JF Kuanzisha Gazeti lake!

kimboka one

JF-Expert Member
Jan 23, 2010
734
85
wadau leo nimekubali Jf nizaidi ya chuo kikuu baada ya kusoma habari ilianza na kichwa UFISADI BILA MAJIBU... na michango ya wadau hakika kuna haja ya kuanzisha gazeti la Jf ili watanzania wengi wapata haya mawazo kwa urahisi.muundo wake litoe mawazo ya wadau na michango kwa zile post bora za wiki.liwe na makala zinazotokana na jf.lisifadhiliwe na wezi.wadau boresheni wazo hili na kumradhi kwa hicho kichwa cha habari nilitaka kuvuta makini yenu nipate mawazo
 
Kwanza mimi siafiki hili wazo lako moja kwa moja:

1. Humu ndani kuna michango taofauti tofauti, na kila mchangiaji anaona wazo lake ndio bora zaidi ya mengine. Itakuwaje kwenye kuselect ni wazo gani la kuandikwa gazetini, wewe huoni kama kutakuwa na manung'uniko miongoni mwa wana JF?

2. Kuna wakati baadhi ya wanaJF wanalalamika kuwa jukwaa hili lina mrengo wa dini fulani au chama fulani cha siasa(japo si kweli) tutawafanyaje watu hawa ili wasitoke nje na kulipaka matope gazeti hilo? Na kama ikitokea hivyo, unadhani lengo la gazeti hilo litatimia?

3. Hili jukwa lipo hivi kwa sababu linaendeshwa hivi. Jiulize kwanza, wewe uanwajua wamiliki wa JF? Je ni wanaJF wangapi wanajua wamiliki halisi wa jukwaa hili? Baada ya kupata majibu, utafakari kwanza kwamba ili kuchapisha gazeti unahitaji miundombinu madhubuti ikiwa ni pamoja na fedha za uendeshaji. Je, hili litakuwa ni wajibu wa nini?

4. Umejiuliza kwanza kama hiyo ID unayotumia ni jina lako sahihi? Je,mimi na wengine? Umeishapata picha ya gazeti ambalo waandishi wake wanatumia majina ya bandia! Wataaminika vipi ktk jamii? Kiukeli tunapta habari nyingi sana humu, tena nyingine ni nyet sanai, je wewe unadhani kama isingekuwa ni hizi IDs zetu tunazotumia humu, ni nani angekubali kuhatarisha kibarua chake au hata uhai wake kutuhabarisha.

5. Endapo gazeti hilo litaanzishwa, lazima kutakuwepo na ofisi zake mahali fulani. Na wafanyakazi wake wengi watafahamika. Je, umeishajiuliza ni kwa namna gani utakuwa umeirahisishia kazi intelijensia ktk kuwaanadama wahusika wa gazeti hili. Je, umesahau yaliyomkuta Kubenea?

6. Nijuavyo mimi, taaluma ya habari ina miiko na taratibu zake. Lakini pia kuna watu wanaosomea taaluma hii. Si kila mtu anaweza kuwa mwandishi wa habari inagawa kila mtu anaweza kutaoa taarifa ya jambo fulani. Hata sisi tuliomo humu(+me), hatuna taaluma hiyo. Kama huamini, jaribu kufuatilia michango na utoaji wa taarifa mbali mbali humu ndani, kisha ujiridhishe kwamba je, ndio waandishi wa namna hii unaotaka waonekane ktk hilo gazeti?

Kimsingi yapo mambo mengi tu ambayo kwanza ungeangalia kabila ya kufikiria hilo jambo. Napenda tu nisisitize kwamba jukwaa hili lipo hivi ni kwa sababu mfumo wake uko hivi! Ukibadilisha mfumo wake halitabaki kuwa hivi! Mimi nadhari tungeridhika tu na huu mfumo wake ili tuendelee kupata habari.

Kua upande mwingine, endapo wana JF wawili watatu wataamua kuanzisha gazeti lao ni sawa. Hakuna tatizo, tunawaunga mkono. Ila hilo gazeti litakuwa ni lao, na litaendeshwa na wao kwa kufuata utaratibu watakaokuwa wamejiwekea. Lakini pia, kwani ni mara ngapi tumeshuhudia vyombo mbalimbali vya habari vikitumia jukwaa hili kama vyanzo vyao vya habari? Mimi naona kama kuna waadishi jasiri waendelee kutumia jukwaa hili kupata taarifa na kuziweka kwenye magazeti yao, bado huo utakuwa ni mchango mkubwa wa JF kwenye jamii.

Tafakari.
 
Back
Top Bottom