Jf uwanja mzuri wa majadiliano.

Jf uwanja mzuri wa majadiliano.

Mulama

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2011
Posts
3,047
Reaction score
1,823
Nimekuwa nikitafakari sana ujio wa jf, nikakumbuka miadhala inayofanyikaga hasa Dar. Nilichokumbuka ni kwamba kwenye miadhala hiyo huwa unakuta watu wanabishana huku wakiongea bila kupeana nafasi ya kusikilizana, yaani kila mtu anashindana na mwenzake kupitisha hoja yake kwa kupaza sauti kumzidi anayebishana naye! ( hapa namaanisha miadhara yote ya ndani au nje yenye kuhusisha majadiliano ya ana kwa ana)
Nikatamani kama wangekuwa wanapata nafasi kama ya jamvini jf ambapo kila mtu anaandika hoja zake na kujibiwa baada ya kusomwa na Kutafakariwa ingekuwa vizuri sana. Kwenye jf ni rahisi kujua uwezo wa mtu kuchangia hoja Fulani na pia kuelewa uwezo wa mchangiaji katika kuelewa mada anayoichangia.
I wish hata mikutano mingi ya kikazi hasa ya kiserikali ingekuwa inafanyika kupitia jf!
Hongera waasisi wa jf.
 
Ukitulia una akili na mawazo mazuri sana nidai ice cream sawa!!!!!!!!!!!!
 
Ni uwanja mzuri kwa werevu,
Ni uwanja mzuri iwapo nia ni kujadili, kueleweshana na kukosoana pasipo ukali wa maneno,
Ni uwanja mzuri iwapo tu wachangiaji hawana uegemeo hata waeleweshwapo,
Ni uwanja mzuri sana tena sana kwa wenye nia njema ya kuchangia na kubadilishana kwa hoja, na si malumbano yasiyo na tija,
Ni uwanja mzuri kama sote tunaipenda na kuithamini JF yetu kama sehemu muhimu ktk jamii yetu ya kiTanzania kwa kuelimishana kiustaarabu.
 
Back
Top Bottom