Jiangalie mtoto wa kiume hii ni Dar

Jiangalie mtoto wa kiume hii ni Dar

maisha yanabadilika ujue...leo unamuona hivo kesho huenda akawa kimbilio..
mwanaume hata uwe player vipi lazima kuna kademu katakua ni point of weakness kwako, huenda wewe ndiye, sababu kama mtu kaenda mbele karudi bado anakufakamia sio kawaida hiyo kwani wewe ndo una kyuma peke yako?
mkaushie keshajifunza huyo
 
Kutokana na kicha cha habari, inaonekana hata ww ulipo kuna jamaa kimejuweka tu, si mwambie tu ukweli kuwa na ww umewekwa na jamaa ili ajue, na inaonyesha kabisa hilo povu, bado unakapenda kajamaa, cha msingi toka ulipowekwa nendeni mkaanze maisha mapya.
 
Umemkataa kwasababu anaishi kwao je angekuwa na goodlyf veep
 
Nilikupenda miaka zaid ya 10 iliyopita wakati huo nipo Olevel nawe upo Advance ulivyofika chuo ukaniona mtoto kwa kauli yako mwenyewe ukasema tuachane

leo baada ya muda mrefu kupita ukapata no yangu tukasalimiana na kubahatika kuonana japo haikuwa planed ilitokea tu wewe kuwepo eneo ambalo nipo

Tukapiga story nikakuonesha mpaka ninapokaa ukiwa kama mshkaji tu cause nilishasahau yalotokea, eti baada ya wiki jioni moja unanambia unanisubiri maeneo ya nyumbani kwangu kaka nimekuita? Nakwambia sipo maeneo ya nyumbani unanambia utanisubiri tu kaka nimekuomba? Nikakujibu hata nikirudi nitakuwa nimechoka mana mda huo ilikuwa inaenda sa tano usiku eti kwa confidence kabisa unanambia haina shida utalala kwangu mpka kesho yake mchana unikande...

Hivi, tumepotezana zaid ya miaka10 hujui niko vp kimahusiano kwa sasa kinachokuaminisha ni nini? pili umenikuta naishi mazingira ya kuridhisha yenye almost kila kitu muhimu ndani kaka unajua nani karahisisha hayo? Mtoto wa kiume unapata wapi nguvu ya kulala kwa msichana ambae si mpenz wako? Ukitatuliwa marinda utakuwa umeonewa?

Wakati uko chuo ulipanga nyumba hukurusu hata siku moja mimi kupajua kwako Mungu ambayo si mwanadamu uka disco na kwenda kusoma nje sasa toka urudi huna hata kazi na unaishi kwenu leo kiherehere cha kulala kwangu kinakujaje ndugu?
Kwa hiyo lengo lako ni kumponda kwamba hana kazi au unalipa kisasi cha kukutosa wakati huo ?


Ndio maana mimi sipendagi mazoea na ma ex zangu, kila mtu apambane na hali yake, hakuna kujuana kuepusha upuuzi kama huu.
 
Ndio ujue hii dar tunatumia akili..kahudumia mwingine kiboya boya kala mwingine...we toa kama unatoa..hutaki acha
 
Back
Top Bottom