Jeshi la polisi mkoani singida mmeonyesha ukomavu sasa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jeshi la polisi mkoani singida mmeonyesha ukomavu sasa.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MADORO, Jan 11, 2012.

 1. M

  MADORO Senior Member

  #1
  Jan 11, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 199
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Jeshi la Polisi Mkoani Singida, limekataa kutii amri haramu ya Mkuu wa Mkoa huo ya Kumkamata Mwenyekiti wa Baraza la vijana Mkoa wa Singida, ndugu Josephat Isango hadi pale Mkuu huyo atakapofika Kituo cha Polisi mwenyewe kufungua mashtaka dhidi ya Mwenyekiti huyo kuwa alimkashifu katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Jumamosi katikati ya mji wa Singida. Mkuu huyo wa mkoa aliamrisha kijana huyo akamatwe lakini polisi wamekataa wakisisitiza kuwa anayetuhuhmiwa alizungumza hoja zenye ushahidi hivyo polisi wangeumbuka kwa kumkamata, kama Mkuu wa mkoa yeye anaweza kujibu hoja zake basi alitakiwa afike kituo cha polisi afungue jalada. Amesita kufanya vile kwa siku mbili sasa. Tunawapongeza jeshi la polisi kwa kujitegemea kimawazo.
   
 2. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,147
  Likes Received: 1,242
  Trophy Points: 280
  Bora waote akili mpya kwani tuko kwenye mwaka mpya pia
   
 3. M

  Molemo JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Alimtuhumu nini?
   
 4. Ikwanja

  Ikwanja JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,988
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  pole pole wataelewa na wa mikoa mingine
   
 5. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2012
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,420
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Tunaelekea pazuri...taratibu tutaongezeka, na mafisadi watakosa pa kutokea.

  Amuchi ahumba va khaitu!
   
 6. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Isango alimtuhumu nini huyu mchumia tumbo anaye taka kutumia madaraka vibaya ? Hebu wekeni alicho kisema tuanze kuzama kwa undani tafdahali
   
 7. D

  Dopas JF-Expert Member

  #7
  Jan 11, 2012
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  tuombe isiwe akili ya muda tu... Wakiendelea hivyo Nchi itakombolewa
   
 8. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #8
  Jan 11, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  au aliongelea ile kampuni ya pavico ltd(parseko visenti cone ltd)iliyopewa tenda ya kukusanya taka mjini singida?
   
 9. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #9
  Jan 11, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,992
  Likes Received: 2,649
  Trophy Points: 280
  Ni ajabu na kweli.
   
 10. K

  KWA MSISI Member

  #10
  Jan 11, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa hilo ninasema hongera jeshi la polisi mkoani Singida.
  Wadau mliokuwepo Singida kwenye mkutano huo wa hadhara hebu tupeni data ambazo Mh.T.Lisu aliuambia umati wa wasikilizaji kuhusu tuhuma kadhaa zinazo mkabiri Mkuu huyo wa Mkoa wa Singida pamoja na magamba wenzake.
   
