Jf ilinikutanisha na tapeli wa mapenzi

Mhhh pole mwaya na asante kututahadhalisha.:A S-coffee:
 
Ninashukuru kwa mawazo yenu, nilichelewa kuja kuwajibu kwani kama mnavyojua hii ni holiday season, my sweetheart amenipeleka vacation. mahusiano yetu bado yako kwenye early stage kwa hiyo muda mwingi hasa kwa likizo hii tunautumia kuwa klaribu na kujuana zaidi. Bila shaka tutakapomaliza holiday yetu nitarudi ili kuweza kuwasalimia tena, kama haamtajali naweza kuwawekea baadhi ya picha zetu za holiday....zile zingine naweza kuziweka jukwaa la wakubwa pia.

Hii comment yako uliyopost pindi ulipo mpata inaonyesha ni kama tayari amri ya sita ilisha vunjwa, vacation kujuana vizuri kisha picha zingine jukwaa la kikikubwa?
 
Matapeli, wawe wa mapenzi au aina yoyote, wapo kila pahali. kama alivyosema mmoja, hata makanisani, masinagodi na misikitini. Hawa watu wamesomea, wakifahamu tu udhaifu wako wanakupa darasaa.

Na pengine ni ukiwa na tahadhari ni rahisi zaidi kumkamata tapeli wa mitandaoni, hasa kwa vile ila za mitandaoni zinajulikana, kuliko yule unayemwona kila siku kumbe ni chui kavaa ngozi ya kondoo.

Tumeshajadili hapa mara nyingi faida na hasara za mitandao, na wengi tunakubaliana kuwa "ikitumiwa vizuri inakuwa na faida nyingi kuliko hasara". Kitu muhimu ni kuwa macho.

Pole sana Nakadori kwa yaliyokukuta na pia Hongera sana kwa kuponea chupuchupu.
 
Wakuu, heshima mbele,

Najuta sana kumtafuta partner humu JF yani pamejaa usanii hapa usipokuwa mjanja kama mimi unalizwa hivi hivi unajiona.


Kipindi kile nilikuja na swala la kutafuta mchumba hapa, kweli huyo aliyejidai mchumba alipatikana bada ya kuchuja chuja na kufanya trial and error. kumbe mchumba hakuwa mchumba bali tapeli wa mapenzi tu. mkasa ulikuwa hivi....... jamaa alisema yuko single na mara ya mwisho kuwa na msichana ni mwaka mmoja uliopita.baada ya kuchat sana kupitia mtandao huu wa JF na email ilibidi tupeane mawasiliano ya simu, na majina ya facebook account. Ukweli mawasiliano yalikuwa hot sana. Simu zilikuwa hazikauki, meseji ndo dahhh siwezi sema, kutwa kuchwa ni kuchat na kupena meseji za mahaba. Ila kwenye facebook friend list yake ilikuwa imefungwa huwezi ona nani ni rafiki yake na huwezi post kwenye wall yake pia.

Basi, sisi tukiwa kwenye mapenzi motomoto na kuliwazana (ila sikuwa mwepesi kutoa tundi ndio ninachoshukuru na kujivunia) kumbe jamaa ana girlfriend wake wa long mie sikujua, basi siku moja niliona friend request ya mdada mmoja hata simjui ameni-add mie bila hiyana kabla ya kumu-accept nikawa natumiana nae inbox kujua ni nani na ni wawapi.....bi dada akaniambia nimuadd kwa faida yangu, ila akawa anadadisi sana kuhusu mahusiano yangu ya kimapenzi, sikuwa muwazi sana hadi aliponitajia jina la facebook la huyu kiumbe tulokutana JF. Huyu binti alisema yeye na huyu fisadi wa mapenzi ni wachumba wa long time ila yeye anafanya kazi mkoani huwa anakuja dsm mara chache sana. Nilimuuliza kuhusu uthibitisho ili niamini maneno yake then alinitumia hadi ushahidi wa pics ambazo sio za kawaida yani za mitego mitego ya kimapenzi zinazoonesha wako na mahusiano live (picha zilionesha hata dates za muda wa karibuni), kuforwad emails za huyu kiumbe wanazotumiana kila leo za kimapenzi n.k.

Ukweli baada ya hayo yote hasira zilinipanda ila nikazituliza nikapata ujasiri wa kumuomba kijana anipishe tugawane ustaarabu. kijana alisita huku akisistiza nimwambie why, mie nikamwambia nimeona siwezi match nae, yeye akawa anasisitiza bado ni mapema mie ku conclude hivyo. Nilipoona anasisitiza nikamwambia live kwamba ana msichana mwingine hivyo ni bora nimpe nafasi ili apumue vizuri! Kijana alibisha hadi leo hii.., pamoja na kumforwadia emails zake lakini wapi bado anakataa.

Hili tukio nimeona nililete ili kuwaasa wasichana wenzangu na hata kaka zangu ambao nao wako kwenye process ya kuisaka ndoa wawe makini sana. mimi kwa hili naweza sema ni Mungu ameniokoa kwani nilikuwa ninaelekea mbali na kuzamia kabisa! huwa nimefikiria ilikuwaje huyu dada akanijua kupitia facebook? au alipewa password na hyu kaka? hapana Mungu aliamua kunionesha na kuniokoa.

Wanawake wenzangu na kaka zangu tumuombe sana Mungu ili atupatie wanaume na wanawake wa ukweli na sio matapeli.

