Definition yangu
JF ni Watu (Watanzania, Majirani na Tanzania, waliowahi kuishi Tanzania au wanaotegemea kuishi Tanzania) waishio ndani na nje ya Tanzania wenye machungu na nchi yao Tanzania juu ya hali ya maisha ilivyo mbaya kwa Watanzania iliyosababishwa na viongozi wao wala rushwa na mafisadi. Ni watu walioamua kusema ukweli, kufunua maovu ya waovu, ku shauti kwa jamii, kushawishi jamii juu ya mwenendo mzima wa watawala wetu. kwa upande mwingine ni watu walioamua kuelimishana juu ya mambo yote ya maisha aliyopitia, aliyonayo na atakayokutana nayo Mtanzania. Mambo hayo yanahusu siasa, imani, starehe, lugha, elimu, nk. Ni watu wenye mitizamo, elimu, uchumi, fikra, busara, maoni tofauti lakini wenye lengo moja kuhusu nchi yao Tanzania kwamba iwe ni nchi ya amani, iliyoendelea kiuchumi, yenye watu wastaarabu, wenye uwezo kiuchumi, wanaoheshimiana na wanaoheshimiwa kimataifa. Ni watu wasiopenda kusifiwa au kujisifu wao binafsi juu ya michango yao na hoja zao(ndio maana hawaandiki majina yao kamili) bali wanapenda kusifiwa au kujisufu kama kundi yaana Jambo forums
Kwa nini usione fahari kujiunga na JF? Wageni karibuni barazani michango yenu inahitajika muno hapa.
Hivyo basi JF tunahitaji kukaza buti tusilegeze ili kufikia malengo.