Jeshi la Polisi shughulikieni uhalifu huu mara moja

Boss la DP World

JF-Expert Member
Dec 12, 2021
1,997
7,546
Napenda kupongeza jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi kuwatimua vijana zaidi ya 400 waliokuwa wamekusanywa na Q NET wakipewa ndoto za utajiri wa haraka na wao kuombwa kiasi cha milioni 5 ili kutajirika.

Sasa iko hivi, hawa Q NET wana ka mtandao kengine wanakaita Rythim Foundation wamewakusanya watoto wa watu na wanapiga simu kwa wazazi na walezi wakiomba milioni 5 kwa kila mtoto ili wawape kazi yenye kipato kisichopungua milioni 1 kwa mwezi, hao watoto ni mabinti wa moto kidogo, kwa hiyo wakufunzi wanawatumia nyakati za usiku kama viburudisho murua huku wakiwaonesha picha za nyumba na magari ya kifahari kama alivyokuwa akifanya Ontario.

Kazi kwenu jeshi la polisi, watoto wamewehushwa huko.
 
Napenda kupongeza jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi kuwatimua vijana zaidi ya 400 waliokuwa wamekusanywa na Q NET wakipewa ndoto za utajiri wa haraka na wao kuombwa kiasi cha milioni 5 ili kutajirika...
serikali ipo wapi kufunga hawa watu?
 
Napenda kupongeza jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi kuwatimua vijana zaidi ya 400 waliokuwa wamekusanywa na Q NET wakipewa ndoto za utajiri wa haraka na wao kuombwa kiasi cha milioni 5 ili kutajirika...
bado hujawasaidia jeshi la polisi ilipaswa uwape trace, mahala walipo, majina yao na hata picha zao mana q net imeenea nchi nzima na dunia nzima
 
Wale watoto wanapata shida sana wanashindia biscuits eti wanawadanganya wengine kuwa maisha mazuri

USSR
Nashauri hao wahuni waongeze juhudi, maana watanzania hatuthaminishi kazi zaidi ya kutaka hela badala ya kujitoa kufanya kazi. Hivi wewe na akili nzima uambiwe eti utoe mil 5 upate kazi na unalundikwa sehemu kama zigo na hao ukute ni graduate wa chuo kabisa
 
Napenda kupongeza jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi kuwatimua vijana zaidi ya 400 waliokuwa wamekusanywa na Q NET wakipewa ndoto za utajiri wa haraka na wao kuombwa kiasi cha milioni 5 ili kutajirika.

Sasa iko hivi, hawa Q NET wana ka mtandao kengine wanakaita Rythim Foundation wamewakusanya watoto wa watu na wanapiga simu kwa wazazi na walezi wakiomba milioni 5 kwa kila mtoto ili wawape kazi yenye kipato kisichopungua milioni 1 kwa mwezi, hao watoto ni mabinti wa moto kidogo, kwa hiyo wakufunzi wanawatumia nyakati za usiku kama viburudisho murua huku wakiwaonesha picha za nyumba na magari ya kifahari kama alivyokuwa akifanya Ontario.

Kazi kwenu jeshi la polisi, watoto wamewehushwa huko.
Umeleta porojo badala ya kusaidia,ilitakiwa ueleze hao mabinti wamekusanywa wapi kwa maana ya Mtaa,Kata,Wilaya,Mkoa na hata namba ya nyumba
 
Nashauri hao wahuni waongeze juhudi, maana watanzania hatuthaminishi kazi zaidi ya kutaka hela badala ya kujitoa kufanya kazi. Hivi wewe na akili nzima uambiwe eti utoe mil 5 upate kazi na unalundikwa sehemu kama zigo na hao ukute ni graduate wa chuo kabisa
Graduate wapo pia mkuu sijui wamelishwa nini
 
Back
Top Bottom