Ukitumia jicho la tatu kwenye machozi mazito aliyotoa aliyekuwa DC wa Hai, Lengai Ole Sabaya kwenye msiba wa kitaifa wa JPM utaelewa yule bwana pale dhamiri yake ilikuwa inaongea waziwazi si msiba tu ulikuwa unamliza ila kuna msiba mkubwa zaidi ya huo haswa juu ya hatma ya maisha yake.
Mojawapo wa manga'muzi ni alitoa ujumbe ukionyesha kwamba, 'God father " niliyemtegemea kuliko Mungu wa mbinguni hayupo na sasa maovu yangu na siri zangu zinakwenda kufichika kwa kuwa mshirika wangu hayupo tena.
Pili, utajiri niliyoukusanya kwa njia haramu sasa mwishowake umefika sitapata hela kwa njia za utapeli na uporaji,maovu,ubaya dhuluma nilizowatendea watu huwenda zikanirudi hivyo nitumie fedha haramu nilizopata nijisafishe kupitia vyombo vya habari na nikimsifu Rais maisha yataendelea kama zamani