Taarifa zilizotolewa kuhusu madai ya
“mwanajeshi wa Marekani” kukamatwa Tarime zimeibua maswali mazito kuliko majibu. Kutaja jina lisilo la kawaida kama
Onkuri Ongeta.
Pamoja na picha zinazomuonyesha mtu huyo akiwa amejipamba kwa pete kama Mganga wa Kienyeji na mavazi yasiyoendana na mafunzo ya kijeshi, koti kuubwa kama Mc Mboneke, haya yanatosha kulifanya jambo hili lionekane kama maigizo yaliyopitiliza.
View attachment 3506344
Zaidi, kutumia mabomu ya machozi ya aina
CS M68, ambayo hutumiwa na polisi, si jeshi la Marekani, kunadhoofisha kabisa hoja iliyotolewa.
Tanzania ya leo ina wananchi wanaodai ukweli. Vyombo vya dola vinapaswa kuheshimu umma na kutoa taarifa sahihi bila utani wala propaganda.