huwenda pia askari hao walikuwa likizo au nao ni watalii.
  [​IMG]MAMA LISHE WAKIWA WANAFANYA BIASHARA KATIKA SEHEMU HATARISHI ZA KITUO KIKUU CHA MABASI JIJINI ARUSHA JUMATATU JULAI 9, 2012


  Pamoja na uchafu huo kutapakaa sehemu hii ya Kituo cha mabasi yaendayo mikoani Jicho Letu liliwakuta Mama Lishe wakitoa huduma za vyakula katika mazingira hatarishi bila kuhofia magonjwa ya mlipuko kutokana na mazingira ya uchafu hali iliyotishia afya za walaji. Jicho lilipata bahati ya kuongea na Mwananchi mmoja ambaye aliliambia jicho hili kuwa hali ya uchafu katika maeneo hayo imezidi kuchukuwa kasi huku halmashauri husika ikionyesha kushindwa kabisa kuidhibiti hali hii. Kwa upande wao Mama Lishe hao wanadai kuwa wamekuwa wakiilipa halmashauri ya Jiji la Arusha fedha za kuuzia eneo hilo zinazochukuliwa na kampuni inayokusanya ushuru wa geti na magari yanayoingia na kutoka katika Kituo hicho.
  [​IMG]WACHUHUZI WAKIWA WANAENDELEA KUFANYA BIASHARA ZAO MAENEO YA KANDO KANDO MWA BARABARA KATIKA VIUNGA VYA JIJI LA ARUSHA JUMATATU JULAI 9, 2012


  Jicho Letu liliamua kutoka maeneo ya Kituo Kikuu cha mabasi, njiani lilishindwa kujuwa kama liko Arusha au liko jijini Dar es Salaam tena kipindi kile ambacho mtaa wa kongo ulikuwa maarufu. jicho Letu liliwaona wafanyabiashara alimaarufu machinga wakiwa wamepanga bidhaa zao mbele ya maduka hali inayofanya msongamano katika barabara kadhaa za jiji hili na mabaraza ya maduka. Jicho Letu lilipata kadhia pamoja na kuwa lilikuwa linatembea kwa miguu. Wafanyabiashara pamoja na wananchi wameitupia lawama halmashauri yao kwa kushindwa kutatua tatizo hili. Wengine walidai kuwa chombo hicho kinaogopa kuchukuwa hatua za kisheria kutokana na sababu za kisiasa huku ikitoa visingizio Lukuki bila ya majibu yakinifu.
  [​IMG]TASWIRA YA MBELE YA SOKO KUU LA JIJINI ARUSHA JUMATATU JULAI 9, 2012


  Jicho Letu lilipofika Soko Kuu lilikaribishwa na rundo la taka, Jicho Letu liliendelea kustaajabishwa na rundo hili la takataka zilizopo pembezoni mwasoko. Uchafu umerundikana na kufanya sehemu hii muhimu yanapo patikana maitaji muhim ya kila siku kwa wakazi wa jiji hili kuwa hatarishi na kero kubwa kwa wafanya biashara pamoja na wanunuzi. Katika hali ya kushangaza Jicho Letu lilimuona kijana mmoja wa makamu akiwa amejipumzisha katikati ya rundo hilo la taka, bila kujari harufu kari iliyokuwa inajitokeza sehemu hiyo yeye aliendelea kulala usingizi. Jicho letu halikufanikiwa kupata jina lake wala muda wa kuongea nae.
  [​IMG]MMOJA WA WAFANYABIASHARA YA MBOGOMBOGA AKIWA AMEPANGA BIDHA ZAKE CHINI KATIKA SOKO KUU LA JIJINI ARUSHA JUMATATU JULAI 9, 2012


  Katika maeneo hayo ya Soko Kuu Jicho Letu liliwakuta wakinamama wakipanga bidhaa zao chini hali inayohatarisha mazingira ya walaji. Taswira hizi zililifanya Jicho letu kuchoka kutazama! Lika amua kwenda kujipumzisha na kupanga kurudi siku nyingine katika jiji hili lenye sifa nyingi. Njiani Jicho Letu likawa lina tafakari matokeo ya uchunguzi wake, hasa pale lilipo ambiwa Halmashauri hiyo ya jiji la Arusha kwasasa imejikita kushughulikia ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali (CAG), Jicho Letu lika jiuliza je? Bwana afya anafanya kazi yeke kweli?
  [​IMG]KITUO KIKUU CHA MABASI CHA JIJINI ARUSHA JUMATATU JULAI 9, 2012


  Likapanga likipata muda tena wa kutazama lazima litatembelea ofisi za wakuu hao. Hali hii ya kutelekezwa jiji hili ni moja ya taswira mbaya na ya kukatisha tama ambayo Jicho lime jione Mwezi huu.


  [​IMG]
   
 2. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #2
  Jul 10, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,753
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Yeah_jiji kwa sasa ni chafu sana,..ila sio arusha tu hata dar ni chafu na pengine zaidi....kwa hiyo kama ni mkakati uwe wa nchi nzima mkuu
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  Jul 10, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Arusha si Geneva ya africa....lol
   
 4. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kazi nzuri sana na umeeleza ukweli lakini hapo juu naona umekosea.
   
 5. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #5
  Jul 10, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,663
  Likes Received: 3,317
  Trophy Points: 280
  Kweli jamani arusha imekuwa chafu!!yaani hadi kinyaa,vituo vya daladala(Hiace)navyo vimefutika kabisa,hivyo kituo ni popote,sijui tatizo nini.
   
 6. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #6
  Jul 10, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Ni kweli, jiji ni chafu sana sasahivi. Nadhani ni kutokana na kutokuwa na mbunge na uchache wa madiwani wa upinzani. Hayo maeneo yote uliyopita yapo chini ya diwani wa ccm, kata ya Mjini kati! Sijui anafanya nini!?
   
 7. Ngofilo

  Ngofilo JF-Expert Member

  #7
  Jul 10, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 214
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  lAKINI LA AJABU HALMASHAURI YA JIJI BADO INAKUSANYA KODI......
   
 8. Hute

  Hute JF-Expert Member

  #8
  Jul 10, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,059
  Likes Received: 3,927
  Trophy Points: 280
  hivi hakuna uongozi hapo halmashauri? wana akili kweli kuona uchafu huo alafu wapowapo tu?
   
 9. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #9
  Jul 10, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160


  Hili ndiyo linanishangaza sana!
  Tena ni wakali kupita kiasi!

  Mi natamani hatima ya MB wetu ijulikane na hata madiwani tuwapate nione A town inarudi ktk hali inayoridhisha!
   
 10. c

  choka Senior Member

  #10
  Jul 10, 2012
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  serikali dhaifu,inafanya mambo yake kigoi goi.
   
 11. Ngofilo

  Ngofilo JF-Expert Member

  #11
  May 12, 2013
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 214
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Huyo ndiye Kikwete mzee.
   
 12. kabanga

  kabanga JF-Expert Member

  #12
  May 12, 2013
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 29,807
  Likes Received: 3,702
  Trophy Points: 280
  Hapo kikwete wanini? Wakati Uko kuna serikali ya mkoa jiji na kila kitu...
   
 13. Noni na Nsugu

  Noni na Nsugu Member

  #13
  May 12, 2013
  Joined: Mar 18, 2013
  Messages: 95
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pachafu sanaaaaa!Ingawa the story is exaggerated and biased kwa kutoonesha sehemu ambazo ni sababu za Arusha kuitwa Geneva of Africa.Kifupi jicho lako ni chongo!
   
Loading...