JF Men & Women Of The Year 2012 Competition

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,695
1,696
Angalizo: Mods kwa hekima mnaombwa msiiamishe thread hii wala kuichanganya na nyingine yoyote. Itakuwa posted kwenye majukwaa yote makuu ili kila member anayependa kushiriki awe anafahamu na hivyo kufanya ushiriki mwaka huu wa 2012 uwe mkubwa zaidi.

Wanajamii; Wana JF

Mwaka 2011 tulifanya mchakato wa kumpata JF Man & Woman of The Year 2011. Shindano kama hili pia lilifanyika Mwaka 2010 na 2009.


  • Washindi wa 2009 "JF SuperLady" au "Celebrity wa JF" alikuwa WoS (Woman of Substance)
  • Washindi wa 2010 "Regia Mtema" (RIP) - Kwa JF Woman of the Year 2010
  • na Nyani Ngabu alifungana na Asprin kama "JF Man of The Year 2010"
  • Mwaka 2011 tulipanua wigo zaidi na kuongeza forums kuu ili kupata washindi:
    • The Boss: alikuwa King of MMU
    • Mchambuzi: Alikuwa Male Politician of the Year
    • Josephine: alikuwa Female Politician of the Year
    • AshaDii alikuwa Overall Woman of the Year
    • Aspirin alikuwa overall Man of the Year
    • Lizzy: alikuwa Queen of MMU

Links zote za Washindi hao ziko hapa:

https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/231032-the-boss-king-of-mmu-2011-a.html
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...zi-jf-male-politician-of-the-year-2011-a.html
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-jf-female-politician-of-the-year-2011-a.html
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/231019-ashadii-jf-woman-of-the-year-2011-a.html
https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/231022-aspirin-jf-man-of-the-year-2011-a.html
https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/231030-lizzy-jf-queen-of-mmu-2011-a.html
https://www.jamiiforums.com/celebri...na-nyani-ngabu-jf-men-of-the-year-2010-a.html
https://www.jamiiforums.com/celebrities-forum/98940-gaijin-na-regia-jf-women-of-the-year-2010-a.html


Mchakato wote mpaka mshindi kupatikana unaweza kuupitia hapa kwa mwaka 2011 na 2010:

https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/229183-jf-man-and-woman-of-the-year-2011-competition.html
https://www.jamiiforums.com/complaint...ar-2010-a.html

Mwaka huu 2013 tunataka kuuboresha mchakato huu na tunapenda kupitia mchakato huu kupata washiriki wengi na kuipa taswira JF kuwa kuna watu wanafakubalika katika hii online community.

Kupitia thread hii tutafanya mchakato wa kuwapata Washindi wa 2012.

Kwa mwaka huu tunahitaji maoni na mapendekezo juu ya:


  1. Categories za kushindaniwa na sababu za kuweka hizo categories
  2. Mchakato wa kupata washindi: Masharti na vigezo
  3. Mchakato wa upigaji wa kura
  4. Mapendekezo ya Members watakaokuwa katika Tume ya Uchaguzi i.e. Judges
  5. mapendekezo mengine yoyote ya kuboresha.

Katika mchakato wa awali 2011 tulipendekeza majina mbalimbali katika category mbalimbali kulingana na wahusika wanakubalika na mwishoni tukachagua watatu kutoka katika kila category na kisha kuwapambanisha kupitia JF POLLS. Mwaka huu napendekeza tuboreshe zaidi zawadi na tutoe zawadi yenye hadhi fulani kwa washindi ili kutoa changamoto za umakini katika mabandiko haba jamvini. Ni vema sponsors wajitokeze. Tutajulishana zawadi hizi tutakapoingia katika mchakato wa Kupiga kura.

Vigezo vifuatavyo vilizingatiwa 2011 katika kutoa mapendekezo ya watakaoshindanishwa katika hizi KURA ZA MAONI:

1. Kama ni category ya WOMAN lazima uwe umemdhania kuwa unayempendekeza ni Mwanamke na una ushahidi wa Kimazingira. katika hali ya mashaka, uhakikisho wa jinsia kutoka kwa muhusika aliyependekezwa utafanya akubalike. Uamuzi wa Tume ya Uchaguzi - JEC ya Shindano hili utakuwa ni Final. Wote mnahakikishiwa hakutakuwa na Uchakachuaji.

2. Kama ni category ya MAN lazima uwe umemdhania kuwa unayempendekeza ni Mwanaume na una ushahidi wa Kimazingira. katika hali ya mashaka, uhakikisho wa jinsia kutoka kwa muhusika aliyependekezwa utafanya akubalike.

3. Anayependekezwa lazima kuwe na ushahidi unaoonyesha kuwa ni Mwana JF aliyebobea hasa kutokana na Threads alizozianzisha na/au pia post anazobandika. Vyote lazima viwe na impact chanya kwa wasomaji wa JF.

4. Awe ni mwenye uwezo wa kusimamia hoja zake na kuzijibu kikamilifu bila jazba na kwa umahiri wa hali ya juu pale ambapo anapata challenge toka kwa wachangiaji.

5. Awe ni mwenye ushawishi wa hali ya juu katika mabandiko anyochangia walau kwa muonekano wa wachangiaji kuunga mkono hoja zake.

6. Kwa Wanaogombea Overall tittle, asibobee kwenye Jukwaa moja tu. Walau awe mchangiaji mzuri wa majukwaa yasiyopungua mawili. Kwa wale wanaopendekezwa MMU basi akubalike katika jumuiya ya MMU

7. Asiwe mtu wa shari katika majibizano kiasi cha kupelekea Mods kumpa "BAN".

8. Aonekane wazi katika mabandiko yake anaweza akahisiwa kuwa Kiongozi Mzuri.

9. Awe Mchangiaji ambaye ni active walau mara moja kwa wiki. Ikiwa zaidi ni vizuri zaidi.

10. Awe ni mtu asiyeogopa kukemea mabandiko yenye lengo la kutukana, kudhalilisha, kubagua, kuleta mfarakano na kutokuelewana baina ya wanachama wa JF.

Naomba sasa kupata maoni na mapendekezo yenu juu ya:


  1. Categories za kushindaniwa na sababu za kuweka hizo categories
  2. Mchakato wa kupata washindi: Masharti na vigezo
  3. Mchakato wa upigaji wa kura
  4. Mapendekezo ya Members watakaokuwa katika Tume ya Uchaguzi i.e. Judges
  5. mapendekezo mengine yoyote ya kuboresha.

Wasalaam
Superman-Logo.jpg

Signed Seal:

Superman

Mwenyekiti - Tume Ya Uchaguzi ya JF (JEC)

images
 
Back
Top Bottom