Jf mmewasha moto udsm | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jf mmewasha moto udsm

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by JATELO1, Oct 5, 2012.

 1. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Wana-JF,
  Hii habari hapa chini nimetumiwa na jamaa yangu ambaye ni member wa UDSM. Ebu jisomee mwenyewe, kumbe ile habari iliyoletwa hapa JF na mwenye ID VUTA-NIKUVUTE ni kweli tupu, kwani wengi wa hata Seniors mshahara umepunguzwa. Kazi kweli kweli. Nisikuchoshe na wewe usinichoshe, hunijui na mimi sikujui wewe msomaji wa habari hii. Pata habari kamili hapa chini,

  Wana UDASA
  Nimeikuta hii kwenye moja ya mitandao ya kijamiiMishahara UDSM 'utata' mtupu... "Kwanza wafanyakazi wa UDSM wameanza kupokea mishahara ya mwezi uliopita tangu jana tarehe 4/10/2012 saa sita mchana. Wameanza wafanyakazi wenye akaunti katika benki ya Makabwela yaani 'National Microfinance Bank-NMB'.

  >
  >Katika mishahara hiyo, wapo watumishi waliopata ongezeko la mishahara. Wapo pia pia wasiopata ongezeko.Hawa wamepata mshahara wao wa kawaida kabla ya ongezeko. Vilevile wapo walioshushwa mishahara. >>Hakuna sababu zilizotolewa na Serikali wala Chuo. Nyaraka za mishahara zinaonesha hivyo. Taarifa zinaonesha kuwa Utawala wa UDSM umeziba pengo la walishushwa mshahara ili kuzuia mgomo wa wafanyakazi wa aina hiyo. >>Hali ni tete. Lolote laweza kutokea pale...

  "
  >>>Nianze kwa kueleza kuwa nimesikitishwa sana kusikia mmoja wa wanachama wa Udasaametishwa kutokana na yale aliyoyatolea maoni kwenye "forum" hii hii. Ifike wakatikoleo tuliite koleo> Mimi binafsi dini ninayoamini inaniambia kuwa "Iseme kweli nahiyo kweli itakuweka huru". Yanayotokea CKD kwa sasa hasa kuhusu mishahara yawafanyakazi inaonesha kuwepo kwa ombwe la uongozi. Nimefanya utafiti kuyasema hayanitakayoyasema hapa chini.

  Yaani matatizo yaliyopo CKD ni matatizo ya miaka nendarudi ambayo yamekuwa yakiikabili Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,mpakanajiuliza kunani CKD?
  >>Nimepata kuongea na mtu wa karibu ambaye yupo ofisi ya mishahara, ameniambia,kwakuwa yeye amekuwepo hapo muda mrefu, matatizo wanayokumbana nayo wafanyakazi kwenyemishahara yao sasa hayakuwapo enzi za Prof. Mathew Luhanga (akiwa VC) na mtanguliziwake. Tena ameendelea kueleza kuwa ilifikia mahali huko nyuma mishahara ilikuwa ikiwahi kufikia tarehe 25 ya kila mwezi mishahara ya wafanyakaziinakuwa tayari imelipwa.

  >
  >Utafiti wangu umenionesha kuwa kufikia mwezi July mwishoni mwaka huu, vyuo vinginena hata vyuo vishiriki vya CKD waliweza kulipwa mshahara wao wa Julai ambao ulikuwana ongezeko la kila mwaka (annual increament) lakini CKD haikuwa hivyo, tatizo ninini? Kuna wafanyakazi wamepandishwa madaraja zaidi ya miezi minne iliyopita lakinihadi sasa wanalipwa mishahara yao ya awali bila ongezeko la madarajawaliyopandishwa, tatizo ni nini? Kwa nini mliwapandisha madaraja kama hamkuwa napesa za kuwalipa? Kwa nini mnashindwa kufikisha taarifa zao kupanda kwao madarajakwenye mamlaka husika ili mishahara yao iletwe kwa wakati?

  >
  >Usomi wetu uwapi kama tunashindwa kufanya kazi na kutatua changamotozinazotukabili? Kwa nini matatizo yale yale yajirudie kila mwaka na sababuzinazotolewa kila mwaka zinakuwa zilezile? Mishahara ya wafanyakazi inacheleweshwa halafu tangazo linawekwa likisomeka "Tunapendakuwatangazia/kuwajulisha kuwa mishahara itachelewa...." Yaani umechelewa kuwalipawafanyakazi wako halafu tena unasema "Ninapenda'? Kwa nini usiseme kuwa"Unasikitika kuwatangazia kuwa mshahara umecheleweshwa kwa....."?

  >
  >Malimbikizo ya mwaka jana ya mishahara hadi sasa hayajalipwa, tatizo ni nini? Mimibinafsi tangu niajiriwe na nafikiri wapo wengi wa aina yangu, ni zaidi ya miakamitatu sasa sijalipwa pesa ya kujikimu iliyopaswa ilipwe (subsistence allowance).Hii ni pesa niliyopaswa kulipwa bila kujali nimeajiriwa toka wapi. Pesa ambayoingekuwa nisipewe ni ya mizigo kwa kuwa mimi niliajiriwa kutokea Dar es Salaam.Tulijaza fomu miaka kama miwili imepita sasa lakini kimya.

  >
  >Tuache kufanya kazi kwa kutumia "vimemo". Tuammke na kuyafanyika kazi mahitaji yamsingi nya yakisheria ya walio chini yetu. This should be a waking call to Prof.Yunus Mgaya. Haya yote yanayotokea yako chini ya ofisi yako. Prof. Mukandala nawetunakuomba uyashughulikie masuala haya yanayokikabili chuo ambacho kwayo wewe ndiwekiongozi wake mkuu. Msipuuze hata kidogo na mkifanya hivyo mtkauwa mnafanya kwa hasara yenu wenyewe.

  Tuna tatizo kwenye utawala wa CKD. Kikubwa kabisa tuna tatizosasa hadi kwenye uongozi wa UDASA, wote kimyaaa,utafikiri hawayaoni haya? Kunafaida gani sasa ya kukatwa pesa yangu kwenda kwenye chama kama Udasa au THTUambacho hakina msaada kwangu? mambo yakiendelea hivi tutafanya ya Mheshimiwa Pinda,"Liwalo na Liwe" ili tujiondoe kwenye vyama kama hivi visivyo na tija kwa wanachamawake.

  >
  >Kubwa zaidi ni kwamba wakati wakubwa pale wakisema hakuna pesa, wao wanajilipa helanyingi za wanachokiita "Responsibility Allowance". Aaaaaagh, kweli aliyeshibahamjui mwenye njaa!!! Mazingira ya kazi kwa sasa yanatushusha nguvu (demoralize)sana sisi "juniors" na tunashindwa kupata nguvu ya kutusemea kwa kuwa "seniors"ndiyo hivyo wako kwenye mikataba na wanaogopa kutusemea kwa kuwa kwa kufanya hivyomikataba yao itakuwa hatarini!!!

  >
  >Siku zote tuiseme kweli ili kweli ituweke huru!! Tuna tatizo la kiuongozi CKD.
   
 2. Fabian the Jr

  Fabian the Jr JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 4, 2012
  Messages: 686
  Likes Received: 530
  Trophy Points: 80
  Good work mkuu, A GREAT THINKER should always give out what he believes to be right for the sake of the majority.
   
Loading...