JF special thread kwaajili ya Facts

BoManganese

JF-Expert Member
Jun 10, 2017
979
2,671
Habari zenu wana JF.

Kama kichwa cha habari kinavyo jieleza hapo juu, dhumuni la Uzi huu ni kupeana Facts au kujuzana mambo mbalimbali yanaweza kuwa ya kustaajabisha au la lakini hapo tunakuwa na lengo moja kuu la kujifunza na kuburudika pia kwa kujuzana mambo ya kushangaza. Karibuni nyote kupeana Facts, hapa tutakuwa tunapeana statement zisizo ndefu iwapo mtu atataka maelezo kwa undani zaidi taarifa zote zipo mtandaoni. Mimi naanza kama ifuatavyo.

Kuwa karibu zaidi na mbwa wako kunasababisha ubongo wako kuzalisha kemikali ziitwazo dopamine na oxytocin ambapo ni sawa kama umpendavyo mtoto

Nchini Norway mwanafunzi yeyote kutoka nje ya nchi hiyo anaruhusiwa kusoma bure kabisa katika vyuo vya umma

Tarehe ya mwisho ambayo wanadamu wote waliishi duniani ilikuwa ni 2 November 2002 baada ya hapo ni lazma kuwepo mtu huko nje ya dunia (international space station) kwahiyo mpaka sasa sio wanadamu wote wanaishi duniani kama ilivyo kuwa kabla ya hiyo tarehe

Kama dunia ikikosa oxygen kwa sekunde 5 hapo kila kitu kilichojengwa kwa zenge kitageuka vumbi

Wanasayansi kutoka japani wamegundua mashine ijulikanayo kama MRI ambayo inauwezo wa kurekodi ndoto zako unazoota unapolala na kuzitunza ukaja kuziangalia baadae

Sperm moja ina MB 32.5 ya taarifa za DNA kwahiyo inamaana bao moja la kawaida linakadiriwa kubeba data zenye ukubwa wa TB 1500 (terabytes)

Mtu anapofariki ubongo wake unakuwa na dakika 7 za kurudisha nyuma kumbukumbu zote za mtu huyo katika mfumo wa ndoto

Albatross ndiye ndege mkubwa mwenye uwezo wa kukaa angani muda mrefu bila kugusa chini hutumia miaka yao 6 ya kwanza kupaa tuu baharini bila kugusa ardhi

Sikio la kulia lipo vizuri zaidi katika kusikia maongezi na sikio la kushoto lipo vizuri zaidi katika kusikiliza Muziki

Daktari aitwaye Duncan McDougall alijaribu kuthibitisha uwepo wa roho ndani ya mwili wa binadamu ambapo alifanya hivyo kwa kupima uzito wa mtu anaye karibia kufa kisha kupima tena uzito wa mtu huyo huyo mara baada tu ya kufa, alifanya hivyo kwa watu sita tofauti tofauti ambapo majibu yalionesha kuwa wastani wa uzito uliopotea baada ya kufariki watu hao ni gram 21 kwa wote

Kama ilivyo alama za vidole kila mtu ana alama za kipekee katika ulimi

Twiga ana ulimi mweusi wenye urefu wa nchi 20

Matirio ghali zaidi duniani inaitwa Antimatter ambapo ina thamani ya dollar trillion 62.5 kwa gram, hii inatosha kuangamiza mji mzima wa New York

Nge ni mdudu mwenye uwezo wa kubana mpumzi hadi siku 6 pia ana uwezo wa kukaa mwaka mzima bila kula chochote

Eurotomia ni ile hali ya mwanamke kwa na ujasiri kujiona mzuri na kuhisi kuna mtu anampenda

Boanthropy ni tatizo la kisaikolojia ambapo mgonjwa anaamini kabisa yeye ni ng'ombe

Kuna kisiwa cha takataka katika bahari ya Pacific ambacho kinaitwa "Great Pacific garbage patch" ambacho kina ukubwa mara 3 zaidi ya nchi ya ufaransa

Tarehe 18 April 1930 BBC walitangaza kuwa hakuna habari siku hiyo hivyo waliweka tuu mziki wa piano

Najua kuna Facts nyingi sana hivyo wadau tujitahidi kushare hizi taarifa tuzidi kujifunza. Kama unapata walakini katika facts hizo fatilia zaidi mtandaoni utapata taarifa kwa kina zaidi.

Karibuni,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom