Jeshi la Polisi: Sheikh Ponda ajisalimishe Polisi ndani ya siku 3, vinginevyo hatokuwa salama

Kamanda Mambosasa akijibu swali la Mwandishi kutoka gazeti la Uhuru, kwanini Polisi walivamia Mkutano wa Shekhe Ponda jana, Kamanda amesema ni kwa makosa ya uchochezi na kuwa anatakiwa aripoti Polisi ndani ya siku tatu ili hatua stahiki zichukuliwe.

Jana Jumatano Sheikh Ponda alitumia lugha ya uchochezi alipozungumza na waandishi wa habari na kutoa kejeli kwa Serikali.

Amesema kukimbia kwake hakutasaidia chochote ni vyema ajitokeze kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu suala hilo.

“Sheikh Ponda alikuwa anajua kwamba anafanya kosa kwa sababu aliwaambia waandishi waje saa nne yeye akawapigia baadhi waje kabla ya saa nne,’’ amesema.

Kamanda Mambosasa amesema baada ya askari kufika eneo ambalo Sheikh Ponda alikutana na waandishi wa habari, waliwachukua waandishi na wafuasi wake kwa mahojiano. Baada mahojiano na Polisi kujiridhisha waliwaachia huru.

---Maoni Yangu---
Nilimsikiliza Sheikh Ponda jana sikuona uchochezi wowote.

Nilimsikiliza Sheikh Ponda pia nimeona hotuba yake haifai, haifai, haifai! Speech yake ina kila virutubisho vya uchochezi. Kwa kweli Kamanda Sirro kuna haja ya kuwaelimisha wakuu wa dini wafanye kazi hao hasa ya kufundisha watoto kusoma Qu'ran na mafundisho mema na sio kudandia siasa. Waache wanasiasa wafanye kazi ya Siasa. Sheikh Ponda huko unakokwenda siko.
 
huyu mzee hana shule hajui anchofanya madhala yake makubwa baadae. Achana na siasa mzee endelea na dini
 
Ekasi Kabisaaa! huyu mzee is a big problem, an epidemic to the society! a brainwasher! anatakiwa aendelee na dini msikitini akiwahamasisha waumini waishi maisha ya upendo na amani, akitatua matatizo ya wanandoa, mashehe wengine waliojaa pepo baya wanaowalawiti watoto, wabakaji etc na sio kutumia social media kuhamasisha watu kwenye njia ovu. Awaache polisi wafanye kazi yao! Amesikia wapi uchunguzi wa kina unachukua mwezi mmoja tu? IGP Sirro si mjinga kusema waache vyombo vinavyohusika vichunguze. Uchunguzi unaweza kuchukua hata miaka mingi. Aangalie series za Discovery DX aone kesi ngapi huko marekani za mauaji ziko pending hata miaka 20 na zaidi? zingine ushahidi unapatikana baada ya miaka tele na jalada linafukuliwa baadae . Sasa yeye anataka IGP Sirro akurupuke halafu wamwandame Kamanda wa watu kuwa amekurupuka? Ponda ache kuponda Amani ya nchi! Tumekuchoka!
 
Polisi inajua au imetafakari madhara yatakayotokana na kukamatwa kwa huyu mtu! Kwani kumpigia simu haitoshi mpaka muutangazie umma hizi shule za ukamanda mlisomea wapi? Nyie haya

Ana nini mpaka asikamatwe? Kwa nini apigiwe simu? yeye alipoita Press Conference alidhani huko ni sawa? kama alikuwa na nia safi si angeenda kwa IGP Sirro kimya kimya na akatoa maoni yake? Polisi imefanya vema kuutangazia umma kuwa afike Kituoni akajieleze. Akiachwa awe anabwabwaja tuu basi tutafika mahali nchi haitatawalika kwa kuwa kila mtu akisema yeye ni Bisho, au Shehe atakuwa anaogopwa kuuliza dhamira yake ya kuutangazia umma jambo hili au lile ni nini. Ifahamike ni mambo yanayopuuzwa madogo madogo ndiyo yanayohatarisha Amani ya nchi. Amani ikishapotea hakuna atakaeweza kuturudisha kwenye mstari. Kwa hipo Ponda akibwabwaja , Polisi ifanye kazi yake ya kumwita na kumhoji kiunagaubaga. Ndiyo kazi ya Polisi kuhakikisha Usalama wa raia haijalishi uwe na kofia ya aina gani.
 
Nani kachocheka na amechoka mpaka degree centigrade ngapi?

Mzee wa watu kaongea fact tupu na kwa unyenyekevu wa hali wa Hali ya juu bado eti Police wanamtaka!

Kweli upolisi ni kimbilio la wale wasovipanga!

Tangu zamani mtu aliyekuwa anajiunga na Jeshi la Polisi ni mtu aliyeshindwa kwa maana ya kufeli elimu ya darasani...!!Mpaka leo iko hivo...!!
Polisi anatakiwa awe ni mtu asiyeweza kufikirisha ubongo wake, ni mtu anayepokea amri tu kwa kupewa kazi za hovyo hovyo na kutekeleza bila kuhoji au kudadisi hata kama ni jambo la kiipumbaf...!!
Haiwezekani eti kwa vile Sheikh Ponda alienda kumsalimia Lissu ambaye hata Serikali imesema iko tayari kuhakikisha anatibiwa popote duniani lakini leo inataka kumkamata mtu aliyetoka kumpa pole Lissu...huu ni ujinga ulipitiliza.

Kwa hiyo ni yaleyale ya Kamanda wao daraja Ziro anaposema kila akimwona Dereva wa Lissu kwenye Picha eti anawaka kwa hiyo ndiyo wanamtaka sana kana kwamba yeye ndiye aliyempiga Lissu risasi 38...!! Halafu mtu huyuhuyu daraja Ziro anapiga marufuku watu wasizungumzie habari za Lissu.....!!!Huu ni zaidi ya uzezeta kwa kweli.
 
jicho la bundi.. You are 100% true.. main problem is lack of knowledge. We are wasting a lot of time for unnecessary things in life.. we are all here for the purpose so let us serve that purpose.. nashanga umri wa huyu anayejihita sheakh ni muda wakuwa karibu sana na mungu wake, umri umeshakwenda very soon his number will be called by GOD, atamwambia nini mungu, NADHANI HANA LA KUFANYA WATU WENGI AMBAO HAWANA YA KUFANYA WANATABIA HII.
 
Nyando.. kwenda Nairobi sio kutokuwa na njaa, huyu mzee anaonesha ananjaa toka lini sheakh akaingia kwenye siasa?,, hana la kufanya ktk familia yake?..

Tangu zamani mtu aliyekuwa anajiunga na Jeshi la Polisi ni mtu aliyeshindwa kwa maana ya kufeli elimu ya darasani...!!Mpaka leo iko hivo...!!
Polisi anatakiwa awe ni mtu asiyeweza kufikirisha ubongo wake, ni mtu anayepokea amri tu kwa kupewa kazi za hovyo hovyo na kutekeleza bila kuhoji au kudadisi hata kama ni jambo la kiipumbaf...!!
Haiwezekani eti kwa vile Sheikh Ponda alienda kumsalimia Lissu ambaye hata Serikali imesema iko tayari kuhakikisha anatibiwa popote duniani lakini leo inataka kumkamata mtu aliyetoka kumpa pole Lissu...huu ni ujinga ulipitiliza.

Kwa hiyo ni yaleyale ya Kamanda wao daraja Ziro anaposema kila akimwona Dereva wa Lissu kwenye Picha eti anawaka kwa hiyo ndiyo wanamtaka sana kana kwamba yeye ndiye aliyempiga Lissu risasi 38...!! Halafu mtu huyuhuyu daraja Ziro anapiga marufuku watu wasizungumzie habari za Lissu.....!!!Huu ni zaidi ya uzezeta kwa kweli.

Uwe na soni unapoandika upuuzi wa aina hii!! Polisi wanafanyakazi nzito mno na hawastahili hata kidogo unnecessary criticism ya aina hii. Wana mishahara duni, wana makazi duni, na hata wakiretire hawana cha kuonyesha mbele ya jamii kwa miaka yao yooote waliyofanyakazi wengi kulinda usalama na mali ya watu wenye utindio wa ubongo kama wako! Polisi hawakuokotwa barabarani. Hivi ni nchi gani unayoifahamu Polisi hapewi amri na mkuu wake? Amri ndiyo nidhamu ya polisi na jeshi la kujenga taifa. Polisi hawauzi mboga kujiamulia kuwa wafanye itakavyo. Kunasheria lazima zifuatwe. Na hiyo ndiyo heshima ya Polisi ulimwengu mzima. Hivi huyo Ponda tangu lini amekuwa karibu na watu ambao yeye akiwaona ni ma-Kafir? Ukistaajabu ya Mussa utaona ya Kirauni! hivi inakujia akilini leo Shehe mwenye sigida anasafiri hadi Nairobi eti kumtetea Lissu wakati kuna waislamu kibao wanaotaka huduma ya kuombewa mahospitalini? hiyo pesa ya kwenda kumwona mgonjwa mmoja tu Lissu si angenunua Juzuu akawapa watoto wa kiisamu kwenye misikiti mingi tuu? Kwanini anachezea pesa za Waislamu namna hiyo? Muislamu wa aina gani yeye? Ponda hebu rudi nyumbani kalee wajukuu. Allah anauona upumbavu unaoufanya!

Humu JF kuna watu wenye ubongo a

uislamu unatufundisha
1.kuamrisha na kusimamia mema i.e kupigania kutetea haki za wanyonge ' wanaoonewa'
2.kukataza au kuondoa mabaya

Kibinadamu na kidini sheikh katekeleza wajibu wake .

Dini haijawaji sema siasa haina.
Ni Nyerere tu na kutoelewa issue za dini akapandikiza fikra potofu za ' usichanganye dini na siasa' ili kuwadhibiti waislamu wasiingie kwenye siasa :awatawale: kirahisi
Alifanikiwa
Wakati yeye(Nyerere) kamweka padri kwenye TANU ili ............... soma kitabu cha sivalon je hapa hakuchanganya siasa na dini???

Na ndio inayoendeeeleeeea hadi sasa.
 
Dini ni mfumo wa maisha unaofatwa na watu
Siasa ni fani ya kuongoza watu kutoka Hali duni kwenda hali Nzuri au bora

uislamu unatufundisha
1.kuamrisha na kusimamia mema i.e kupigania kutetea haki za wanyonge ' wanaoonewa'
2.kukataza au kuondoa mabaya

Kibinadamu na kidini sheikh Ponda katekeleza wajibu wake kumjulia hali Lissu mtanzania anayetibiwa nairobi

Dini ya uislam haijawaji sema siasa haina.
Siasa ipo Katika uislamu kwasababu kuna uongozi na Mungu ametuleta ili tuwaongoze wasio waadilifu.

Ni Nyerere tu na kutaka kuwagawa watu akapandikiza fikra potofu za ' usichanganye dini na siasa' ili kuwadhibiti waislamu wasiingie kwenye siasa :awatawale: kirahisi
Alifanikiwa
Wakati yeye(Nyerere) kamweka padri kwenye TANU ili ............... soma kitabu cha sivalon je hapa hakuchanganya siasa na dini???

Na ndio inayoendeeeleeeea hadi sasa.
 
uislamu unatufundisha
1.kuamrisha na kusimamia mema i.e kupigania kutetea haki za wanyonge ' wanaoonewa'
2.kukataza au kuondoa mabaya

Kibinadamu na kidini sheikh katekeleza wajibu wake .

