Katika nchi yetu Jeshi la Polisi ni Taasisi kubwa ambayo imefanyakazi nyingi kubwa zilizolenga kulinda Usalama wa Raia na Mali zao. Mmekomesha Ujambazi maarufu kwa MTAJI WA MASKINI NI NGUVU ZAKE MWENYEWE.
Mmekomesha Uvamizi wa majambazi benki. Mmekomesha vitendo vya Uvamizi wa Vituo vya Polisi na dalili za Vitendo vya Ugaidi kule Kibiti na Amboni. Hongereni sana.
Lakini kuna matukio ambayo siku za hivi karibuni yameonekana kama fedhea kwa Jeshi.
1. RPC GEITA anatangazia Umma gari lake limeibwa matairi Usiku amelala! Unajiuliza RPC analindwa 24/7 anamiliki askari na silaha zote ndani ya Mkoa. Hao Vibaka wamefikaje kwenye makazi yake, wamepataje Upenyo, na intelejensia yake ilikuwa wapi?
Je, kulikuwa na hajja ya kututangazia huu uzembe? Unapotezea siku zinaenda unakuta na hii na. 2
2. RPC MULIRO wa Mwanza namuamini sana, yeye anakuja na tukio lingine la Uvamizi wa Benki ya NMB IGOMA wezi wamekata bati, wamevunja ceilling board wameingia ndani ya Benki wamevuruga Vijana wake wanakuja kustuka tooo late tukio liko mwishoni. Unajiuliza benki inalindwa na askari wasiopungua wawili 24/7 walikuwa wapiiii. Kuna dalili zote za Uzembe kwenye matukio ya aina hii.
Tumewaaacha Maaskari waingie kwenye Lindo na SIMU JANJA hakuna namna askari yuko bize na simu yake WhatsApp, Insta, JF amenogewa, Huyo siyo askari tena huyo ni Mtalii wa Mtandaoni macho yamepigwa mwanga wa simu haoniiii ni mwendo wa kunyang'anywa silaha kirahisi tu, wezi wataingia kirahisi tu.
Lakini unajiuliza hawa makamanda wanatangazia Umma haya matukio ili tujifunze nini? Kwamba askari ni wazembe, au hawana mbinu za kukabili Vibaka na wezi, ama Jeshi halichuji taarifa kabla ya kuweka wazi kwa Umma?
Mjitafakari kwa hayo haijakaa vizuri kabisa, ni Mtizamo tu lakini. Salute