Mkuu,Hakika nimekuwa mlevi mkubwa wa JF mpaka najisahau na kutoa kamchina kangu popote bila kuangalia mazingira, jana jioni nikiwa naelekea mjini nikitokea Temeke kufika Mivinjeni nikakuta foleni kubwa, foleni iliyotokana na ukarabati unaoendelea wa barabara ya Kilwa.
Baada ya kukaa kwa muda, nikaitoa simu yangu aina ya Techno 611 ambayo haina hata wiki mbili tangu niinunue, na ndiyo simu ghali kwangu tangu nianze kumiliki. Nikiwa nimezama ktk JF, ghafla akatokea kibaka na kuikwapua ile simu, nami sikujivunga! nilifungua mlango na kumkimbiza huku nikipiga kelele za mwiziii! mwiziii! mwiziii! nilimkimbiza peke yangu bila kupata kampani yoyote.
Na muda huo huo gari zikawa zimeruhusiwa nikajikuta nimeweka foleni nyingine huku milio ya honi ikiwa imepamba moto.
Kule alipokimbilia kumbe kulikuwa na vibaka wenzake! wakaanza kunirushia mawe na kujikuta nashindwa la kufanya na kumuacha yule mwanakharamu akitokomea na mchina wangu.
Nilirudi kwenye gari huku nikiwa nimechanganyikiwa vibaya, hali hiyo ilinifanya nipoteze umakini barabarani. Nilipaki gari pembeni, hata safari yenyewe ilinitumbukia nyongo!.
Hivyo natoa tahadhari kwa wengine, maeneo yale ya Mivinjeni zilipovunjwa nyumba ni hatari sana!
Hakika nimekuwa mlevi mkubwa wa JF mpaka najisahau na kutoa kamchina kangu popote bila kuangalia mazingira, jana jioni nikiwa naelekea mjini nikitokea Temeke kufika Mivinjeni nikakuta foleni kubwa, foleni iliyotokana na ukarabati unaoendelea wa barabara ya Kilwa.
Baada ya kukaa kwa muda, nikaitoa simu yangu aina ya Techno 611 ambayo haina hata wiki mbili tangu niinunue, na ndiyo simu ghali kwangu tangu nianze kumiliki. Nikiwa nimezama ktk JF, ghafla akatokea kibaka na kuikwapua ile simu, nami sikujivunga! nilifungua mlango na kumkimbiza huku nikipiga kelele za mwiziii! mwiziii! mwiziii! nilimkimbiza peke yangu bila kupata kampani yoyote.
Na muda huo huo gari zikawa zimeruhusiwa nikajikuta nimeweka foleni nyingine huku milio ya honi ikiwa imepamba moto.
Kule alipokimbilia kumbe kulikuwa na vibaka wenzake! wakaanza kunirushia mawe na kujikuta nashindwa la kufanya na kumuacha yule mwanakharamu akitokomea na mchina wangu.
Nilirudi kwenye gari huku nikiwa nimechanganyikiwa vibaya, hali hiyo ilinifanya nipoteze umakini barabarani. Nilipaki gari pembeni, hata safari yenyewe ilinitumbukia nyongo!.
Hivyo natoa tahadhari kwa wengine, maeneo yale ya Mivinjeni zilipovunjwa nyumba ni hatari sana!
Pole sana mkuu huo uizi ni maarufu sana hapa Dar na wengi wamelizwa sana...bahati mbaya watu wengi huwa wagumu kujifunza...
Ruhazwe JR lile bandiko lako la onyo limepata muhanga wa kwanza...
Ahsante...Maneno ya busara kabisa haya!
mkuuu pitia hapa tu-share maumivu woteMkuu bahati mbaya sikubahatika kuliona hilo bandiko!