Jeshi la Polisi Manyara linamshikilia mbunge Mary Nagu kwa amri ya Mkuu wa wilaya ya Hanang Sara Ally

radika

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
20,427
32,196
MARY NAGU.jpg

Mh. Nagu alikamatwa majira ya saa 11:00 jioni kufuatia agizo la mkuu wa Wilaya ya Hanang Sara Ally Msafiri kwa madai kuwa Mbunge huyo alitofautiana maagizo na mkuu huyo wa Wilaya.

Hata hivyo Mh. Nagu aliachiwa jana hiyo hiyo baada ya uongozi wa CCM Wilaya ya Hanang kuingilia kati kutafuta suluhisho la mvutano huo ambao haujaelezwa ulikuwa unahusu nini haswa.

====

Mbunge wa Jimbo la Hanang, mkoani Manyara Dkt Mary Nagu(CCM) na mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo waanashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani humo kwa amri ya Mkuu wa wilaya hiyo kutokana na sababu ya kushindwa kuelewana kiutendaji.

Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya Sarah Msafiri ameeleza kuwa ameagiza kukamatwa kwa Mbunge huyo baada ya kuchoka kumvumilia kutokana na kauli anazozitoa kwenye mikutano yake na wananchi akihamasisha wasishiriki shughuli za maendeleo.

Pia amemtuhumu Mbunge huyo kuwataka wananchi wasishirikiane naye jambo ambalo alidai ni sawa na kuwataka wananchi wasishirikiane na serikali kwa sababu yeye anasimama kama serikali

“Ni kweli tumemkamata na sababu kubwa ni kuhamasisha wananchi wasishiriki shughuli za maendeleo na pia anawataka wananchi wasishirikiane na Mimi wakati anajua Mimi nasimama kama serikali” -DC Msafiri
 
nagu-660x400.jpg

Wallah watendaji wa hiki chama wananipa raha hadi basi
 
Tatizo wameambukizwa kuwa kila wanalofikiri wao ni sahihi, ukipinga mawazo yao au fikra zao wanakuona adui, wewe kama mipango yako naona ni ya kijinga naanzaje kuifuata??? Kisa wewe mteule au?? uteule wenyewe hawakukaguliwa vyeti sasa naanzaje kufata mawazo yako kama naona hayafai???,
 
Back
Top Bottom