Jeshi sasa laanza biashara ya ulinzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jeshi sasa laanza biashara ya ulinzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kite Munganga, Dec 26, 2008.

 1. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #1
  Dec 26, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Katika kupitia gazeti la Nipashe nimekumbana na habari yenye kichwa cha habari kinachosema-Jeshi sasa laanza biashara ya ulinzi, na baada ya hapo ilinikumbusha miaka ya 1979/80 hivi wakati Dar ilikuwa inalindwa na JKT pamoja na Polisi hata hivyo ilikuja gundulika kuwa hao hao walikuwa ama wanashirikiana na majambazi au wanaazimisha bunduki zao kwa majambazi, mwisho wake serikali ilisitisha mradi huo, sasa najaribu kuwaza kuwa vijana hawa watakuwa trained kijeshi na wataiva kisawasawa (kumbuka ghasia zote za JKT) na baada ya hapo umpe ajira akalinde mamilioni au mabillioni ya matajiri wetu, sasa swali kubwa ninalojiuliza ni kwa mshahara upi mali hiyo itakuwa salama? kwani hata kama watapewa mshahara unaolingana na JWTZ bado watakosa marupurupu wanayopata wakiwa kambini ambayo hulainisha ugumu wa maisha uraiani, je serikali haioni kuwa inatayarisha hatari kwa watu wake na yenyewe pia? Mfano kijana huyu umpeleke North Mara Barrick akalinde dhahabu ya wale jamaa na huku unamlipa KCC unategemea nini hapo kwa mtu aliyepitia JKT?

   
 2. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2008
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ni hatari kwa jeshi kujiingiza kwenye biashara
   
 3. M

  Manyiri Member

  #3
  Dec 26, 2008
  Joined: Oct 27, 2007
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  hakuna hatari yoyote kwa jeshi kujiingiza kwenye biashara kinachotakiwa ni kuboresha masirahi yao. mbona escortza mamilioni yafedha inafanywa na polisi wenye mshahara wa kcc?
   
 4. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #4
  Dec 26, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Escort ya fedha ya Polisi ni tofauti kabisa na ulinzi wa 100% wanaotaka kuufanya hawa na ukumbuke kuwa watakuwa kwenye lindo la vitu vyenye thamani akiwa mmoja au na mwenzie tu, hata hivyo hujasikia kuwa Polisi wengi tu wamefukuzwa kwa kushirikiana na Majambazi?
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Dec 26, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Meremeta nyingine?
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Dec 26, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,520
  Likes Received: 81,905
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe kabisa katika hili. Ulinzi wa Watanzania lazima ufanywe na polisi walioajiriwa na serikali siyo vikampuni uchwara vitavyoibuka na kuajiri majambazi ambao watajifanya ni walinzi lakini wakati huo huo wakichora mchoro wa jinsi ya kuvamia na kujipatia mamilioni kama siyo mabilioni ya pesa. Serikali itoe kauli haraka ya kupinga tamko hili la jeshi la polisi.
   
 7. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #7
  Dec 26, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu mimi naomba mnisaidie manake ni kizazi kisichopitia JKT.
  Hoja ya hao wakuu kuwa migomo ya sasa vyuo vikuu ni kwa sababu wanafunzi hawakupitia JKT ambako wangefundishwa nidhamu ya kijeshi hivyo wasingegoma ina ukweli wowote?Je huko nyuma pamoja na kuwapo mafunzo ya JKT hakukuwa na migomo vyuo vikuu?Manake kama sikosei nilishawahi kusikia migomo mlimani katika kipindi cha nyerere na kuna rumour nilisikia kuwa Prof Mwandosya kipindi hicho akiwa kiongozi(wa msosi?)mlimani aliwahi kuramba bakora za Rais Nyerere kwa sababu ya kuchochea mgomo
   
 8. J

  JokaKuu Platinum Member

  #8
  Dec 26, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,958
  Trophy Points: 280
  Mtarajiwa,

  ..Dr.Mark Mwandosya amesoma Birmingham University first degree na PhD. hana masters degree.

  ..inawezekana vipi asome UK, lakini aongoze migomo UDSM, na zaidi achapwe viboko na Chancellor wa UDSM[Mwalimu Nyerere]??

  ..Afande aliyedai mafunzo ya JKT yataondoa migomo ya wanafunzi hajui analoongea. migomo ilikuwepo tangu miaka ambayo vijana walikuwa wakipitia JKT kabla ya kujiunga na vyuo vikuu.
   
 9. Nzokanhyilu

  Nzokanhyilu JF-Expert Member

  #9
  Dec 26, 2008
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,087
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  mambo ya private military yananukia sasa eh? haya!
   
 10. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #10
  Dec 26, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Ni marehemu Mwabulambo, ndiye mtumzima aliyekula mbakora Iklulu.
   
 11. C

  Chuma JF-Expert Member

  #11
  Dec 27, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Majambazi karibu wengi ni wanajeshi...Let us wait n see the future of TZ...,

  Ni vema wakuu wangeseparate Jeshi na Biashara ya Ulinzi...Kama serikali inataka walinzi wa makampuni wapate basic training za jeshi au la.na SI wanajeshi wakafanye kazi za kulinda Maduka...Yanayotarajiwa kutokea hapa in the near future huenda yakawa sawa na yale ya IRAQ na private security companies!!!