Mbarkiwe sana.
Pole sana, sio wewe tu, kuna dada mwingine alikutana na kisa kinafanana na cha kwako humu humu, dada wa watu akafa akaoza yaliyomkuta ni kutumiwa sms kila siku na mwanamke wa gume gume akimsihi amuachie gumegume lake, mpk ikambidi dada wa watu abadili namba ya simu. Dawa yao ni kuwaweka tu hadharani. Gumegume linaitwa Chip...zi, walaaniwe kabisa watu wa namna hii kwa kucheza na hisia za watu. Poleni sana
 
Nawewe punguza ukurupukaji, kwani unapomsoma mtu ni lazima uwe mbali nae?kwanza utamjuaje vizuri kama huko karibu nae? kwa mimi naweza msoma mtu kama nikiwa karibu nae na sikuwa mbali nae. lingine mapenzi motomoto na kuliwazana aliyosema mtoa hoja ni kuwa karibu kwa hizo meseji, calls na mawasiliano mengine. sasa kuna ubaya kuchat na mtu kwa ukaribu na maneno ya kimahaba? sioni tatizo hapo wewe umekurupuka kama kawaida yako.

Hebu pitia hiyo mistari yako,halafu utajua tofauti ya mpangilio na kukurupuka.Halafu kawaida yangu,duh! umenifananisha
 
wapo watu humu wamekutana na wamefunga ndoa
wapo ambao wamepata wapenzi na wapo pamoja
wapo ambao wametapeliwa na wanalia....
just be careful......

uwongo ni mwingi humu kuliko ukweli but msiwe pessimistic.............
still watu wa kweli wapo humu.....ingawa ni wachache
 
kumbe watu wanaposema wanatafuta wapenzi/wachumba humu huwa wako serious? yaani kwa kweli sikuwa naamini kwamba watu wapo serious, nilidhani wanatania tu.
Pole sana my dear.
 
wapo watu humu wamekutana na wamefunga ndoa
wapo ambao wamepata wapenzi na wapo pamoja
wapo ambao wametapeliwa na wanalia....
just be careful......

uwongo ni mwingi humu kuliko ukweli but msiwe pessimistic.............
still watu wa kweli wapo humu.....ingawa ni wachache

Ni kweli ..lakn kama ilivyo sehemu nyingine yoyote hata kanisani ..inahitaji neema ya Mungu kujua mkweli...
 
Hii comment yako uliyopost pindi ulipo mpata inaonyesha ni kama tayari amri ya sita ilisha vunjwa, vacation kujuana vizuri kisha picha zingine jukwaa la kikikubwa?
watu hamdanganyiki???????????? lakini ndo zetu wadada, mambo yakiharibika huwa tunasema hatukufika mbali, ha haaaaaaa.
 
Ni kweli ..lakn kama ilivyo sehemu nyingine yoyote hata kanisani ..inahitaji neema ya Mungu kujua mkweli...
Ni kweli, lakini unapotoa tangazo kwa kila mtu kuwa unatafuta mpenzi unategemea nini? matapeli watakuja wengi kuliko genuine..... ni mtazamo wangu tu
 
wapo watu humu wamekutana na wamefunga ndoa
wapo ambao wamepata wapenzi na wapo pamoja
wapo ambao wametapeliwa na wanalia....
just be careful......

uwongo ni mwingi humu kuliko ukweli but msiwe pessimistic.............
still watu wa kweli wapo humu.....ingawa ni wachache
rafiki, hivi kuna kuwa careful wakati upo desperate?
 
wapo watu humu wamekutana na wamefunga ndoa
wapo ambao wamepata wapenzi na wapo pamoja
wapo ambao wametapeliwa na wanalia....
just be careful......

uwongo ni mwingi humu kuliko ukweli but msiwe pessimistic.............
still watu wa kweli wapo humu.....ingawa ni wachache


ni kweli TB ila wengi wa akina dada wanaamini ahadi ya mafanikio kuliko uhalisia wa mahitaji halisi .. kani wao ndoa ndo muongozo wao kuliko kutengeneza mazingira ya ufaham,u
 
Baadhi ya wakaka huku wako so fake kushinda unavyoweza kuamini...ushauri wangu kuweni waangalifu.
 
Ni kweli, lakini unapotoa tangazo kwa kila mtu kuwa unatafuta mpenzi unategemea nini? matapeli watakuja wengi kuliko genuine..... ni mtazamo wangu tu

Inawezekana ni kweli..Ninachojua mm kama unaongozwa na Roho wa Mungu lazima atakuonyesha njia.Haijalishi ni ipi ilmradi isiwe kinyume na maandiko matakatifu..Bible.
All in all kuwa desperate ndio tatizo kubwa kwani linawafanya watu wawe vipofu na wazito kufikiri.
 
kati ya makosa ambayo uliyafanya ni kutokutana na huyo kijana uso kwa uso na mkaongea kwani waweza mlaumu kumbe kuna mtu labda kampiga chini na anamkomoa hata kama umeamua kuachana ni vzr mngekutana na kueleza kwanini hasa na usikilize upande wa pili. kwa technolojia ya sasa picha sio sehemu ya kuamini sana na ukumbuke kuwa huwezi kuta mwanaume bikiri. mfano naweza kuwa nimepiga picha naye mialka miwili nyume then nikabadili tarehe ya picha.

hata hivyo
 
Back
Top Bottom