JF Expected Downtime: October 23, 2019

Status
Not open for further replies.
Ahsante kwa taarifa. Jambo lingine kwa sisi tunaotumia website unapo taka kumtaja mtu kwa kuanza na alama '@' zinakuja suggestions za kutosha(jambo jema)

ila unapo taka ku scroll down ili upate jina unalilitaka ile list ina vanish je kunaweza kuwa na namna nyingine ya kuboresha hilo? Kama sijaeleweka sina nmna nyingine ya kueleza.

Vinginevyo nawapongeza kwa kazi nzuri.
Waiweke hii kitu kwa app pia pawe na urahisi katika ku-mention/ku-tag
 
Jaman kwa wale wana computer wenzangu leo uo mda majamaaa watafanya
"Git push -u orgini master"
 
Wakuu,

Tunatarajia kati ya saa 7 kamili usiku hadi saa 8 usiku wa leo (1:00am - 2:00am) kwa muda wa Afrika Mashariki kutakuwa na downtime (kutopatikana) kwa Mtandao wa JamiiForums ambayo imepangwa kwa ajili ya kuimarisha zaidi miundombinu yetu na kuboresha mambo kadhaa katika miundombinu.

Mabadiliko hayataonekana kwa macho bali experience ya JF upande wa ufungukaji (kasi) ndo itaongezeka.

Tusingeweza kufanya mabadiliko haya makubwa bila kwenda offline kutokana na sababu zisizoepukika. Mabadiliko mengine ya kimwonekano na upande wa app yatafanyika bila ya kwenda offline kabisa.

Tunawashukuru sana kwa uelewa wenu
Mungu ibariki JF
 
Oki dokie

Ila hili la Notifications kwenye app ni tatizo sugu sasa kama la kuchota maji kuwawekea viboko kwenye bwawa
Sijui nimeandika nini
 
Invisible

Kuna mada nyingi sisi hatutaki ziona japo wengine wanataka ziona kwanini usituwezeshe tuweze kuzuia kuona hizo mada.
Mfano mtu kaweka mada kuhusu ushoga na mimi sitaki ionekane kwangu
Au
Mtu anaandika utoto na mimi sitaki kuuona baada ya kusoma mara ya kwanza
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom