MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,564
- 850
Aligusia katika kila nyanja! Je katika soka na hati miliki za wanamuziki alisema nini?
Alizungumizia haki za wafanyakazi, ufisadi, vyama vya siasa, wagombea binafsi nk. Yani hii ni moja ya hotuba zake zilizo gusa karibia kila nyanja.
kwa hapo aliwapa muhimu mdogo sana pamoja na kujitoa kwao kwagealigusia katika kila nyanja! Je katika soka na hati miliki za wanamuziki alisema nini?
MwanaFalsafa1, shukrani nyingi kwa ku-upload hizi hotuba za baba yetu wa taifa hayati mwl JK Nyerere. Nimetumia siku nzima kuzisikiliza kwa makini sana na kurudia rudia mara nyingi. Huyu mtu alikuwa kiongozi mzuri tuliyekuwa tumepewa, na maneno yake yanagusa hisia, akili na moyo. Maneno yake yamesheheni hekima na utambuzi uliopeuka. Kama tungeweza kumsikiliza na kumwelewa kisha tukatenda kama alivyotuusia, ni hakika tusingekuwa hapa tulipo sasa. Nitakapo kaa sawa nitazitafuta hotuba zake zote (DVDs) nizinunue ili niendelee kujifunza kutoka kwa mwalimu huyu wa Tanzania. Ijapokuwa amekufa bado angali akinena.
Ni kweli mkuu. Tatizo wakati huo watu walikua wanaona asha pitwa na wakati na mawazo yake yame pitwa na wakati wakampuuzia. Uliona alivyo mgeukia Mramba na kumfokea "Basil, kwa nini hamkuanyi kodi?" Yani this speech was visionary.
Nyerere Baba yetu,tunakukumbuka kwa mawazo yako, the guy has ability to see future, has subconcious mindset.Anyway,kizuri hakikai, kibaya tunacho mpaka leo
Anatetea haki za Raia na kukosoa mfumo uliopo, kama vile unaokataza haki za mgombea binafsi katika mfumo wa demokrasia za vyama vingi, haki ambazo hata yeye alipokuwa na mamlaka ya nchi hakuzitoa.
Alikuwa mwanasiasa mnafiki sana.
Kama anakubali yeye alivurunda basi anapoteza haki ya kuwa mkufunzi, lecturer, mkosoaji wa mambo ambayo yeye yalimshinda, anafundisha ambayo hakuweza kuya practice. Siasa hizo ni unafik.
Ukisikiliza hotuba amekubali kosa la kuminya vyama vya upinzani. Amekiri yote hayo. Sasa kwa vile Nyerere alikosea basi na wao wengine kuendeleza hayo makosa ni sahihi?