JF on the next level...

Invisible

JF Admin
Feb 26, 2006
16,285
8,363
Heshima zenu wana JF,

Tunawashukuru nyote kwa ushirikiano mnaotupa. Aidha tunaomba ushirikiano zaidi katika hatua mpya tunayokaribia kuingia...

Siku si nyingi zijazo tutafanya marebisho makubwa ambayo yataambatana na kuweka sawa baadhi ya mada na kupunguza wingi wa majukwaa ama kuongeza.

Katika hili, tunahitaji ushirikiano wenu ili tujue nini kiongezeke, nini kipungue, nini kifanyike kwa ufanisi zaidi na kivipi. Mimi na crew nzima tutafurahi zaidi endapo maoni yenu yatatumwa kwetu kwa njia ya barua pepe ama kuchangia katika mada hii. Kwa wale ambao hamjajisajili na mngependa kuchangia juu ya nini kifanyike kwa manufaa ya watanzania wote na wale wanaoitumia JF tafadhali tufahamishe kupitia webmaster@jamboforums.com nasi tutayafanyia kazi. Kila barua pepe itajibiwa!

Aidha, tunaomba yeyote mwenye kupenda kutuwezesha kwa namna moja ama nyingine awasiliane nasi ama atuchangie kwa kutumia link hii ya Support JamboForums.com (kwa kutumia Debit/Credit Card). Tunawashukuru nyote ambao mmekuwa sehemu ya familia yetu na tunaendelea kuwaomba ushirikiano zaidi tunapoelekea katika hatua nyingine yenye tija kwa wote.

Ahsanteni kwa ushirikiano na endelea kufurahia huduma zetu.

Invisible
For JF Management Crew
 
Invisible and your Crew,

We salute you! This is a most useful arena for a worldwide national conversation.

I ask that you try to make your pages more easily downloadable. There are users with access to very small bandwidth only. They cannot download web pages with heavy graphics. (I may or may not be one of those)! Minimize on the graphics (if you can).

Have some control on the text size too. Font 12 would seem to be adequate for all postings.

Let us know what you intend to do, and then we will tell you whether it is suitable or not.

Thanks,

Augustine Moshi
 
Ni ngeshauri tujipange kitaalamu zaidi, nikiwa na maana wa mfano wa kisheria zaidi, maana sisi ni wana harakati na wanaharakati mara nyingi wanakumbwa na misukosuko mingi inayopelekea kukamatwa na dola na vitu kama hivyo, then kwanini tusiwe na mfuko rasmi na wanasheria wetu wa humu humu kwa ajili hiyo, kuliko kama ilivyo sasa nikikumbana na mambo yanayohusiana na sheria tuaanza kutafutana humu?

Naomba msamaha kabla kama utaratibu utakuwa uko implimented tayari maana mi nimejiunga muda si mrefu sana

Natanguliza shukurani
 
Invisible and your Crew,

We salute you! This is a most useful arena for a worldwide national conversation.

I ask that you try to make your pages more easily downloadable. There are users with access to very small bandwidth only. They cannot download web pages with heavy graphics. (I may or may not be one of those)! Minimize on the graphics (if you can).

Have some control on the text size too. Font 12 would seem to be adequate for all postings.

Let us know what you intend to do, and then we will tell you whether it is suitable or not.

Thanks,

Augustine Moshi

Kwa kuongeza, naomba tuendelee kujitole a kwa kizidi kuitangaza JF,(kama lile wazo la T-shirt)sasa tungetengeneza na stickers, mugs, na vitu kama hivyo,maana ki ukweli wengi sana hapa nyumbani hawaijui kabisa JF.
 
Pengine pia, katika kupunguza idadi ya thread, mnaweza kufikiria kuwa na section ya "kutoka magazetini" ambapo habari na makala interesting kutoka kwenye magazeti zinaingia huko badala ya kupost habari au makala moja moja. Pengine tunaweza kuwa na breaking news section pia.
 
Definition yangu

JF ni Watu (Watanzania, Majirani na Tanzania, waliowahi kuishi Tanzania au wanaotegemea kuishi Tanzania) waishio ndani na nje ya Tanzania wenye machungu na nchi yao Tanzania juu ya hali ya maisha ilivyo mbaya kwa Watanzania iliyosababishwa na viongozi wao wala rushwa na mafisadi. Ni watu walioamua kusema ukweli, kufunua maovu ya waovu, ku shauti kwa jamii, kushawishi jamii juu ya mwenendo mzima wa watawala wetu. kwa upande mwingine ni watu walioamua kuelimishana juu ya mambo yote ya maisha aliyopitia, aliyonayo na atakayokutana nayo Mtanzania. Mambo hayo yanahusu siasa, imani, starehe, lugha, elimu, nk. Ni watu wenye mitizamo, elimu, uchumi, fikra, busara, maoni tofauti lakini wenye lengo moja kuhusu nchi yao Tanzania kwamba iwe ni nchi ya amani, iliyoendelea kiuchumi, yenye watu wastaarabu, wenye uwezo kiuchumi, wanaoheshimiana na wanaoheshimiwa kimataifa. Ni watu wasiopenda kusifiwa au kujisifu wao binafsi juu ya michango yao na hoja zao(ndio maana hawaandiki majina yao kamili) bali wanapenda kusifiwa au kujisufu kama kundi yaana Jambo forums

Kwa nini usione fahari kujiunga na JF? Wageni karibuni barazani michango yenu inahitajika muno hapa.

Hivyo basi JF tunahitaji kukaza buti tusilegeze ili kufikia malengo.
 
Mkuu, nadhani itakuwa vema iwapo utawasilisha rasimu ya mabadiliko ili tuwe na guidelines za kutoa mapendekezo. Naunga mkono wazo la la kuwa na sections za kutoka magzetini na breaking news
 
Mkuu, nadhani itakuwa vema iwapo utawasilisha rasimu ya mabadiliko ili tuwe na guidelines za kutoa mapendekezo. Naunga mkono wazo la la kuwa na sections za kutoka magzetini na breaking news
yah i 2nd the notion, it will make more sense, manake saa zingine inapunguza ile utamu wa jf wa kubreak news first, so inakuwa kama umeingia kwenye mtandao wa magazeti, all ina all nasapoti mabadiliko yote yenye nia ya kuifanya jf izidi kunoga zaidi, SALUTE!
 
Salute Invisible & Crew,

Kuhusu Forums,, yah ikiwezekana zipungue ili kuondoa msongamano wa threads katika baadhi ya msjukwaa,

But if yuo intend kuongeza forums pia sio mbaya mkiongeza forums ya Historia yetu na matukio mbalimbali yaliyowahi kutukuta watanzania,,

Kuhusu kuchangia JF, naomba muangalie utaratibu mwingine maana huu wa credit na debit card tunauogopa tunaweza kukamatwa bwana kwamba tunafadhili JF ambayo ni mwiba kwa serikali na wala rushwa wa Tanzania,

Nawatakia kila la kheri na ninaahidi kutoa mchango kadri niwezavyo endapo kutakua na njia mbadala ya credit/debit cards.

Was'laam
 
Weka sehemu ya ukabila na makabila kuruhusiwa kuzungumza mambo yao wao kwa wao na anza na kabila la kikwere ili waweze kumshauri mtawala wetu
 
..invisible,

..mvumilivu hula mbivu!...."subira huvuta heri"....kazi iendelee!

..hamna kitu kinachonikera lately humu kama hizi "spam" za mambo ya dini. nadhani it's high time kuwafunga kamba hawa,wawe na kiasi!

..otherwise,it's all good!
 
Back
Top Bottom