JF Exclusive: The Buzwagi Contract

invisible u dont have to wory, ndio ukubwa wa JF huo, Let them know kuwa kuna serious pple discussing serious issue.
 
shamba la bibi siku zote watu hupita na kujichumia watakavyo.... nadhani ili watanzania wengi wapate kujua ukweli wa jinsi nchi yao inavyoliwa na wao kubaki kuwa mafukara wa kunuka ni vyema ukatafsiriwa ktk lugha mama na kusambazwa kwa watanzania wengi iwezekanavyo. hakuna haja ya kuwa na serikali ya hiki chama cha sisi mmmh ambacho kina-walafi wasiokuwa na chembe ya huruma na nchi yao maskini yenye utajiri mkubwa ... wananchi tuamke tutambue kuwa ccm si baba wala mama yetu kuwa waendelee kuboronga na sisi tusiwe na jinsi zaidi ya kuendelea kuwa nao....
 
Mheshimiwa Invisible,

Msome kwa makini CMB. Hakuna wa kukugusa, tena wewe umeficha ficha, angalia sasa CMB kaweka wazi bwaaaa... na hawa THISDAY na KULIKONI waliweka hadharani, na wapinzani waliugawa kama njugu,, nchi imebadilika na wananchi sasa WANA KIU KUBWA YA MABADILIKO, TUSIRUDI NYUMA.. JK alipata URAIS KUTOKANA NA KIU YA MABADILIKO, KARUME ALIPATA URAIS ZNZ KWA SABABU NDANI YA CCM WALITAKA MABADILIKO. MABADILIKO SI LAZIMA YAWE YA UPINZANI TU, HATA YA KIFIKRA, KIUTENDAJI NA HATA HAO MA SISI EMU WANAWEZA KUAMUA KUBADILIKA. CHA MSINGI TUANGALIE MASLAHI YA TAIFA, USALAMA WA TAIFA NA SI MASLAHI YA WACHACHE NA USALAMA WA WACHACHE
 
Mheshimiwa Invisible,

Msome kwa makini CMB. Hakuna wa kukugusa, tena wewe umeficha ficha, angalia sasa CMB kaweka wazi bwaaaa...

Haha nah, I fear nothing buddy. Nalishtuka kuwa kumbe kuna walioweza kuudadafua na kuujua muziki ule. Was such a nice song buddy.

Mengi yamenikuta lakini si tatizo... Dhamira ni njema kabisa na ukweli ukijulikana daima unamuweka mtu huru. Tatizo ukweli mwingine ukiujua unabakia kujilaumu kwanini umejua maana...!
 
...... What?!?

🙁

Dont worry Invisible.. this is a good turn, a free advertizement for our beloved JF

am sure wengi wataingia JF kupitia kusoma article hiyo, lakini furaha yangu zaidi ni kwamba kila atakaye ingia humu hato toka bure, lazima atatoka ameongoka kumkoma nyani mchana kweupe!!! Moto kwa kwenda mbele hakuna kurudi nyuma.

Kitaeleweka tu!.
 
JF KIDEDEA.....eeeh!x 50,000
You made my day!Yaani ....
 
JF KIDEDEA.....eeeh!x 50,000
You made my day!

Mama Lao, the game continues. Kuna mambo mengi yamesitirika. ThisDay ndio kidedea kwa kufikisha ujumbe kwa wananchi huko nyumbani ambao sina hakika kama wana access ya internet kila mahala. We love our country Tanzania, penye kustahili pongezi tutapongeza (mfano juhudi za kuitangaza nje Tz) lakini penye mapungufu we're sorry... We dare to talk Openly! Tutayaanika tu.
 
Hivi tunaweza kuupitia kipengele kwa kipengele kwa wale waliobahatika kuupitia vema? Au mkubwa sana kiasi inahitaji mwezi kuupitia wote?

Natumaini tunaweza kuchambua kipengele kwa kipengele na kuona faida zake kwa taifa letu na kama kuna hasara tuziainishe kwenye topic hii na hata ikibidi tutoe mapendekezo yetu. Lawama tu nadhani hazitotosheleza bila kutoa hitimisho juu ya nini kifanyike na nani afanye hivyo na kivipi.

Ni mawazo tu
 
Kila mtu aliambiwa ajiweke kopi yake sasa wewe naona ulichemsha. Teh e teh eteh.................Bye.
 