 11. I

  Isango R I P

  #11
  Jan 11, 2012
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 295
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nilichosema katika mkutano wa Singida,ambacho ndicho natuhumiwa kuwa ni kumkashifu Mkuu wa Mkoa wa Singida ni Hiki kwa ufupi: Na ambacho ndicho anataka kusema nikamatwe. Siogopi, nitasema iwe usiku,mchana, asubuhi au hata jioni. Iwe pembeni Juu chini hata pembeni na kando kando,Msimamo wangu ni kuwa:
  [h=1]Tunalalamika kuwa Mteule huyu ametufanyia machukizo kumi yafuatayo:[/h][h=1] [/h][h=1]Kwanza Ni Mkuu wa Mkoa anayetoa matusi hadharani. Kutukana wanakijiji Mteule huyu wa Rais alipanga safari tarehe 24/2/2009, hadharani kweupe pe, mbele ya wanakijiji akawa na ujasiri wa kimadaraka ukatoa matusi, huku ibara ya 12 (2) ya katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayodai “Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake’ ibara hii ilikuwa ikiendelea kumkodolea macho ya mshagao. Ibara jirani nayo haikusita kumjia kumshangaa. Ibara ya 16 (1) ikamwaambia kuwa kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi ya nafsi yake, maisha yake binafsi……………..”. suala la usawa mbele ya sheria na liliwekwa wapi? Mkuu wa Mkoa wa Singida kwanini ulitoa matusi hadharani? Unadhani kuomba radhi kunakuondolea hatia? Kama uliomba radhi mbona hujutii vitendo vile unaendelea kuwakashifu waliokusababisha ukaombe radhi?. Hivi Kikwete kwanini unatupatia Mkuu wa Mkoa anayetoa matusi? Mkuu wa mkoa anayetuona sisi ni ‘washenzi, na wapumbavu”[/h][h=1] [/h][h=1]Huyu ni mteule wa Rais anayetumia madaraka vibaya, na rasilimali za watanzania. Mteule huyu alipanga safari tarehe 31/3/2009, siku ya Jumanne kwenda kuongea na Halmashauri ya kijiji ili kupanga nao kuja kuongea na wanakijiji kuomba radhi kwa matusi yake. Na ndipo msafara wa mashangingi mengi tarehe 2/4/2009, ulifika kijijini eti Mkuu wa mkoa kuomba radhi. Yaani tunatumia kodi za watanzania kwenda vijijini kuomba radhi kwa ajili ya matusi yaliyotolewa na mtu kwa kiburi chake. Vipi mteule huyu?[/h][h=1] [/h][h=1]Chukizo la Pili, Mteule huyu, Mkuu wa Mkoa wa Singida, anaingilia hata michakato ya uwekezaji kitaifa. Aibu. Kituo cha Taifa cha uwekezaji (TIC) kilitoa cheti cha kivutio kwa wawekezaji wa Umeme wa Upepo katika mkoa wa Singida. Cheti kinaonyesha kuwa uwekezaji ungefanyika Kijiji cha Kititimo na Kijiji cha Unyambwa. Cheti kilitolewa tarehe 25 Agosti 2008. Ilikuwaje Mkuu wa Mkoa tarehe 20 Agosti 2009, ofisi yako ikatoa barua yenye kumb. Na. AB.457/457/O2A/194 ukaelekeza tofauti na ilivyotolewa na TIC? Mkuu wa Mkoa ana mamlaka gani kisheria kuingilia michakato hiyo ya uwekezaji na kubadili maeneo yaliyoelekezwa?. Mteule huyu jamani. Mteule huyu alipata wapi ruhusa ya kuitisha kikao ili agawe ardhi ya watu wa Singda tarehe 29/April/2009? Mbona hakushirikisha wanakijiji au hata madiwani na wabunge wao? Aliitisha kikao hicho yeyé kama nani kwa ardhi ya wanasingida? Mteule wako huyu Kikwete.[/h][h=1] [/h][h=1]Chukizo la tatu, Mkuu wa Mkoa huyu hana aibu, amemwingiza mkenge Mkuu wa nchi. Rais anahutubia taifa kila mara kuwa uwekezaji umekaribia, kumbe anapewa data za uongo na Mkuu wa Mkoa. Sasa tumuulize Rais hivi Umeme unaouhubiri katika Televisheni na katika magazeti utafanyika kijiji gani? Hebu taja? Mbona Kampuni inataja eneo tofauti, Mkuu wa Mkoa anatoa barua tofauti, Mkurugenzi ambaye ndiye msemaji halali wa maeneo anasema hakuna eneo. Aibu gani hii Kikwete na mteule wako? Ninaanza kutengeneza manati kusubiri kamati teule ya Bunge ambayo sitakubali ije kuchunguza ujinga huu ambao tunauweka wazi mwanzoni, ila viongozi wa Taifa na wateule wenu mnajidai ‘mbumbumbu’. Aibu!. Rais tunapoandika kuwa hapa unadanganywa kwanini hufuatilii, hivi na wewe na wasaidizi wako sio makini? Mbona tunakusaidia. Unataka tukusaidie vipi zaidi?[/h][h=1] [/h][h=1]Chukizo la nne; Kitendo cha Mkuu wa Mkoa kujigeuza kuwa mzoa taka wa Manispaa ya Singida. Kitendo cha Mkuu wa Mkoa kujidai kuwa anahitaji pesa zetu za malipo ya mwezi kwa kibarua cha kuzoa taka. Huyu ndiye msimamizi anayetakiwa asimamie wafanyakazi wengine, lakini haridhiki na kazi ya kusimamia anaamua naye afanye pamoja na wengine ili apate posho mbili. Hapa ilikuwaje? Je ni kwa sababu ulijua huwezi kupingwa kuchukua zabuni ya kuzoa taka? Kwanini zabuni hiyo haukushindanishwa na watu wengine? Kwanini waliokuwa na zabuni hiyo kabla ya kampuni yako kuchukua hawajalipwa mpaka sasa, ila wewe uliyechukua baadaye umeshalipwa? Pesa za kukulipa wewe zilitoka wapi na kwanini wengine wanaodai Manispaa hawalipwi? Watasimamiwa haki zao na nani wakati na wewe umejipanga kudai zile za kuzoa taka? Kikwete, mteule wako huyu![/h][h=1] [/h][h=1]Chukizo la Tano: Baada ya kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi ya kuzoa taka, ambayo pia ni aibu mimi kukutaja kuwa uliamua kuifanya. Mtoto wako alilazimisha vijana wa Singida kufanya kazi bila malipo, kwa shinikizo katika mazingira magumu, walipokataa aliwamwagia kitu kinachosadikiwa ni sumu. Walienda polisi wakapewa fomu za matibabu (PF 3). Mganga ameshathibitisha kuwa walimwagiwa sumu inayosababisha wao kubanwa kifua, kuwashwa koo. Tunasali wasife, au wasidhurike zaidi. Lakini mbona mpaka sasa kijana wako hajatiwa hatiani? Kesi yake ni namba ngapi mbona hata polisi hakuna RB? Huu ndio mfano tunaopaswa kufuata wa kutii sheria bila shuruti? Mteule unatufundisha nini?. Siku moja ng’ombe wako alikufa ghafla uliagiza polisi wafanye uchunguzi, hivi inakuwaje kwa ubinadamu wa ndugu zetu walioathiriwa na sumu iyomwagwa na mtoto wako mteule? Unatufundisha nini?

  Josephat Isango
  [/h][h=1] [/h][h=1] [/h][h=1]Chukizo la Sita: Mteule unaelekea kuwa na tamaa ya kujichukulia maeneo tena kwa kulazimisha bila ridhaa. Ulitaka kujimilikisha eneo la Kindai Holding ili liwe ranchi, mihtasari ya vikao vya halmashauri inakulalamikia, madiwani wanakulalamikia. Lakini kwa kuwa wewe ni mteule. Huna hatia kweli? Au tuache kufuata sheria za nchi kila mtu aige jinsi wateule wanavyofanya?[/h][h=1] [/h][h=1]Chukizo la saba;Nimezaliwa miaka mingi iliyopita, sijawahi kusikia amri haramu ya kuzuia watu wasilime mahindi kama ulivyoamrisha. Sijawahi kusikia. Hivi waliopita kabla ya wewe hawajui kuliko wewe? Unataka kusema kweli wakaazi wote wa Singida wanaolima mahindi ni wajinga sana? Unataka kusema mikoa yote inayotegemea kuchukua mahindi Singida wanachukua kwa bahati mbaya? Soko la mahindi linalookoa wanachi wa Singida na mikoa jirani lipo ofisi za CCM mkoa, huko hujawahi kutembelea?. Kwa hili hata Kikwete akisoma hapa atakushangaa kwa kuwa anaijua Singida. Sasa uamuzi huu wa kukurupuka vile uliutoa usingizini? Mahindi yasilimwe Singida, tule nini? Tukale kwa nani? Yanayouzwa sasa Singida tunakopa kwa nani? Mteule jamani![/h][h=1] [/h][h=1]Chukizo la nane; unapingana wazi wazi na Viongozi hata wa CCM. Viongozi wa Chadema unawaita ‘kidudu mtu’. Tulitegemea viongozi wa CCM wangekuunga mkono hata katika sera haramu. Mwenyekiti wa CCM wa mkoa ameandika barua tarehe 1/12/2011, na inaonekana imepokelewa ofisini kwako tarehe 2/12/2011. Barua hiyo yenye Kumb Na. CMS/M.20/VOL.2/99. Tujiulize. Kama viongozi wa CHADEMA hukubaliani nao, wa CCM unapingana nao je unatekeleza ilani ya Chama gani Singida? Iliwezekanaje Mwenyekiti wa CCM ndugu Joramu Alute akakupinga kwa barua? Huwa hamna vikao vya pamoja kushauriana kama Chama? Na kama umepoteza mashiko mpaka viongozi wa CCM wanakulima barua, sioni busara kwanini usijiuzulu. Watakuwa wanakusindikiza kwa unafiki katika ziara zako ila sirini wanakupinga. Ufalme unaopingana wenyewe hauwezi kusimama imara.[/h][h=1] [/h][h=1]Chukizo la tisa: kwa sasa unaonekana kuwa mjasiriamali katika shughuli ambazo hatutarajii kuwa Rais alikuteua kuja kuzifanya. Unafanya kazi ya Siasa kuwafundisha watu kujua tofauti za CHADEMA na CCM badala ya kuwa msimamizi wa shughuli za serikali katika mkoa. Hili pia ni chukizo.[/h][h=1] [/h][h=1] [/h][h=1]Chukizo la Kumi, Unaonekana kuwa Dikteta, hufikii maamuzi ya pamoja na viongozi wenzako, wananchi, au viongozi wa siasa hata viongozi wa Chama chako. Maana ungekuwa unafanya majadiliano Joramu Alute, Mwenyekiti wa CCM asingekupinga. Kwa kuwa ni kazi ya CCM kubebana hata katika uovu, ameogopa kusema hadharani ndio maana amekuandikia barua kukustahi. Ila sisi wapekuaji wa jamii tunaweka mambo hadharani. Inatosha sasa Mzee, Kikwete akupumzishe kwa manufaa yetu. La akiendelea kung’ang’ania uendelee kutuangamiza hivi, basi damu ya wana Singida iwe juu yako na juu ya Kikwete katika mateso haya mkijua kuwa hamtutakii mema. Lakini nasi tupime kama tutaendelea kuvumilia haya kwa hasara yetu[/h]
   
 12. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #12
  Jan 11, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,947
  Likes Received: 1,272
  Trophy Points: 280
  acha ukabila wewe
   
 13. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #13
  Jan 11, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,947
  Likes Received: 1,272
  Trophy Points: 280
  @ isango, ukombozi gharama. Usikate tamaa
   
Loading...