Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,208
- 4,405
JESHI LA WABUGURUSI.
1)Awakarimu manani,mola wetu wa mbinguni.
Awape nyingi imani,na amani za nyoyoni.
Mzidi kumuamini,namumtie rohoni.
Jeshi la wabugurusi,lisonge mbele zaidi.
2)makamanda ni makini,wenye akili vichwani.
Jahazilo baharini,lipasua mawambini.
Na silaha mabegani,kalamuzo mikononi.

3)limekuwa darasani,kujifunzia shuleni.
Wengi wanalitamani,wapate mbinu makini.
Wakiliona hewani,wanaanza lala chini.

4)la kale tangu zamani,la wika hadi mjini.
Linaijali thamani,ya utunzi na nishani.
Wengi wanalithamini,wa bara hadi wa pwani.

5)lilete lulu nchini,lisambae duniani.
Afrika na marikani,asia na afughani.
Liende hadi shishani,comoro hadi sudani.

Shairi=JESHI LA WABUGURUSU.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallayninga@gmail.com