Wakuu,

Unajua gazeti la maana kama Thisday kuiongelea Jamboforums kwa kiasi hiki na mafanikio makubwa sana kwa jamboforums. Hongera wote mlioifikisha hii forum hapa ilipo sasa.

Buzwagi contract finds its way onto Internet

-Chat room members refer to it as the 'Tanzanian song'

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

 
Wakuu,

Unajua gazeti la maana kama Thisday kuiongelea Jamboforums kwa kiasi hiki na mafanikio makubwa sana kwa jamboforums. Hongera wote mlioifikisha hii forum hapa ilipo sasa.

Tukianza na wewe mkuu... Thanks kwa kutuletea ujumbe huu lakini Post number 8 katika topic hii iliyowakilishwa na Halisi imeligusia hili.

ThisDay: Hawa ni wapambanaji na wameibua mengi. Wametikiswa sana lakini crew yao iko imara haitikisiki. Ni sawa na MwanaHalisi ambao nao wako imara pamoja na mikwara mingi inayowakumba. Nawapongeza wahariri wa magazeti haya na mengine ambayo sijayataja ambao hukumbana na dhahma mara kwa mara lakini wamesimama imara.

Bado nasubiri kuona maoni ya wadau kuhusiana na mkataba wenyewe; sijui ndio watu wameleweshwa kiwango cha kushindwa kuchangia tena? Au ndio kusema lugha imetumika mpya? Au lugha za ki-mikataba hazieleweki? Au tutafute wataalam toka Norway wakatafsiri iweze kuongeleka?

Tupo pamoja!
 
hata mawaziri wanasoma nondo za hapa jamboforums,wakti umefika sasa kwa watanzaniakuamka kutoka katika usingizi ulioleweshw an mwenge wa uhuru unaokimbizwa kila mwaka,

tafakari na chukua maamuzi sahihi,tuanziena uchaguzi wa madiwani unaokuja
 
hahaha .....magazeti ya bongo bwana :d

but i guess ilikuwa ni njia ya kuitangazia jambo forums tu. big up muandishi wetu. sasa watu watajua wakitaka habari moto moto wapi pakuzipata
 
Thisday Na Jamboforums

Wakuu,

Unajua gazeti la maana kama Thisday kuiongelea Jamboforums kwa kiasi hiki na mafanikio makubwa sana kwa jamboforums. Hongera wote mlioifikisha hii forum hapa ilipo sasa.
Ndio maana huko nyuma niliomba tubadilike hapa forum na sasa tuanze kumkomanyani mchana kweupe, maana huko kwingine kote wananchi tayari wameshaamka, tuache uoga maana kama wewe hapa forum unaogopa fikiria hao wa gazeti la Thisday?

Moto umewashwa sasa mwendo uendelee kuwa mdundo, majungu hatutaki hapa tunataka facts, angalia magazeti yote ya bongo leo uone jinsi hata waandishi wa habari walivyochoka yaani sasa spade inaitwa spade, leo vichwa vya habari vinaitwanga serikali na BOT, na waziri Kapuya na mgodi wake,

Saaafi sana, wacha mawaziri waende mikoani sisi huku tunaendelea kuwatwanga tu, mpaka kieleweke, maana badala ya kwenda kujisafisha mahakamani wao wanaenda mikoani what a Banana Republic!
 
mie nadhani iwekwe tracker kujua ni watu wangapi wanatembelea hapa,
 
Wajanja wameshaunyofoa. Nimeshindwa ku-download.
 
Tukianza na wewe mkuu... Thanks kwa kutuletea ujumbe huu lakini Post number 8 katika topic hii iliyowakilishwa na Halisi imeligusia hili.

Samahani mkuu! Hilo nimekuja liona baadaye kwamba kuna mtu alish post hiyo habari. Nili search kwanza sikuiona mahali.

Mengine yote OYEEEEEE!!!! kwa JF.

Jasusi nitumie email binafsi na nitakutumia copy.
 
Wajanja wameshaunyofoa. Nimeshindwa ku-download.

Jasusi bana,,, wewe si Jasusi tena! Yani ulishindwa ile jana? Nilikutumia maelekezo sana lakini naona ilikuwa aidha ni firewall yako kali ama vinginevyo.

Sasa wasiliana na Mtanzania maana mimi sina ati...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…