Dini haijawaji sema siasa haina.
Ni Nyerere tu na kutoelewa issue za dini akapandikiza fikra potofu za ' usichanganye dini na siasa' ili kuwadhibiti waislamu wasiingie kwenye siasa :awatawale: kirahisi
Alifanikiwa
Wakati yeye(Nyerere) kamweka padri kwenye TANU ili ............... soma kitabu cha sivalon je hapa hakuchanganya siasa na dini???

Na ndio inayoendeeeleeeea hadi sasa.

MBM, Kuna kupigana na kupigania haki. Anachofanya Ponda ni kupigana na sio kupigania.

Uislau ni usafi, hasa tabia ya unadhifu, staha. Tabia ya usafi ni tabia iliyo na athari sana kwa watu, ni tabia yenye mvuto mkubwa kiasi kwamba kwa kulijua hili baadhi ya watu hutumia unadhifu wao kufikia malengo yao mbalimbali.
Usafi tunaouzungumzia waislamu hapa ni ule usafi wa ndani, usafi wa moyo ambao unatokana na itikadi safi na sahihi. Itikadi ya kuamini Mungu mmoja asiye mfano, mwana wala baba. Matunda ya usafi huu huonekana kwa tabia njema zinazoupamba utu. Uaminifu, ukweli, kujiheshimu, kutojivuna, kutokuwaringia watu, kuwasaidia wenye shida, kuwatendea wema watu wengine hasa waislamu wenzako, kuwafikiria watu wengine vizuri na tabia nyingine zote nzuri ni matokeo ya usafi huu wa ndani.

Usafi wa aina hii tu ndio utakaoiweka dunia katika hali ya usalama na amani. Aidha, kukosekana kwake ndiko kulikoitumbukiza dunia katika machafuko na misukosuko isiyokwisha ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Usafi hapa nazungumzia usafi wa kuacha mihemko na kufuata upepo wa yule kasema nini basi na mimi nadandia hapo. Nanyoosha kidole tuuu ili mradi nisikike. Hapa Ponda amedandia treni ama kwa makusudi, ama kwa kutumiwa na watu wachache wenye tamaa ya kushika madaraka at all cost. Hapa Ponda amechemsha. Ponda kama ni kuelimisha angeweza kufanya hayo ayatakayo kwa staha. Huo ndio Uislamu. Siyo statements chonganishi zinazoegemea upande mmoja. Mimi ni Muislamu, Huko Ponda Akaa! Sio uislamu huo. unatupotosha. Nenda kawanunulie watoto Juzuu wasome dini yao, watoto wa kiislamu wanashida nyingi hawataki porojo za kisiasa. Mwache Mbowe afanye siasa yake. Ndiyo ajira yake. Ndiyo karama yake. Wewe baki njia kuu. Allah anakuona Shehe wangu. Anakuona! Uzee unakuenda kubaya, huko siko!
 
Kamanda Mambosasa akijibu swali la Mwandishi kutoka gazeti la Uhuru, kwanini Polisi walivamia Mkutano wa Shekhe Ponda jana, Kamanda amesema ni kwa makosa ya uchochezi na kuwa anatakiwa aripoti Polisi ndani ya siku tatu ili hatua stahiki zichukuliwe.

Jana Jumatano Sheikh Ponda alitumia lugha ya uchochezi alipozungumza na waandishi wa habari na kutoa kejeli kwa Serikali.

Amesema kukimbia kwake hakutasaidia chochote ni vyema ajitokeze kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu suala hilo.

“Sheikh Ponda alikuwa anajua kwamba anafanya kosa kwa sababu aliwaambia waandishi waje saa nne yeye akawapigia baadhi waje kabla ya saa nne,’’ amesema.

Kamanda Mambosasa amesema baada ya askari kufika eneo ambalo Sheikh Ponda alikutana na waandishi wa habari, waliwachukua waandishi na wafuasi wake kwa mahojiano. Baada mahojiano na Polisi kujiridhisha waliwaachia huru.

---Maoni Yangu---
Nilimsikiliza Sheikh Ponda jana sikuona uchochezi wowote.

ww HUKUONA UCHOCHEZI haimanishi UCHOCHEZI HAUPO
 
Back
Top Bottom