  Primary roles za jeshi ni tofauti na hii....nafikiri kila kitengo cha jeshi kina roles zake...next polisi nao watakuwa na private security company... i agree na suala la Ujenzi wa nchi ktk secta zingine..na si Ulinzi...
   
 12. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #12
  Dec 27, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Badala ya kuanzisha kampuni ya ulinzi binafsi, afadhali hiyo JKT ikaungana na polisi kulinda public institutions
   
 13. T

  Tom JF-Expert Member

  #13
  Dec 27, 2008
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  JKT ni vizuri kufanya biashara kubwa zaidi kama kujiingiza ama kuwekeza ktk viwanda vya silaha, electronics, nguo, marumaru, masanduku na babegi, nk, pia miradi mbali mbali ya ujenzi na uzalishaji zaidi ya wafanyayo sasa kwa kutumia askari wake. Miradi hii itawapa mapato zaidi na kufanya jeshi lijitegemee na kuogeza mapatao ama na bonusi kwa askari wake na kua imara zaidi, lakini lazima kuwepo na sheria za kijeshi kulinda na kuendeleza miradi hiyo ama la sivyo itakufa. Sheria za kijeshi zitasidia sana kuendeleza miradi na kudhibiti ufisadi. Serikali KUU inaweza toa mkopo kwa JKT lakini wakiboronga lazima kuwe na kuwajibika.
  Kazi ya ulinzi haitaleta mapato maridhawa kwa Jeshi. Kuajiriwa kulinda mali ya raia, pia kutaongeza mgongano wa moja kwa moja na raia. JKT itaimairika zaidi kwa kuzalisha bidhaa zaidi ambapo wataziuza kwa raia na majeshi mengine ama kuuza nje (kuuza nje lazima serikali isimamie).
  Kazi yao ya ULINZI WA TAIFA isiingiliwe na ulinzi wa watu binafsi na mali zao. Hata hivyo wanaweza toa huduma hiyo kwa baadhi ya sehemu muhimu kwa kibali maalum pale serikali inapoona umuhimu kwa mfano miradi mikubwa ya umma ama kibinafsi itoayo mchango mkubwa kwa uchumi wa Taifa.
   
 14. M

  Masatu JF-Expert Member

  #14
  Dec 27, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ikiwa Ikulu watu wanafanya biashara mnashangaa Jeshi? Waacheni nao "wajiongezee" kipato! mnaaambiwa nchi ime switch onto auto Pilot mambo yanajiendesha wenyewe tu tusubiri landing ( kama tutafika )
   
  Last edited: Dec 27, 2008
 15. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #15
  Dec 27, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu, yaani ndio unawaongezea ufisadi. Kama hiyo Meremeta waliyoingia kinmyemela wamekula namna hiyo, sembuse hiyo miradi ambayo itakuwa rasmi!!! Kumbuka kuwa kutakuwa na uwezo mdogo sana wa kuingiza uchunguzi huko kisingizio kikiwa ni kilekile kuwa masuala nyeti ya kijeshi
   
 16. M

  Mkandara Verified User

  #16
  Dec 27, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mimi siona kosa hapa kama nimeelewa vizuri lengo ni kuwapa ajira vijana waliomaliza mafunzo ya ulinzi JKT. Kinachozungumziwa hapa ni ulinzi wa security iwe ktk malls, viwanda ama mashirika yanayohitaji mlinzi..Tumeona pia JKT wakijikita ktk sehemu nyingne za Ujenzi na ndivyo ilivyotakiwa JKT kuwa chombo cha Kujenga Taifa.

  Sasa badala ya kutumia Mgambo, JKT imejikita kama employment agency ambaye unaweza kuwaamini zaidi kwa sababu huyo kijana atakuwa amepitishwa na chombo hiki, kuna certain guarantee ya mafunzo na agent wake. Kama kutatokea tatizo la ulinzi JKT wanakuwa answerable badala ya mgambo ambaye atakimbia na hujui wapi pa kuanzia kufuatilia wizi huo.
  It sound good, hata Ulaya kuna security guards ambao wamepitia mafunzo ya awali ya Ulinzi na kupewa ajira na vyombo vinavyolinda.
   
 17. M

  Masatu JF-Expert Member

  #17
  Dec 27, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mkandara,

  Tatizo hapo hayo ma SMG na SAR yatakapoanza kusambaa ovyo kwenye malindo utakuta "zinakodishwa" na kuwekewa "hesabu" kila usiku ilhali mlinzi kabaki na rungu na asubuhi anarudisha silaha armourer
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Dec 27, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Masatu,
  Kweli maneno yako lakini sii JKT watakuwa na utaratibu wa kufuatilia hayo maanake nakumbuka enzi zetu JKT ktk Ulinzi mtu mmoja tu ndiye alikuwa na risas za kweli wengine tuna baruti tu. Kama agency nadhani watakuwa na uatatibu mzuri kuliko Mgambo ambao bado kiutendaji kazi hawakuwa na nafuu..
  Ni kweli ukitazama watu na mazingira yetu inahitaji sana askari Polisi lakini sioni tofauti kubwa kati ya Polisi na JKT ikiwa JKT wataweza kujenga upya kitivo hicho kwa malengo ya Ulinzi wa security.
   
 19. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #19
  Dec 27, 2008
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Mkandara ndio maana hatuendelei.
   
 20. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #20
  Dec 27, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  JKU wameanza kitambo mambo ya Ulinzi...Naona JKT watafanya vizuri zaidi
   
Loading...