Jeshi la Polisi: Sheikh Ponda ajisalimishe Polisi ndani ya siku 3, vinginevyo hatokuwa salama

Siyo wa kwanza. Usimsahau Askofu Niwemugizi alisema Katiba Mpya pekee itamaliza shida zote hizi, yuko tayari aitwe mchochezi. Akaja Askofu Munga akalaani shambulizi la Lissu akasahau ya Tanga Jimboni kwake. Huyu ni wa tatu aisee, ila naye naona kasahau mauaji ya kwao Kibiti hapahapa Pwani.
Nn kinasababisha hao wengine wasiitwe polisi?
 
Sasa kwa wanasiasa waende likizo,waandishi habari andika za ufisadi zaidi,waliobaki,tukachape kazi zetu zaidi kwa faida ya familia zetu, mpo hapooo????!!!!
 
Sipendi majina ya wengi KTK jamii forum, tumia majina halisi,shauri kwa uhalisi,tumia lugha ya staha,Tafadhali sana!
 
Sipendi majina ya wengi KTK jamii forum, tumia majina halisi,shauri kwa uhalisi,tumia lugha ya staha,Tafadhali sana!
"Nyani haoni kundule" mbona jina lako humu sio halisi? umejiunga juzi tu halafu unataka kuleta masharti! Kama hupendi majina ya wengi unafata nini humu?
 
N


Kamanda Mambosasa akijibu swali la Mwandishi kutoka gazeti la Uhuru, kwanini Polisi walivamia Mkutano wa Shekhe Ponda jana, Kamanda amesema ni kwa makosa ya uchochezi na kuwa anatakiwa aripoti Polisi ndani ya siku tatu ili hatua stahiki zichukuliwe.

Jana Jumatano Sheikh Ponda alitumia lugha ya uchochezi alipozungumza na waandishi wa habari na kutoa kejeli kwa Serikali.

Amesema kukimbia kwake hakutasaidia chochote ni vyema ajitokeze kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu suala hilo.

“Sheikh Ponda alikuwa anajua kwamba anafanya kosa kwa sababu aliwaambia waandishi waje saa nne yeye akawapigia baadhi waje kabla ya saa nne,’’ amesema.

Kamanda Mambosasa amesema baada ya askari kufika eneo ambalo Sheikh Ponda alikutana na waandishi wa habari, waliwachukua waandishi na wafuasi wake kwa mahojiano. Baada mahojiano na Polisi kujiridhisha waliwaachia huru.


---Maoni Yangu---
Nilimsikiliza Sheikh Ponda jana sikuona uchochezi wowote.



Ningekuwa mimi sheikh ponda ningeenda Syria kupigana jihadi " nikifa niende peponi" sio kuingia kwenye ukafili wa siasa za watu weusi. acha njaa ponda mwogope mungu..KAFILI HAWEZI KUWA RAFIKI ---KORAN
 
Anatumia kofia ya dini kuchochea. Dini msikitini sio kwenye press conference atanyooka tu. Magufuli rudisha nidhamu iliyopotea hakuna Uhuru usio na mipaka muonyesheni mipaka huyo sheikh
Kwahiyo nje ya msikiti/kanisa hakuna dini?
Nje ya msikiti/kanisa wewe siyo muislam/mkristo?
 
kwenye hiyo clip suala la gari lililotelekezwa ndio ameniacha hoi!hilo gari halina wamiliki?maana baada ya majambazi kkukimbia ikawa ndio mwisho wa story!
Hawa watu ni wa kuwaskiliza (kama una muda) na kuwaacha
 
Mkuu angekuwa wa kukamatwa angeshakamatwa. Hapo ndiyo unaona undumilakuwili wa hii Serikali dhalimu. Huyo jambazi muro katamka hadharani kutaka Lema na Nassari wauawe lakini polisiccm hawana sababu ya kumkamata ila Sheikh Ponda kuongea kuhusu Lissu ni kosa kubwa nchi hii! Ndiyo matatizo ya nchi kuongozwa na kidikteta uchwara.
Wapi Muro kasema wauawe?
 
N



Ningekuwa mimi sheikh ponda ningeenda Syria kupigana jihadi " nikifa niende peponi" sio kuingia kwenye ukafili wa siasa za watu weusi. acha njaa ponda mwogope mungu..KAFILI HAWEZI KUWA RAFIKI ---KORAN
Ungekuwa! Its too late!
 
Dini haiongelewi kwenye press conferences.
Alikuwa anaongelea kuhusu dini? hebu kaangalie tena ile video uje kujenga hoja upya maana inaelekea hata maana ya dini hujui na hakuna sheria inayokataza dini kuongelewa katika press conference kwa mujibu wa katiba ya Tanzania.Mara ngapi Mufti wa bakwata anatangaza katika press conference maswala ya sikukuu za Eid au sala ya Eid kitaifa itasaliwa wapi au hayo siyo dini?
 
Back
Top Bottom