Mkuu wangu,
Hawa hasa ndio tunawalenga. Kwenye matengenezo yetu tunajaribu kuboresha zaidi namna ya kuweka attachments ili wadau wanapofanya hivyo iwe rahisi kwa wenzetu.
KWA WENGINE:
JF ni tovuti ambayo kwa Tanzania imekuwa ya mfano kwa kuwapa fursa wenye changamoto ya kuona (wengine huwaita vipofu) ili nao washiriki kwenye mijadala anuai.
Mnaombwa mnapoweka attachments mziweke kama “full attachments” na mkiweza tafadhali wekeeni na caption ili wenzetu wenye changamoto ya kuona au wenye uoni hafifu washiriki nasi.
Technologically tumejitahidi kufanya inclusion lakini wadau huenda hamkujua hili hivyo kuwapa wakati mgumu wenzetu kusoma attachments.
Picha zikiwa attached JF wenzetu bado wanaweza kujua lakini caption zinawarahisishia sana.
Sina hakika kama mdau niliyemnukuu ana changamoto hii lakini ni “wake up call” kwetu sote kuwajali na kuwarahisishia kushiriki nasi.
Asante